Wanawake kwisha habari yao

Hebu litafakarini neno katika roho na kweli...


Hili andiko naliona wazi wazi kwa macho ya nyama. Hata wewe kama upo vizuri unaweza kuona. Yafuatayo:
1. Andiko linaonyesha wanawake watakuwa wengi kuliko wanaume. Yaani wanawake 7:1
2. Wanawake watakuwa na uwezo wa kujihudumia. Kujilisha na kujivalisha.
Tuje kwenye uhalisia sasa. Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wanawake lenye kutia mashaka hasa kwa wanawake waliopo umri wa kuolewa.
Kwa upande wa kiuchumi wanawake sasa hivi wanajitahidi na nadhani miaka 10 ijayo wanawake wengi watakuwa na uchumi mzuri kuliko wanaume weng
 
Utaelewa tuu. Sio maneno yangu. Kitendo cha mwanamke kukataa kutolewa mahari kinathibitisha unabii huu utatimia hivi karibuni. Mwanamke anaanzaje kukataa kutolewa mahari ikiwa anajiamini.
Dah pole sana maana miaka inavyozidi kwenda mtaona mabadiliko mengi sana kwa wanawake. Huwezi badili dunia inavyoenda
 
Mleta mada nakukumbusha tu kuwa kuna maisha pia bila ndoa. Kuna watu wanajuta na ndoa zao kiasi cha kujitoa uhai. Ni heri niwe peke yangu ila niishi kwa amani kuliko kuikimbilia ndoa itakayogeuka ndoano!

Mkuu umesema iliyokweli. Ila unabii sharti utimie. Hayo ni maneno tuu ili upoteze time na focus ya ndoa ili muda ukikupita ukumbuke shuka kumekucha. Unaongea ukweli lazima uwe makini l
 
Umefeli sana, ata kifungu cha biblia uchotumia kama rejea bado hujakielewa ata chembe bali umekurupuka, umefeli kabisa, yaan sifuri.
 
Dah pole sana maana miaka inavyozidi kwenda mtaona mabadiliko mengi sana kwa wanawake. Huwezi badili dunia inavyoenda

Wape wenzako pole sio mimi. Wanaume hawajawahi kubadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…