Wanawake: Tujihadhari na uchumba sugu

Wanawake: Tujihadhari na uchumba sugu

muzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,046
Reaction score
1,473
Ni jambo la wazi wanawake wengi wanaangikia kwenye dimbwi la mapenzi pasipokupenda kwa sababu mbalimbali. Kuna shoga zangu wanajikuta huko sababu ya mimba za bahati mbaya, wengine kama kiki ya kulazimisha kuolewa, wengine kujirahisisha ili kupendwa, wengine kisingizio cha kumkamata dume ili akuoe na sababu kadha wa kadha.

Sasa leo siangalii hayo, tuchukulie kama imetokea maana imepangwa/haijapangwa. Cha kushangaza baada ya kutokea hayo, wanawake wanajishahau kufanya lolote liwezekanalo ili sasa kuhalalisha mahusiano yawe rasmi kupitia kanisani, msikitini, serikalini au hata njia za jadi. Wanaume huwa wanatuchezea danadana sana kuwa ngoja maisha yakae kwenye mstari ndipo tuhalalisha swala la NDOA kwa kusingizia kujenga, kupata misingi imara ya kipato/kazi/ajira, wengine kununua gari na sababu zingine nyingi ili mradi akuchezee mpaka uzeeke.

Inaleta hasira sana nimekutana na shoga zangu wamezaa mtoto wa 1, 2, 3 mpaka wa 4 bado hajahalalisha ndoa. Hii ndo tunaisha uchumba SUGU. Uuuwiiiiii jamani sasa sijui tuwaweke kundi lipi, maana mwanamke kila mwaka unapanua tuu unatotoleshwa hata hufikirii kuweka ngumu swala la ndoa. Unaishi na mwanaume miaka 4, 5,7 hata wengine 10, sijui tuwaite wachumba sugu, nafikiri mtanisaidia jina zuri.

Unajua haya maisha yanapita kuna leo na kesho linaloweza kutokea mfano kifo, ajali na mengine yatakayokuondosha katika uimwengu huuu. Sasa kwa wale waumini wazuri wa dini kama ukifika hujaweka mambo mazuri ya ndoa inaleta shida kidogo kiimani, kwa watoto, kwa wazazi wako mke na jamii nzima kwa ujumla.

Wanawake tuamke jamani, hizi ahadi za kuahirisha ndoa kila mara zinatuweka pabaya, hata HESHIMA ya ndoa haipo wapendwa. Tusitake kufurahisha ulimwengu kwa ndoa/harusi za mamilioni kisa tu nionekane, tuangalie roho zetu na uondokapo duniani hao watoto utawaacha katika mazingira gani. Fanya sherehe simple that's all!

Shoga zangu Tupinge vikali Uchumba Sugu ni AIBU jamani, hata kama tulifanya makosa kuingia huko turekebishe hayo makosa, tunajisahau sana.

Hope nimesomeka vizuri.

Thanks and Take Care!
 
Love is not the better choice, but it's a great risk.

Acha nikuunge mkono
 
HAKUNA MWANAMKE MJANJA KWA MWANAUME UTALIWA TU NA KUZALISHWA PIA
 
Hii mifumo ya maisha ya kimjinimjini ndiyo shida sana. Na bahati mbaya hatutaki kuangalia tulipojikwaa ili turekebishe na jamii ikae sawa.

Raha ya ndoa na thamani yake iko pale hatua zinapofuatwa kwa uadilifu tangu awali. Kila kabila lina taratibu zake za mambo ya kuoana.

Nina uhakika
~hakuna mzazi huwa anapenda kuona mtoto wake ameanza tu kuishi na mtu bila utaratibu.
~Nijuavyo mimi hakuna utaratibu ambao ni mgumu unaozuia kuoana.

Mwanamke unajirahisi tu unaanza kupika, unaosha vyombo, unafua eti kwa mchumba ili aone kuwa ni mchapa kazi. Hakuna kitu kama hicho, wakati unakuwa bado. Na wengi kwa kujenga hayo mazingira unajirahisi hata na mwili wako kisa tu mchumba.

Na akishakuwa anapata huduma ndiyo basi tena, mwanamke ndiyo atakuwa mtumwa.
 
Wengi ukiwauliza wanasema Ndoa ni gharama anataka ajipange miaka inakwenda tu namuuliza ndoa au harusi Ndo gharama?na kipi chenye umuhimu Kati ya harusi na ndoa? Jamani ndoa sio gharama ya kumfanya mtu ajipange miaka
 
Kuna jirani yangu hapa yeye ana mwaka wa nne tangu aanze kuishi na baba mtoto wake, kuhusu ndoa anasema mpaka wajenge nyumba ya familia ndo watafunga ndoa.
Ninachojiuliza ni kuwa miaka yote hii anakaa kwenye nyumba ya kupanga na mtoto kampatia kwenye nyumba ya kupanga ila harusi anataka imkute kwake,
ina maana nyumba ni muhimu kuliko mtoto aliye mpatia nje ya ndoa tena kwenye nyumba ya kupanga??
 
Kuna jirani yangu hapa yeye ana mwaka wa nne tangu aanze kuishi na baba mtoto wake, kuhusu ndoa anasema mpaka wajenge nyumba ya familia ndo watafunga ndoa.
Ninachojiuliza ni kuwa miaka yote hii anakaa kwenye nyumba ya kupanga na mtoto kampatia kwenye nyumba ya kupanga ila harusi anataka imkute kwake,
ina maana nyumba ni muhimu kuliko mtoto aliye mpatia nje ya ndoa tena kwenye nyumba ya kupanga??
Wanaona harusi ni muhimu kulko ndoa inashangaza sana.kuishi bila ndoa sio Vema
 
Wanaona harusi ni muhimu kulko ndoa inashangaza sana.kuishi bila ndoa sio Vema
Ni kweli mamy.
Kupata mimba kabla ya ndoa inaweza tokea bila kupanga, lakini mmekaa mpaka miaka 3 au zaidi huoni kama ni tatizo na unaendelea kuzaa watoto katika uzinzi, huwa inawapa watoto wakati mgumu sana wanapokuwa wakubwa au wanapoanza kujitambua mana akifikiria kuwa alipatikana nje ya ndoa huwa inaleta shida fulani and i know how it fill mana nilishapitia huko so siko tayari kumfanya mtoto wangu aje apitie hali kama niliyoipitia mimi.
 
Tatizo watu sasa tumeona kama ni kitu cha kawaida sana wakati kiukweli hakileti taswira nzuri katika jamii na hasa kwa watoto. Hatuoni aibu tena na wengine wanajisifu kabisa kwa kuwa single mama. Haukua mpango wa Mungu huo.
 
Back
Top Bottom