Wanawake na Siasa

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,721
Nimekuwa najiuliza maswali mengi juu ya siasa za sasa za kitaifa na za kimataifa nikajikuta kwamba bado ninabaki na maswali mengi sana juu ya nafasi ya mwanamke katika uongozi. nashindwa kauelewa ni kwanini wanawake bado tunashindwa kuwashawishi wanaume kivitendo hadi tuonekane kama tunaweza kuwa viongozi wenye uwezo unaotakiwa.

Binafsi nakubaliana kabisa kwamba kila binadamu ana mapungufu yake lakini bado pia napata kigugumizi kwanini mapungufu ya kike kiutawala yanakuwa na sumu kali sana. Ingawa kwa nchi kama yetu imejitahidi sana kuinua wanawake hasa kwenye nafasi za uongozi iwe kwenye taasisi ama hata kwenye nafasi za juu kama uwaziri ubunge nk kimataifa na kitaifa lakini bado wanawake sisi mwisho wetu unakuwa kwamba hatuwez ku excel kama ambavyo wengi walitaka iwe.

nimejaribu kuangalia kwa umakini sera ya kuwa na viongozi kwa ratio ya 1:1 bungeni lakini nikajiuliza swali moja la msingi je tunategemea ratio hii ya 1:1 iletwe na viti maalum tu??

je ni nini ambacho wanawake waliotangulia kwenye haya madaraka wamekifanya ili basi kuongeza nafasi za wanawake kugombea na sio nafasi za viti maalum??

ukiangalia kwa makini utajiuliza zaid hivi nje ya viti maalum inamaana hakuna viongozi wa wanawake 20 ambao wanaweza kugombea nafasi na wakapita kwa kura za wananchi?? ni kwanini sasa huu ni mwaka wa 20unakuja toka tuanze uchaguzi wa vyama vingi mpaka leo bado wanawake tunategemea kwa azaid ya 50% viti maalum??

tumeona wanawake wakiwezeshwa na kujiwezesha kiuchumi, kielimu na hata kisiasa lakini hatuoni kabisa kama mafanikio yao kisiasa yanamkomboa mwanamke mwingine aliyeko chini. zaid sana utasikia baada ya muda kashfa zikimuandama kama vile za ngono, ufisadi, wizi, kunyanyasa etc. sasa kuna shida gani hapa??

wanawake walioko bungeni zaid ya kusutana hawana jingine siwaoni kama wanania thabiti ya kutaka mwanamke akomboke kisisasa kwamba ifike mahali wanaume waamini kabisa kwamba mwanamke anaweza kuwaongoza na katika uongozi wake mambo yakaenda sawia. Binafsi kuna mambo tu ambayo nimeona kwamba pengine yaweza kuwa sababu ya haya yote nayo ni
  • wanawake tunashindwa kutofautisha kati ya madaraka ya uongozi nyumbani na madaraka ya uongozi ofisini ama kwenye siasa. madaraka ya nyumbani siku zote ni lazima yatanguliwe na maamuzi ya mwisho kutoka kwa baba, na hata pale unapoona kwamba hukubaliani nalo basi ni wazi huwez kumbishia mbele ya watoto ama watu ila utamwambia mkiwa wawili kwa namna ya kueleweka zaid. Lakini maaamuzi ya madaraka ya uongozi ofisini ama kwenye siasa ni lazima yatanguliwe na wewe mama kwamba kauli yako iwe thabiti lakini iwe na mantiki sana katika jambo husika. ni lazima upoteze muda wako kusoma wengine kwenye swala husika waliamua vipi ili uwe na references za kutosha kwamba hata unapotoa maamuzi basi yalete tija ulipo.
  • wanawake tunapenda zaid huruma ya second part kuliko, kupenda kushawishi kwa uwezo wetu. nafikiri walioanza kwa kutupa huruma ndio waliotudumaza hivi tulivyo. ukiskia disco ladies free, siasani viti maalumu mashuleni wasichana wanapewa upendeleo sikatai ni mwanzo mzuri lakini tunapaswa sasa tuachane nao. nakumbuka wakati najiunga chuo kulikuwa na mradi mmoja wa CARNIGIE PROGRAMME ambao ulikuwa na lengo la kusomesha watoto wa kike masomo ya sayansi chuoni. niliupenda ule mradi manake siku unafunguliwa walisema hivi, "" sisi tutawasomesheni kwa vipindi vinne baadae nyie mtakuwa mmeshaangaza nuru kwa wadogo zenu ili wao wasisubiri carnigie tena bali waweze wenyewe"" ukweli baada ya vipindi vyao vinne kupita waliondoka lakini cha ajabu hakukuwa na mpango mwingine nyuma wa kumfanya mtoto wa kike apende sayansi sasa ikabaki wanasubiri huruma za senete tu kwamba mwaka huu wasichana sayansi tuwachukue hadi point ngapi. hali hiyo imeendelea hadi huku kwenye siasa jambo ambalo linazidi kushusha credibility ya mwanamke kiuongozi.
  • wanawake kutokupendana ama sijui kugombanishwa yaani sijui hata niiweke vipi lakini hili nalo ni tatizo kubwa sana sana miongoni mwa wanawake wengi sana.
hebu wanajamvi semeni nini kifanyike ili kuweza kuboresha hali hii??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…