Wanawake mpewe nini ati????

Kinyengeli

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
452
Reaction score
143
Habarini za leo wana MMU wenzangu!!,

Leo nimeona si vibaya nikaamua kuwaelekeza dada zetu hasa nyie ambao mmeolewa mmekuwa na matatizo sana kiasi cha kuwa ndio chanzo kikuu cha kuharibu ndoa zenu. Wakati tukiwa boyfriend na girlfriend way back kuna tofauti kubwa na leo tukiwa mke na mume, mitazamo na fikra za wakati ule na sasa nitofauti pia kumbuka wakati ule ilikuwa ni muhimu na mawazo yetu yalikuwa yakiujana zaidi mfano kuwa na gheto kali hata kama la kupanga lililosheni vitu muhimu, Mziki, Tv Bed la ukweli na vimitoko vya kutosha vya hapa na pale, vijizawadi kama Cards, bites, vijinguo nguo vya ndani, kusifiana sifiana hata kama kwa uongo etc.

Sasa tumeoana Mungu katujalia labda hata mtoto au watoto, malengo na fikra zinabadilika sana hususani kwa wanaume kama ulikuwa unafikiria sana mapenzi na vitu mfano wa hapo juu mtazamo unaingia stage nyingine,. Wanaume wengi huanza kujiona na kujitambua kuwa ni watu wenye majukumu, kuhakikisha anamtunza vema mkewe na familia kwa ujumla, kutafuta namna ya kuongeza kipato ili aweze kukidhi yote hayo, kufikiria ujenzi wa nyumba , kumiliki vitega uchumi na kufanya kazi kwa bidii kiasi cha kumfanya kuwa busy sana na kujikuta automatic baadhi ya vitu alivyokuwa anavipa kipaumbele wakati huo kama kumsifia mkewe utani wa hapa na pale, kumpetipeti, vijizawadi vya mara kwa mara na vimitoko hupungua kwa sababu za kiuchumi na majukumu kuongezeka lakini wakati mwingine kusahau.

Enyi wanawake tusaidieni waume zenu tunateseka sana kwa ajili yenu, msituone kama hatuwajali na kuanza kutufikiria tuna wanawake wengine hapana wengi wa wanaume wa kweli wanaojua wajibu wao ni watafutaji hasa na sio wavivu, mtuonee huruma tunahitaji sana faraja zenu na kuonyesha appreciation kutoka kwenu. Mara nyingi wanawake ambao wameolewa na wanaume waliofanikiwa sana ndio wanakumbwa na tatizo la kutoka nje ya ndoa zao , unajua hii ni kwanini? Ewe mwanamke tambua binadamu ni yule yule huwezi kupata kila kitu kutoka kwa binadamu., kama atakupa hv hawezi kukupa vile kwa kiwango utakacho ndio maana wazee wa zamani walisema ndoa ni kuvumiliana hata nyie kuna vitu hatupati kutoka kwenu kama ilivyokuwa kabla ya kutuzalia watoto hao lakini still tunawavumilia.

Kuweni makini msije kusema sikuwambia adui ya mtu ni mtu, na mwanamke mjinga huvunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Enyi wake watiini waume zenu , nanyi waume wapendeni wake zenu. Hivyo hakuna upendo pasipo na utii.
Mchana mwemaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!
 

mkuu,dawa yao huwa ni kuwapa uongo tu,usipowapa uongo utaumia mwenyewe
 
^^
Hilo fundisho la wanawake watiini waume zenu..siku hizi linaandikwa kwa penseli..
Hudumia familia tu mengine mwachie Mungu..wanawake wanaoridhika wanahesabika siku hizi
^^
 
hata kama uko busy ni vyema kutenga muda na familia

wengune busy 24/7 eti anatafuta pesa......na kuongeza kipato

kila kitu kipewe nafasi yake..........
 
Wanawake mmesikia?
Sio kila wakati uko wapi?..huyo ni nani?..unarudi saa ngapi?
Jueni sio kila wakati tunachgua mademu bana....saa zingine tunatafuta mijihela!
 
tunawajua mnaposema uongo sema vile na sie tunawadanganya tunaona sawa tu.

usinambie ngoma droo?sasa inakuwaje pale mdada anapotumika then anadampiwa?mbona huwa anakuwa na hasira?kama wote ni nidanganye danganye?
 
Msemee mkeo, usidhani wanawake wote wanawatesa waume zao, tena ukute wake wengine ni providers wakuu wa home.

Kuhusu mwanamke -------- kuivunja nyumba yake, haikubaliki bila digestion.
 
hata kama uko busy ni vyema kutenga muda na familia

wengune busy 24/7 eti anatafuta pesa......na kuongeza kipato

kila kitu kipewe nafasi yake..........

Na nyinyi punguzeni adiction ya mitandao, kuna Dada mmoja hapa mahiri kweli wa kushauri mahusiano ila kuna siku nilimuuliza hivi ni saa ngapi unapractise haya unayoshauri? Akakosa jibu.
 
ni ujumbe mzuri kwa kweli, mwenye kusikia atasikia....
lakini, wakati mwingine mume atenge muda kwa ajili ya familia yake..
pesa hazitoshagi jamani.... hata ukeshe ukizitafuta, kesho yake pia
utaendelea kuzitafuta
 
Kaka andiko lako ni zuri sana ila kuna siri ambayo hujaijua, mtafutaji wa hela na mtu busy hawezi kupata tabia ya kufanya hivyo baada ya kupata mtoto au watoto. Binadamu tunatofautiana mwingine anaweza kuwa mtafutaji sana na busy akipata familia sasa anataka kuspend muda mwingi kidogo na familia na mwingine kinyume na mwingine anaona mkewe sasa amekuwa outdated na sasa anaanza kucheza nje. swali gumu kuliko yote ni kuwa utamjuaje kuwa ni yupi sasa. Jibu lake usiangalie wa nje elewana na wako m convice ajue unachofanya kuwa ni cha maendeleo. Usichanganye wanawake wote maana wangu wakati mwingine ananiambia husband leo kula huko huko hatupiki au si tutakula kipolo lakini mwingine hawezi tamka hivyo yuko ladhi akologe kologe chakula ili mradi ule home
 
Mi naanimi kwa kadti ndoa inavyokua na umri mkubwa ndivyo kiwango cha kupendana na kuheshimiana kinapaswa kuongezeka pia.
Tuweke mlinganyo sahihi kati ya majukumu ya ujenzi wa familia na romantic and love aspect chochote kisifanywe kwa kuzid na kuchukua nafasi ya kingine.
 
Nimeandika hapo juu kwamba baadhi ya mambo yanapungua sio kwamba yanakosekana kabisa lakini wengi wenu mnataka iwe vilevile kama enzi zetu za uboyfriend.
hata kama uko busy ni vyema kutenga muda na familia

wengune busy 24/7 eti anatafuta pesa......na kuongeza kipato

kila kitu kipewe nafasi yake..........
 
Kinyengeli kwanza nakupongeza kwa kuwa mume mzuri na hii ni kutokana na maelezo yako,lakini nataka nikukumbushe kitu kimoja tu mkuu nothing good and important like the time together with your family,yote hayo cars,houses good clothes an blah blah zinazotokana na pesa ni mbwembwe tu na wala familia bora haitokani na hivyo ila mawasiliano mazuri na kupata walau muda hata kama ni kidogo wa kukaa na mtoto na mkeo kuwaonyesha unawapenda kihisia pia na sio kimahitaji yao ya kimwili tu,jitahidi sana mkuu kutafuta kusikunyime nafasi ya kumwonyesha mkeo jinsi unavyompenda na kumthamini kwani pesa sio kipimo cha mapenzi bali vile umtendeavyo mkeo,pesa ni chachu tu your wife needs you more than the money you search for her.
 
Last edited by a moderator:
Na nyinyi punguzeni adiction ya mitandao, kuna Dada mmoja hapa mahiri kweli wa kushauri mahusiano ila kuna siku nilimuuliza hivi ni saa ngapi unapractise haya unayoshauri? Akakosa jibu.

labda yuko single.............ndio maana yuko mtandaoni mda wote

jana kuna swali nilikuuliza hukunijibu
 
Nimeandika hapo juu kwamba baadhi ya mambo yanapungua sio kwamba yanakosekana kabisa lakini wengi wenu mnataka iwe vilevile kama enzi zetu za uboyfriend.

mbona na nyie huwa mnalalamika eti mapenzi yamepungua yamehamia kwa mtoto

ko na nyie kubalieni pia kuwa kuna baadhi ya mambo huwa yanachangeee
 
mbona nyie hamridhiki na dudu...mnakimbiza hadi wasichana wa kazi na ma-bar medi....mpewe nini mridhike ni ...nyonyo?
 
Msemee mkeo, usidhani wanawake wote wanawatesa waume zao, tena ukute wake wengine ni providers wakuu wa home.

Kuhusu mwanamke -------- kuivunja nyumba yake, haikubaliki bila digestion.
Kuwa providers haimaanishi kwamba mwanaume basi akae tu nyumbani kumbuka pesa zenu nyie wengi wenu huwa ni zenu tu mkitoa hamuwezi kuvumilia kutoa wakati wote na masimamngo huwa hayakosi kwenu na kujiona kama hujaolewa. Rejea mabandiko yenu mengi humu mnasema mwanaume atoe huduma, na pesa ya kuhongwa ni tamu. Hv wewe unaweza kuprovide kila siku kwa familia na ukaona sawa tu kama mumeo yupo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…