Wanawake wa Dar es Salaam mmenisikitisha na kunihuzunisha sana. Kujishebedua kote huko kwanini Ilihali mnalala mbavu za mbwa?

WITH UPDATES***

Kifupi mimi naishi countryside na huko Dar nilisoma tu mavyuo na hivyo mimi siku hizi huja kwa kupumzika na matembezi mafupi kwenda znz nk au kufanya deal moja mbili tatu kisha nasepa huku mikoani ambao ndio watu tunaoishi maisha tunaishi! no bughudha no stress na pilikapilika za maisha ya huo Dar.

Sasa bana mimi niko vizuri sana. Kifupi hela ninayo kifupi sijapungukiwa iwe mi ndinga au mijengo. Ila nikiwa Dar kwa kuwa napenda kuwa huru na kujiachia maana mimi huwa najiweka simple saana vyeo na cadre niliyonayo ukiniona huwezi dhani. Kifupi napenda kuishi maisha to the fullest.

Kuliko nipande uber au tax nikiwa Dar mm huwa napenda nipande daladala au mwendokasi kutegemea na uharaka wangu wa siku hiyo lakini haimaanishi sipand hizo vingine. Sasa kupanda Daladala huko ni kwa ajili nipate kujichanganya nione maisha ya watu na masumbuko ya binadamu jijini Dar. Kifupi nimeona watu Dar kila mtu stress kwa kumsoma tu uso na gestures zake. Maisha yanapiga watu saana Dar.

Sasa nirudi katika mada..mara nyingi nimekuwa nikiona mademu wa Dar katika Daladala au nikiwa posta au mwenge nk kule kwenye malls mbalimbali yaani mademu utamuona classic kama malaika...yaani mtoto mzuri alivojiweka utadhani anakunya katika choo cha dhahabu ila sasa jitahidi kuwajua utasikitika.

Nilishawahi fanya uchunguzi kama huu ila nikasema nirudie tena..kuna siku nilikuwa nimepanda Daladala kifupi nikamkuta du moja kwenye seat jiran kwanza nikamsalimu hakuitika alikua busy na simu mi earphones masikoni nini, yaani ukimuona Utadhani beyonce..ooh nikasema no sweat haina tabu nikaketi. Tukawa kimya mimi natafakari uturi ananukia yaani utadhani mtoto ametoka mbinguni.

Basi konda akawa anachukua nauli mimi nikampa elfu kumi note maana kiukweli huwa natembea na hela kama hizo tu..bas konda akasema wawili!? duh nikawaza nikasema okay wawili kata nikimaanisha na yule duh. Ifahamike yule Duh alikua busy na msimu wake ile wakati narudishiwa change ndo akawa kama ameona ni suala la nauli akawa kama anatoa yake nikamwambia usijali nimeshakulipia.

Akasema ooh realy?? why?? no way huna haja kunilipia mm nikamwambia no problem sisi binadamu tu niliona vema kufanya hivyo kwa wakati huo sahihi no strings attached na ajisikie amani. Akawa kama ananiangaliaa kunipimiaa kisha akasema ok thanks. Basi ukimya ukatanda tena ikumbukwe mimi nilikua nataka kwenda maeneo ya mlimani city ila jamaa angu fulani akaniambia mlimani city hakuna issue nimfate sijui wapi pale chini mkabala na mlimani city kunakuaga na karaoke nini panahappen sana. Basi nikawa nashukia pale kituo karibu na kwa kakobe.

Mara na yule du akawa anashukia hapo..nikasema kimoyo moyo hebu ngoja nirushe nyavu hata kama demu anaonekana mtoto wa kigogo. Basi nikashuka na yeye akashuka pale basi mimi sikuvunga nikavunja ukimya oh ni kumbe tunashuka kituo kimoja naona ni bahati sana kwangu!? akanigeuka akawa kama like what!? nani huyu ananiongelesha! ikawa kama alivogeuka kuniona mimi kama vile akawa anataka kusita na kuignore ila kifupi mimi kama nina charisma hata kama najiweka simple sana ila maduu wengi wakiniangalia napata sana kibali kwao yaani sikataliki. Yaani niko charismatic nilishaambiwa na wengi hata huyu hapo baadae. Basi akaona no sweat anijibu tu kwani shi ngapi!? basi akasema yah nashuka hapa...huku akiwa busy kama kuondoka.

Nikamwambia hey hunijui sikujui ila ningependa nikufahamu! akanijibu what!? what are you talking about! ikumbukwe mimi nilikua naongea kiswahili ila duh viingereza vingi bila yeye kujua hiyo lugha mimi ndo ya kwanza kuongea mpaka nilipofikisha miaka sita kurudi Tz na wazee. Mimi sikutaka ligi nikabaki na kiswahili...nikarudi ndio nahitaji kukufahamu najua uko busy na yako na mimi pia niko busy ila nahitaji nikufahamu ( huku nampa simu yangu aweke namba yake nimemuwekea kabisa moja kwa moja kwenye kusave contact.

Dem akawa kama ananitazama kwa dharau sio dharau yaani kama vile hanielewei na hanimalizi hivi. Ila kwa kuwa pale kituoni kuwa watu wengi na mimi nimejitoa ufahamu basi akawa kama automatic hivi amepokea simu yangu na kuweka namba yake...nikasema kimoyomoyo yeess..aliponikabidhi simu nikafanya kama kuhakiki namba kwa kumpigia kisha nikamwambia ya kwangu hiyo save na kumtajia jina.

UPDATE***

Basi baada ya hapo! yule mtoto akaniangalia kama ilivo kawaida yake kama kunipimia na kunitathmini hivi na mimi nikawaza haina shanapata ni make a move! basi nikanyoosha mkono kumpa mkono akawa kama anasita kidogo ila sijui alwaza nini bahati nzuri hakusita kabisa akatoa wake kuupokea wangu. Ni muhimu sana kutoa handshake ki kanuni na taratibu ni kitendo cha kiungwana na waungwana na wajanja lazima wafanye hilo maana katika handshake ni njia pia yakupendeza hisia. Basi kama vile hisia zilipenya kwa mtoto huku mimi nikimtabasamia nikamwambia natumai mwisho wetu utapelekea tuonane tena mara ya pili! Akajibu kwa kifupi tu Okay you wish! huku akawa kama kageukia pembeni.

Basi mdau wenu nikamwambia kwa heri hata hakujibu. Mimi huyo nikawa kama najivuta taratibu huku natafakari hili na lile na kuhusu huyu mtoto. Kifupi niwaambie huyu demu nakuambia ukimuangalia mara mbili mbili unaweza ogopa utamuanzaje maana ni classic kimuonekano hasaa! Tatizo mimi hao ni kawaida sana kwangu huwa siwaogopi najiamini nguvu zangu sana. Basi nikawa nimefika pale pale sijui wapi hapo chini karibu na mawasiliano tower na mliman inakuwa upande wa pili wa barabara. Nikamkuta chali angu ananisubiri.

Basi mimi huwa natumia tu redbull na maji kwa wingi sana situmii pombe ni kanuni zangu tu za maisha nimejiwekea. Basi kwa kuwa chali angu wa Dar ndio mwenyeji wangu pale, mimi nilimwambia tu awe huru kula kunywa chochote mimi nipo pale kupumzika tu kuona maisha na mihangaiko ya watu muhimu nipate nafasi za kuimba zakutosha karaoke maana ndo furaha yangu. Basi stori za hapa na pale muda unayoyoma tukaagiza chakula meza stori mingi mara kukutana na rafiki na rafiki wa rafiki basi kwa kuwa nilikua vizuri mfukoni hakuna mtu alokosa anachilohitaji. Mimi ndio niko hivyo napenda wengine wafurahi na sina mkono wa birika kabisa labda ndo maana sipungukiwi.

Basi mimi nikawa naimba karaoke watu walipiga shangwe kusifia maana kiukweli nina kipaji cha kuimba ila sijawahi waza kukifanyia kazi. Na mimi ni mzee wa nyimbo za pop, soul ...country na love songs za malegend. Basi nikawa naimba nyimbo ya Kenny Rogers Lady! ebana niliimba kwa hisia sana huku namvutia picha yule mtoto nilokutana nae nikiwish angekuwa hapo. Basi bana baadhi wa mademu na pale kulikua kuna mademu wakali watoto wengi wa Dar walikua hapo walikuja mpaka kunishika mkono kuja mezani kuona ni nani huyo anaimba!. Si nisishangae anakuja demu namgeukia ni yule nilokutana nae.

Duh alishtuka kidogo kushangaa anayekuja kumtuza ni mimi nilokutana nae saa kama nne tano zilizopita. Alikua ameshika savannah hivi hivyo alikua kama amevaa miwani tayari kiaina basi ndo ikamuondoa soni. Akasema woow is that you!? omg you are such an incredible singer! woow huku anamuita rafiki yake come meet him! he is my friend hata sikujua. Mimi niko namwangalia tu huku natabasamu akanitambulisha rafiki yake nikawa namshangaa kimoyomoyo maana alinichangamkia saana sikudhani pisi toto toto kama lile liko charming hivyo. Ila nikajiongeza kimawazo nikasema hii ni tabia ya mademu wa Dar hawaji hivi hivi mpaka uwe na kitu fulani tofauti hapo ndo utaona heshima. Basi nikawaambia mnaweza kutujoin meza. Basi rafiki zake wawili wakajoin.

Tukawa kama tupo watu saba pamoja na rafiki yangu na rafiki zake wawili. Wenzangu walikua high kistaarabu hivyo mambo yakawa yamechanganya. Vinywaji chakula nk mezani havikosekani. Mimi na clear bills. Nipo na yule dem tumeongea mengi saana nikijitahidi kumjua maana watu nao macho mengi yalikua meza yetu wakimuangalia huyo demu maana kiukweli ni bonge ya mashine. Ikafika mida ya saa saba hivi nikamwambia rafiki yangu mm nataka nisepe nikapumzike kulala kwa kuwa ni usiku aniite Uber! na mm huwa nikija Dar napenda kulala ile hotelini nina ndugu kibao ila moja hivi inaitwa La France Hotel. Basi kwa kuwa ni hapo karibu tu nikamwambia mtoto mimi naondoka nikashangaa ananiambia Baby tuende wote! duh nikasema mtihani huu naitwa beby! Nikwambia mimi naishi hotelini akasema nimpitishe kwake kwanza kisha sijui achukue nini kisha niondoke nae!

Aisee uber akaja akaitwa hao tukaondoka! na ilikua mitaa ya sinza hivi sio mbali saana nikasema no sweat twende. Wana jamii forum mtanisamehe kusema kuwa kiukweli nilipofika hapo anapopaita kwake mazingira tu niloyakuta nilisikitika saaana saaana yaani saana! kiukweli nilibaki katika uber sikutaka hata kushuka kwa sababu za kiusalama maana hiyo mitaa kwa kweli sikudhani hata chembe kuwa mtoto kama huyo ndiko anakotoka.

Yaani sijui hata nielezeje yaani ni abject poverty ya kiwango cha lami!. Ndugu zangu kweli nauchukia umasikini ila simchukii masikini napenda nieleweke hivyo ..yaani mahali alipongia ndo kusema chumba chake hakika hata sehemu hiyo banda la kuku wangu wanaishi zaidi ya hapo. Nilisikitika sana yaani kuwaza msichana kama yule maisha ya starehe barabarani kama Jenifer Lopez! lakini ndipo anapoishi!? niliishia kumuonea huruma sana hata ile hamu ya kuondoka nae ikawa imeisha. Nikawa nawaza ni jinsi gani nitaweza kumsaidia tu hata hali ya maisha yake halisia ibadilike. Nikawaza sana nikasema kweli ndo maisha ya mtu anakaa Dar haya!? yaani fulu ghetto life!

Basi akawa amerudi, kifupi nadhani zile pombe alizokunywa ndizo zilimpa kujiamini kuona poa tu mm kumleta mpaka kupajua anapolaza mbavu zake. Mimi nikawaza sio mbaya saa nane za usiku hizi acha tu niende nae hotelini kwangu ila hakika sitamgusa. Mimi ndo nipo hivyo nikisita jambo huwa sifanyi maana najua sana kuzuia tamaa zangu na kuishi kwa malengo. Nikawaza sana ni jinsi gani nitaweza kumsaidia tu kimaisha nikasema kwanza lazima niweze kumbadilisha mind set yake.

Nikifanikiwa hilo basi na maisha yake mengine yatabadilika. Tukafika hotelini nikapanda juu pale kwa room yangu niko na yule duh. Yaani kufika tu akakimbilia bafuni kuoga! mimi huwa napenda sana kuwatreat watu waliokunywa pombe kuwa baada ya kunywa pombe wale chakula. Hivyo nilikuwa nimemunulia kuku nikamfungia kwa foil paper kama take away na juisi.

Mimi kama kawaida na redbull yangu na maji yakutosha. Wakati anavua nguo kuoga kiukweli nilitaka kama kuanza kusahau shida zake kifupi demu kaumbika jamani hapana bonge ya dem akachukua taulo huku ananiambia you are such a guy with charm ..nashangaa nimekuwa mrahisi hivyo kwako! you are charismatic indeed!. Mimi nikamwambia yote heri ilipangwa haya yatokee. Kifupi ninachowapendea wanawake wa Dar wako straight forward hapo tu.

Basi akaenda kwa Jacuzzi kuoga kisha akarudi baada ya Muda ikawa kama pombe inamuisha hivi akawa kama ana aibu aibu inamuingia . Akaniambia omg nashangaa nimekujaje hapa kirahisi hivi! huku akiwa anakuja kitandani. Nikamwambia kaa pale kwenye meza kwanza ale chakula! kasema oh you are such a guy with so much care and concern! nikamwambia ndivyo nimekuzwa. Basi nilikua na usingizi nikamsindikiza kidogo na stori mbili tatu kujaribu kumshauri maisha nk huku akila na kumuambia mm nadhani angefanya vizuri sana angekuja kufanya kazi mikoani maana nilishawaza wapi pa kumueka. Akawa anashangaa sana mimi ni mwanaume wa namna gani na nikamwambia sitamgusa niko very concern na maisha yake tu kwa leo.

Hakuamini na mm ndo nilikua nimeamua hivyo. Na mm kumpima imani yake nikawa nimeweka hela cash iliyobaki pale kwenye meza kabisa ili nijue ni malaya au la maana aliniambia yeye anafanya kazi posta pale ofisi fulani kama mtu wa masijala. Aisee asikuambie mtu usiku ulikua mzito kwel kweli nikajikaza kushinda tamaa zote yeye akawa kama haamini namuacha kumla! after all treatment nilomfanyia. Mimi nikasema simba lazima niweze pia kutokula nyama sio kula tu kila siku nijue pia kutokula.

Yule binti alikua yuko uchi wa mnyama kabisa kajifunga taulo tu tukapiga stori akawa amenishika shika mb** imesimama balaa ila nikamwambia aache hatutafanya. Sijui niliishia wapi ila niliposhtuka ni asubuhi yake saa nne hivi kuchek pembeni simuoni mtoto...ile kuamka kitandani kukaa vizuri namuona mtoto anatoka washroom ! sikuamini! akaniambia aliamka saa nyingi akawa anasubiria niamke. Nikacheki mezani pesa zangu ka 210k na docs zangu zipo pale pale. Nikasema doh makubwa kumbe huyu duh mwaminifu kama mimi nilivyokuwa mwaminifu kwake.

Hari ya kutaka kumsaidia ilizidi sana. Nikapiga simu kitchen wakaleta breakfast chumbani ya watu wawili. Sasa ilikua jumamosi hiyo jioni ndo narudi kilimanjaro.Nikaapa siwezi badili maisha magumu ya wote pale nilipokuta wanaishi ila naweza badili maisha ya huyu mmoja. Tukiwa twapata breakfast nikamshawish Aje kaskazini kuangalia fursa na afanye biashara. Huwez amini yuls duh alikaa nami siku nzima mpaka jioni akanisindikiza Airport.

Nikafika kaskazini akanitwangia simu kuniambia you are such a gentleman I have ever met! Thank you. Mimi nikatabasamu. Basi tukaanza mahusiano mema hivyo baada ya mwezi hivi nikamtumia mshiko mkubwa afungue biashara! alete mkoani aachanae na kazi ya ofisi ambayo mshahara wake hata gate man wetu anamzidi. Kweli huwezi amini ni miezi tisha hivi sasa huyu binti amepiga hela mbaya ni milioni tano tu nilimpa ila nilipokuja kumtembelea sehemu ya biashara yake na nyumbani kwake kwa kweli niliridhika kwa sasa anakaa mitaa ya changanyikeni nyumba alokodi inaridhisha na biashara amefungua tawi mpaka hapa arusha...kaniambia tufikirie sasa aweze kwenda nje ya nchi kabisa kuleta mzigo.

Sasa watu huwa wanashangaa sana jinsi navyoheshimika na kupapatikiwa na demu huyu ika hawajui nimetoka wapi nae..wanamuona hivi alivo hawajui alivyokuwa huko awali. The moral of this story is Wema hauozi. Na muwe na huruma. Ila mademu wa Dar msiwe na dharau maisha yenyewe hayo mnaishi hamjui kesho mtaamkaje basi mkiamkiwa muitikie maana hamumjui malaika wenu wa kesho.

NB nilisahau kwa mabaharia nadhani mtauliza kama nilimla au sikumla kabisa..jibu ni kuwa kwa sasa ana mimba yangu ya miezi mitatu!
Mwanangu siku ya kumkodi MC nipe hio deal nije ku host!
 
Kaka nyumbani ni bukoba sehem gani mkuu
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ila sijui tatizo ni nini haswa ila kila mtu wa mkoani akina Dsm lazima atazungumzia Mlimani City..yani jamaa wa mikoani na Mlimani City ndo wanaonaga kama vile wameshakua wajanja hahahaha
Ni ukweli kuwa is a centre ya watoto wa mjini kukutan kirahis hasa kwa location yake ,ukiend iringa bila kufika mtaa wa chuo cha Ruco hujafika,ukienda arusha bila kufikq kalolen bado mgeni,ni kila mkoa unawanPokutana wenye mji na wagen hupenda kwenda hapo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom