Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,672
- 2,700
Amani iwe nanyi,
Naomba mnialike rasmi kwenye jukwaa la huba, mgeni wenu natokea majukwaa jirani hapo, hususan Ajira na Tenda.
Basi, nisikuchoshe, kuna kisa kifupi nitasimulia lakini naomba niwahase kitu dada zangu.
'Mwisho wa Siku, Mwanamume atakutamani kwa namna ulivyo, yaani maumbile yako, lakini atakupendea kwa namna unavyoenenda, yaani tabia yako'
Wenzetu kule Ulaya wanasema 'Boys Will be boys' wakiwa wanamaanisha kwamba, ki haiba Wanaume wanachelewa sana kukuwa, hivyo usimshangae jibaba likiwa linafanya mambo ya kitoto. Lakini mambo yamegeuka, dada zangu siku hizi HAMKUI, mmeganda kwenye Ulimbukeni, mnaendeshwa na Ujinga halafu Umri ukikutupa mkono sasa, unakuja JF kuandika vigezo vya Mwanamume unayemtaka, kumbe akili yako haipo tayari kumpokea, mtoto.
TWENDE SAWA.
Baada ya kupigwa na maisha, ambayo bado yanipiga mpaka sasa, nikahamia kilinge kingine hapa Jijini Dar, eneo la Mbezi. Kama ilivyo ada, ukiamia mahali pageni, unakutana na watu wapya. Basi nikakutana na Mdada ambaye anakimbilia miaka 29 hivi sasa, amepanga karibu nami, yani kuta tu imetutenganisha.
Basi katika kuishi kwetu na kuingiliana, zipo nyakati ambazo tukaanza kukaa pamoja tukipiga story za uongo na kweli, na wakati mwingine kuanzia jioni mpaka Usiku sana, tukimaliza kila mtu anatafuta mlango wake anaenda kulala.
Lakini mambo yakawa si Story peke yake tena, upepo ukabadilika, asubuhi moja hivi, kama kawaida Bachelor mimi nikajipikilisha, ubwabwa na samaki wa mchemsho, nikapakua kidogo nikaanza kufungua kinywa, sikuwa najua kama jirani yangu yupo. Naomba ujue kuwa hiyo 'nyumba' tupo watatu, kuna Bachelor mwenzangu ambae si mshindaji kabisa hapa.
Basi tuendelee, siku hiyo bwana sijui kama yeye naye yupo OFF, mi ndio najiandaa kwenda mizunguko huko, ghafla nikaona mlango unafunguliwa, tukasalimiana, nikauliza akanambia kama yupo OFF, basi nikamwambia nitafurahia kama jirani yangu utaonja pishi langu leo, akakubali mwanaume nikaingia chumbani nikala nikajiandaa nikasepa.
Akala, akanitumia mesej kwamba kulikuwa kitamu, basi nikaona fresh nikaendelea na mishe zangu huko. Zikapita kama siku mbili hivi, narudi Job,halafu sina nauli, so ikabidi ni print tu mpaka napokaa, hapo sijui nakula nini home, ila nikaona ngoja nifike kwanza, mengine ntajua huko, nipo njiani ghafla mesej inaingia.
'Jirani kama umerudi, utafungua kabati yako hapo, kuna mzigo nimekuwekea' nikatafakari kidogo, ila ikabidi nikajionee, kwa kweli nilikuwa nahamu ya kujua ni kitu gani, kumbe bwana siku hiyo na yeye kajipikilisha, nafungua ma hotpot, jamani ni hatari, mambo yamenona huko sio poa, nikala siku ile ikabidi nimshukuru na Mungu, maana kwa kweli sikuwa naelewa ningekula nini. Hapa sasa jioni ntajua la kufanya.
Basi hapo ndipo mazoea yetu yakaanza kupanuka sasa, kuna muda tulikuwa tunasaidiana kupika, tunakula wote. Ikawa kawaida sasa,kiukweli yale mazoea yalinifanya nianze kumpenda yule dada, na hakuna namna ningelikataa hilo.
Siku moja wakati narudi home, nimefika hivi nikamkuta mtoto wa mama mwenye nyumba yupo Chumbani kwa yule dada, ni jamaa mmoja hivi umri kwa kukadiria ni kama 30s hivi, au labda ni mdogo ila pombe zimemtafuna. Basi nikawa namuona anatoka chumbani kwa yule dada, roho iliniuma sana kujua kwamba jamaa ndio anapiga, ila nikawa najipa moyo, 'kama sio mpenzi wangu, kinachoniumiza kitu gani sasa' ikanibidi nikubali tu, mambo yakawa yanasonga hivyo hivyo, nikakubali kuwa mnyonge.
Basi bwana; kuna mtu nilimfanyia kazi yake ya graphics, ni mtu mzima kidogo, hiyo siku nikampigia simu, kwa ajili ya malipo, akawa ananizungusha, na hapo ni baada ya kama wiki mbili kupita, ananizungusha tu. Siku hiyo nikaona liwalo na liwe, kwa kawaida mimi nina aibu, na siwezi kumdai mtu fedha kama hajaamua kunipa, ila nitakuwa namkumbusha tuu, kistaarabu.
Basi, nikaenda kununua 'kadadaa' wanywaji mnanielewa, sio walevi, naomba nisisitize hapa. Nikapiga glass kama mbili hivi, ili niwe na confidence ya kumdai, basi napiga simu yake haipatikani, piga sana haipatikani, hiyo ni kama mida ya saa 2 usiku, nikaona hapa natwanga maji kwenye kinu, nikatoka nje, kuna mahala nikakaa, nimeongea peke yangu pale, nikamtukana sana yule mzee ili niondoe hasira zangu mpaka mida kama ya saa nne hivi, nikarudi zangu ndani, nikaendelea na glass yangu.
Ghafla ule mlango wa nje ukawa unafunguliwa. Mimi majirani zangu wakiwa wanaingia tu najua huyu ni nani, basi nikajua ni yule dada kaja, wakati huo nipo WhatsApp hapo, nikaona na yeye yupo online, nikamsalimia, ika blue tick, hakujibu, ghafla naona simu yake inaingia akanambia "Mambo" nikamwambia "kwa Yesu" basi akaanza kucheka, akaniuliza kama nimekuwa mlokole, tukapiga story mbili tatu pale ndipo nikaanza visa sasa. Nikamwambia
"Kumbe juzi ulikuwa na shemeji rafki yangu, umekuwa mama mwenye nyumba sa hivi, nikikusanya tuhela twangu nitakuwa nakupa"
Kama kuna siku yule dada alicheka sana ndio ile, akaniambia "Hapana, yule sio bwana angu, nilimpigia simu aje kunisaidia kufunga kitanda changu, halafu na pazia langu lilikuwa limeanguka so alikiwa anagongelea hapo juu, mana niliona wewe hujarudi"
Pale kidogo hata kamoyo kakanishuka, nikajisikia afadhali kidogo, nikasema haya hakuna shida nikahisi ndio baba yetu huyo" akacheka tena, akaniuliza kama leo nimemuamulia.
Bwana asikufiche mtu, Pombe mbaya, nikajikuta namwambia "siku nikikuamulia unadhani patakalika humu ndani, mana naona kuna mtu ni kama anachezea bahati hivi" akaanza kushangaa, maana hajanizoea hivyo mkristo mimi, " nikamwambia, ni vile tu nina mtu napendana naye, na nina mahusiano ninayotaka niyaishi, ila umeniweza sana"
Bwana yule dada hakuamini anachosikia, akaniuliza "hivi una confidence ya kuongea hivyo mbele yangu, mbona kama sikuelewi"
Mwanaume nikamjibu "Fungua mlango nije nikwambie huku nakuangalia usoni kama huamini" weeeeee, akafungua mlango kweli bwana, nasikia kabisa mlango unafunguka, pombe ilivyokuwa haina adabu, Abdala kichwa wazi asisimame, moja kwa moja nikafungua na mimi wa kwangu naelekea chumbani kwake.....
Ntaendelea.