Wanawake: Madhara ya Mapenzi ya Mbali, Kuweni Makini na Mapoozeo!

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Hii stori nimeikuta mahali. Sijui kama chanzo chake ni huku JF ila nadhani inafaa kwa mafundisho. Mafundisho ni kuwa "Mwanamme akichepuka, dhambi inakuwa nje ya mwili wake na mpenzi/mke anaweza kumsamehe ilhali kwa mwanamke uchepukaji ni dhambi ya ndani, kusamehewa na mme/mpenzi ni mashaka makubwa".

Mwanamke hakuumbwa kuchepuka kwani dhambiye I ndani yake. Uzi wenyewe ni huu:


Kaka naomba ushauri wako, mimi ni Binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba ambaye tuko kwenye mahusiano kwa miaka 6 sasa, mimi nafanya kazi mkoani nayeye yupo dar, kutokana na ubize wa kazi zetu basi tunaonana mara moja kwa miezi sita lakini kila siku tunaongea na tunapendana sana. Kuna Kaka mmoja yupo hapa ofisini, sasa kaka tukaanza mazoea mpaka tukawa wapenzi, yeye naye mpenzi wake yuko mbali hivyo sisi tukawa tunatumiana tu kupunguziana hamu.

Kila mmoja alikua anajua mwenzake ana mtu wake, aliniambia ana mchumba na akija huwa namheshimu. Tumekua kwenye mahusiano kwa miaka miwili bila kugombana, mchumba wangu akija anamheshimu na mimi akija wake namheshimu. Sasa mwezi wa pili nilipata ujauzito, nilijua kabisa ni wake kwani mimi mchumba wangu nilikua nishakaa kama miezi minne hatujaonana.

Nilimuambia mwanaume akaniambia kuwa nitoe kwani yeye ana mchumba tayari, nilimuambia kuwa mimi siwezi kutoa kwani kama ni mchumba na mimi ninaye ila nimba ni yetu. Kusema kweli nilishaanza kumpenda hivyo nilijua kuwa mimba itambakiza kwangu, tuligombana sana mpaka kufikia hatuongei lakini baada ya kuona msimamo wangu alinywea na kuniambia kuwa zilikua hasira atalea.

Kaka mahusiano yalirudi mpaka sasa, shida ikaja kujitambulisha kwetu, kila nikimuambia aende akawa ananizugisha, ananipiga kalenda mpaka mwezi huu mwanzoni, alichukua likizo na kwenda kwao, Kaka nimefuatilia kumbe kaenda kufunga ndoa, wakati wote huu kumbe maandalizi kwao yalikua yanaendelea, namuuliza ananiambia amefikiria hawezi kumuacha mchumba wake kwani wametoka mbali.

Kaka niliumia sana, nilitafuta namba ya huyo mwanamke wake, nilimpigia kama mwanamke mwenzangu na kumuambia kuwa nina mimba ya mume wake hivyo ajipange alinijibu kuwa mume wake alishamuambia kuwa alifanya kosa yeye akamsamehe hivyo kama ni mtoto nijifungue kwanza ishu ya kulea hana shida hata kama mume wake akitaka kumchukua mtoto atalea kwani ni damu yao. Kaka nimekasirika kwani kanijibu kwa sharau kabisa hata hakukasirika kana kwamba mimi si mwanamke mwenzake!

Kaaka mwanaume karudi, tangu arudi namuona kazini hata salamu hamna, karudi na mke wake kwani alikua anafanya kazi binafsi na mkataba huko kazini kwao umeisha. Nikimtumia meseji kuhusu mtoto ananijibu nisubiri nizae kwanza watu hawahudumii mimba. Mchumba wangu bado tunawasiliana, nina mimba ya nane na yeye hajui kama nina mimba, nawaza niitoe, watu wananiambia kubwa sana nitakufa, kingine kinachonipa wasiwasi nikuwa hapa ninapofanya kazi kuna rafiki zake wanajua nina mimba na mara nyingi wananipa hongera wanajua ni ya jamaa sasa nikitoa itakuaje si wanaweza muambia ikawa shida, naomba ushauri wako Kaka.


Kaka, Mjomba, Baba, Babu na Wanaume wote, mmeombwa ushauri!


Bazazi
 
Una mimba ya miez nane na mchumba ako hajui?! Duuh! Ina maana miez yote hyo hamjaonana!? Au na yeye tayari kashayajenga na mtu mwingine huko!? Unadhan marafiki zake watakuwa hawajampigia kumpa hongera!? Hahahaaaa
Wengi watatumia hii reply kama summary badala ya kusoma uzi wote hapo juu.
 
Lesson learnt kwa wanaume: ukiharibu sehemu na ukaona 98% of chances habari zitamfikia wife/mchumba, wewe wahi mapema umpe ukweli wote plus some salt kidogo. Wana huruma sana hawa viumbe na atakusamehe tu ili pia kumkomoa mwanamke aliyetendwa huko.
 
Siku zote unachokitafuta utakipata.. Afurahie kazi na matunda ya kazi yake...
 
Mjinga ni Mwanamke. Mlikubaliana Kulana Na Kusepa Sasa Ww umenogewa na Mimba Umebeba Kinachokushinda Kulea Ni Nini wakati una Kazi. Jamaa Kasimamia Kucha na Kaoa Tayari

We endelea na Maisha Ya Kudanga
 
Back
Top Bottom