Mi siwalaumu natoa tu ushauri walione na hiliUnawaonea tu mkuu, wao wenyewe huwa hawajielewi ni wakusaidia tu, ndivyo walivyo.
Akili zao wanazijua wao wenyewe, kama mwanaume pale tunapoweza kuwaisaidia let we do our best to help them.
Hili ndo linalotofautisha response kati ya mwanamke na mwanaume. Kwamba mwanaume response yake ni ya hapo kwa hapo katika kutoa msaada. Ila mwanamke ataona huruma tu then baadae sana ndo anaweza akafikiria labda atoe msaada.
Wanaweza wakawa wamekaaa wanamwangalia mwanamke mjamzito au aliyebeba mtoto mgongoni, WANAMHURUMIA SANA tu, ila sasa maamuzi ya haraka kutoa msaada ndo kashekashe. Usishangae kuona wanaume kutoa msaada haraka haraka ndivyo tulivyoumbwa kwa akili zetu. Na hili ni mojawapo ya tofauti kati ya mwanaume na mwanamke, ukiacha nyingine nyingi zilizopo.
Kwa hiyo inawezekana alichokisema mwanawao kina kaukweli kidogo, eti mnakuwa wazito ktk kitoa maamuzi?Kwa upande wangu huwa nikiona mzee,mjamzito au mama mwenye mtoto huwa napisha.
Pia inategemea nimekaa sehemu gani mana kama nimekaa mwisho kabisa ni ngumu.
Kuna siku moja nilikuwa natoka mjini naelekea sehemu basi zile gari zilikuwa hazitki mpaka zijaze kabisa ndio nyingine inapakia na hapo ilikuwa mida ya saa mojamoja jioni.
Nikapanda kwenye gari na siti nikapata tena mwanzoni mwanzoni tu.Gari ilipojaa akapanda mzee mmoja ikambidi asimame basi gari ikaanza kuondoka.Ila gari kabla haijaondoka nilikuwa nsjishauri kumwachia siti yule mzee au niendelee kukaa.
Mwishoe rohoni nikajisemea nakaa asimame tu kwani kwenye gari nipo peke yangu nimpe nafasi mbona wengine wamekausha tu.
Njiani sasa yule mzee alivyokuwa anapata shida gari ikiyumba na yeye anayumbishwa mara huku mara kule halafu kila nikimuona nafsi inanisuta.Mzee wa watu akashuka njiani(alifika alipokuwa anaenda).Njia nzima mpaka nafika nafsi ilikuwa inanisuta kila mara ile picha inanijia.
Nilijisikia vibaya kwakweli mana ilinichukua muda kusahau.
Ila toka hiyo siku nikikuta mtu wa aina hiyo amesimama tena karibu yangu nampisha tu akae.
Nilijifunza kwakweli.
Yawezekana piaKwa hiyo inawezekana alichokisema mwanawao kina kaukweli kidogo, eti mnakuwa wazito ktk kitoa maamuzi?
Kwa gali za Mbagala ili upate gari yenye siti labda usubiri miaka 10. Halafu kwa yale magari yanatoka maeneo ya mjini kutoka nje ya mji huwa yanajaza yalipotoka, kwa hiyo ili upate siti inabidi ukapandie mjini au usisafiri kabisaMimi naomba niongee hili kitofauti katika awamu tatu:
1. Mimba sio ugonjwa. Sio muda wote kwa sababu una mimba basi ndo huwezi kusimama hata kutoka morocco hadi makumbusho. Tuache kujiendekeza!
2. Mama una mtoto au tumbo kubwa, subiri gari lenye siti au gari ikisimama tu muombe konda au dereva akuwekee siti eboo(mimi nimetumia hii method kwenye ujauzito wangu na sikuwahi kupata shida ya kusimama kwenye basi). Mtu yuko mwanzo wa gari, lets say Makumbusho, gari likishajaa ndo huyo anapanda na mwanae. Sio fair kwa abiria wenzio.
3. Halafu wanaume mnasaidiaga si kutoka moyoni bali ili muonekane maana mwanaume akimpisha mama mjamzito au mwenye mtoto basi discussion kwenye basi inachange, ni "wanawake wana roho mbaya" mpaka mwisho. Wewe mwenye roho nzuri mbona hutendi wema ukaenda zako?
Toka mapema, panda gari ugeuze nalo. Huwezi simama na usubiri kudra za Mungu upishwe siti.Kwa gali za Mbagala ili upate gari yenye siti labda usubiri miaka 10. Halafu kwa yale magari yanatoka maeneo ya mjini kutoka nje ya mji huwa yanajaza yalipotoka, kwa hiyo ili upate siti inabidi ukapandie mjini au usisafiri kabisa