eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,320
- 16,293
Ukifika dar cha kwanza kujutana nacho ni wanawake na wanaume wa dar wakiwa wamevaa suruali za kubana
Jambo hili lilinishangaza sana na yasemekana wameiga huko mamtoni kwa wasanii na waigizaji wa huko nao wakaanza kuzivaa huku wakijiona wamependeza kupita kiasi
Hata kwa wanaume na wanawake wanaotoka mkoa nao wameingizwa mjini
Ilinilazimu kuuliza inakuaje wanawake na wanaume wa dar ni visuruali vya kubana tu
Niliishia kuonekana mshamba tu na wakuja
Sijui kiafya ikoje lakini naamini wanawake na wanaume wa dar wanaangamia taratibu bila kujijua kwa sababu za hivi visuruali vya kubana
Mtaalam mmoja aliniambia kua zinasababisha upungufu wa nguvu za kiume pia