Habari zenu wana janvi,
Imebidi uzi huu niwashirikishe maana ni kitu ambacho hata mimi kimeniuma sana baada ya kutokea. Sisi ni binadamu na huruma mwenyezi Mungu alituwekea katika nafsi zetu japo wapo binadamu wasiokuwa na huruma hata chembe.
Kuna jamaa mmoja alikuwa na mahusiano na binti fulani kwa mda wa mwaka mmoja hivi na binti alimtambulisha kijana na taratibu za ndoa zilianza. Kijana alikuwa siyo mkweli kwa binti, maana alimdanganya binti mambo mengi sana yaani asilimia 80 ilikuwa ni uongo.
Binti alikuja kugundua kuwa aliyoambiwa na huyo kijana ni uongo mtupu siku chache kabla ya ndoa. Binti alilia sana na akailaumu nafsi yake kwanini hakuwa mdadisi wa kina ili kujua kama aliyoambiwa ni kweli au laah. Binti aliamua kuachana na mchakato wa ndoa na waliochanga walirudishiwa chao, japo Mchungaji alimshauri binti asamehe mchakato uendelee lakini binti alikataa katakata.
Ndugu wanajanvi hususani wanawake mnapenda sana kuolewa maana nahisi mtu anapooa au kuolewa huongeza heshima fulani katika jamii.
Nawaombeni muwe mnachunguzana kwa kina, muulize kwao wapi, mkoa gani, wilaya gani, kijiji gani, nia na madhumuni ni kupajua kwao pamoja na kufanya uchunguzi kimyakimya bila hata yeye kujua.
Hiyo itakusaidia sana wewe kujuwa hali halisi ya mwenza wako pamoja na kujiridhisha aliyokwambia kuhusu yeye na familia yao ni kweli au sanaa tupu.
Hakuna majaribio ya kuoa au kuolewa, tusiziache mila zetu tukaiga zaidi ya wazungu, maana utasikia oooh unataka kuoa familia yangu au unataka kunioa mimi, binadamu wa dunia ya leo wametawaliwa na tamaa na ubinafsi, bila kumjua vyema unayemuoa au anayekuoa ni kupeleka aibu na fedheha kwenye familia yako kama ilivyotokea kwa huyu mwenzetu. Familia imealika ndugu, jamaa na marafiki mwisho wa siku sijuwi mnawaambiaje wageni waalikwa, ni aibu sana na inaumiza sana.
Tutafakari kwa kina sana na tuchunguzane kwa kina sana kabla ya kupelekana kwenye familia zetu.