Wanawake kinachowatesa katika ndoa ni Karma

raia_mwema

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
479
314
Heshima zenu wakuu....

Hapa jukwaani kila uchao kwa asilimia kubwa ya thread zinazoanzishwa na wanawake ni za malalamiko na za kutaka ushauri juu ya ndoa zao.Wanawake hamjajiuliza kwann ndoa huwa zinakuwa ndoano kwenu? Wengi wa wanawake huongozwa na tamaa pindi wanapokuwa katika mahusiano unakuta mwanaume anakupenda kwa dhati na kwa moyo wote lakn baada ya siku kadhaa unamtafutia sababu ya kuachana. Mwanaume ukichunguza unagundua yule mwanamke amepata kwingine. Mwanamke anafanya hayo bila kuangalia commitment mtu aliyokuwa nayo kwake. Tena bila kujali. Hii hupelekea wanaume kuwa hit and run.

Lakini Karma hurudi kuwatafuna wanawake maisha yao yote hubaki kulia eti wananyanyasika bila kujua chanzo ndio wao. Ndio maana wengi wanakosa amani kwenye ndoa zao, vidonda vya tumbo vinawasumbua.

Wanawake msipobadilika mkaacha kuwatenda Innocent, basi Karma itawatafuna saana.
 
Maelezo yako ni mazuri ila hapo kwenye karma ndio kunautata, kwa kifupi Karma haipo
 
Shyeeeh...!!! kweli Karma atawafaidi, hivi ndo yule wanamsema... is a bitch au huyu ni wapi?
 
Karma goes either way.

Wanaume inawapata pata kwa kuoa wanawake vimeo.

Mnawachezea mabinti za watu weee mkijua fika hamtawaoa.

Karma anawacheki anasema ***** zenu mkimaliza nipo na nyie. Lol.

Kwakweli huu ushauri alipaswa autoe kwa wote. Sema huyu itakuwa katendwa kwahiyo anahisi wanawake ndio watendaji tu.
 
Kuna mdada kaweka uzi humu jana nkashangaa sn....jaribuni kutoweka v2 personal wazi haijalishi mtu kakufanyia nn,sometimes kumpuuza mtu ndio silaha kubwa.
 
Wanaume hebu tufungeni na kamba basii muache kutuzungumzia, kila uchwao thread ni ya wanaume kwenda kwa wanawake alafu mnatusingizia sisi ndio tunaosema
 
Kabisaaaa na usipom sapoti atasema umetendwa:D

Haya mambo bwana!!
Tatizo linakuja kwamba mwanaume anakutongoza kwakuwa umemeet vigezo vyake, swali linakuja je yeye amemeet vigezo vyako!! Ukimkataa basi utaonekana mbaya kuliko viumbe vilivyowahi kutokea, sasa utakubali wangapi!!!

Binadamu wote tuna tamaa, si wanawake si wanaume, kuna wanaume pia wanateseka kwenye hizo ndoa acha tu.

Hapa cha msingi angeongelea kwamba wote bila kujali jinsia tuthamini tu hisia za wenzetu, kama unaona kwakweli hapa pendo nehii kuwa tu wazi mapemaa kabla mambo hayajakwenda mbali. Ila pia ukiachwa usimuombee mwenzio mabaya bwana na kutaka aendako akakakutane na mabalaa tu. Wish him/her luck maana sidhani kama wewe unayemtakia mwenzio mabaya wewe mazuri yataandamana nawe wakati nafsi yako imejaa chuki..
 
Back
Top Bottom