Umeolewa,una kazi nzuri,mme ni mfanyibiashara,mambo yake yamechanganya,nice house,gari,watoto shule za bei mbaya etc , lakini kila kukicha unahisi ana mahawara.The fact kwamba mmeo ni mhangaikaji kila wakati bize kwenye simu. Mume ana matatizo TRA,anayemsaidia ni mdada,anapigiwa simu wakati mko pamoja sebuleni,anapokea na kuongea na huyo mdada,mke anasikia sauti ya kike kwa mbali,presha inapanda inashuka.Anavizia mzee amekwenda toilet anachukua simu ya mmewe na kuscroll last number received,anai note,anai set simu yake kwenye sms na kumwandika mama wa watu ujumbe huu:
"Nani wewe unampigia simu mume wangu (anamtaja kwa jina),malaya mkubwa wewe,kwanza una ukimwi,mkome mme wangu...etc etc". Upande wa pili mama wa watu anapokea ujumbe huo wakati yeye ndo anahangaika kwa nia njema kumsaidia jamaa mambo yake ya kodi......just imagine,halafu ni mama mtu mzima ana heshima zake.
Yaani....nimechoka kabisa.
usikimbilie kwenye hili.
Labda bishanga hajajenga mazingira ya kuaminiwa, kama kila siku ana mwacha na maswali basi mke lazima awe insecure.
Umeni miss eh?sijui Bishanga kapigwa na mwiko, mbona kapotea?
njoo mwaya, nakuonea huruma kweli, na huyu mkeo lazima tumchape, yaani kakuharibia japo si sana.
Sasa jipange kwenda kuomba msamaha huyu mbibi wa TRA tu ili aendelee kukusaidia, ila msipigiane simu saa za usiku.
pole sana bishanga,
kwa nini mkeo hajiamini?
Ina maana miaka yote mliyoishi pamoja hajakujua tu?
Au umeweka mazingira ya kutoaminika kwa mkeo?
Hebu keti zungumza na mkeo kuhusu swala hilo, na athari alizokusababishia, na wewe kama una mambo chobingo au mazingira ambayo sio aminifu yaache.....
Pole sana
BT na wewe unachukua akili za shankumpempe kongosho?hilo nalo neno kongosho....
Au bishanga ana small hausi zake mkewe anazisaka? Dhahama imemuangukia bibi wa tra? Haiwezekani mkewe akurupuke tu kama hakukuwa na 'mazingira ' yasiyoeleweka.....z
Pole bishanga, inawezekana hukujijengea uaminifu kwa mkeo tangu awali, humu jf tu pia huaminiki(joke). Jifunze kumshirikisha mkeo hizo mambo yako hata kama si kwa kumtaka ushauri hata kwa kujiongelesha pia si vibaya.
Mwanamke mpumbavu
Umeolewa,una kazi nzuri,mme ni mfanyibiashara,mambo yake yamechanganya,nice house,gari,watoto shule za bei mbaya etc , lakini kila kukicha unahisi ana mahawara.The fact kwamba mmeo ni mhangaikaji kila wakati bize kwenye simu. Mume ana matatizo TRA,anayemsaidia ni mdada,anapigiwa simu wakati mko pamoja sebuleni,anapokea na kuongea na huyo mdada,mke anasikia sauti ya kike kwa mbali,presha inapanda inashuka.Anavizia mzee amekwenda toilet anachukua simu ya mmewe na kuscroll last number received,anai note,anai set simu yake kwenye sms na kumwandika mama wa watu ujumbe huu:
"Nani wewe unampigia simu mume wangu (anamtaja kwa jina),malaya mkubwa wewe,kwanza una ukimwi,mkome mme wangu...etc etc". Upande wa pili mama wa watu anapokea ujumbe huo wakati yeye ndo anahangaika kwa nia njema kumsaidia jamaa mambo yake ya kodi......just imagine,halafu ni mama mtu mzima ana heshima zake.
Yaani....nimechoka kabisa.
sasa unaficha, siku ukifa nani atarithi?
Na atajua unamiliki nini na nini na viko wapi?
Kama humuamini kiasi hiki bora nioe mie tu.