Wanawake, Jifunzeni kuongea zaidi ya kulalamika

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
43,844
2,000
Mwanaume huelewa zaidi pale unapoongea na si kulalamika. Najua wanawake wametengenezwa kwa namna ambayo akiongea kitu kwa kulalamika basi hujisikia huru, hupata nafuu na wakati mwingine hata mwanaume asipobadilika basi yeye kwa kuongea hupona.

Lakini wanachoshindwa kuelewa na wanachoshangaa kwanini pamoja na kulalamika kwao kila siku wanaume hawabadiliki nikuwa wanaume wao hawajaumbwa kusikiliza malalamiko.

Mwanaume huelewa zaidi pale unapoongea na si kulalamika, kwamba kama anakukera kitu fulani basi ongea naye na sio ulalamike, unapolalamika wanaume wengi huchukulia poa kuwa hii ni tabia yao wanawake, una mdomo, huwezi kunyamaza na mwisho wa siku basi huishia kusema huyu nishamzoea.

Lakini ni ngumu wakati mwingine kutofautisha kati ya kulalamika na kuongea. Labda niwafafanulie kidogo, kulalamika ni pale ambapo mwanaume anafanya kitu na husubiri kikapita unaanza kulia, au kuongea kana kwamba unaonewa na kumlalamikia.

Lakini kuongea ni pale ambapo mwanaume anafanya kitu, unasubiri baada ya muda, akili zenu zimetulia, hamuwazi mambo mengi basi unamuambia lakini mume wangu kwanini usingefanya hivi na vile, unampa sababu za yeye kufanya mambo kwa namna ambayo unataka wewe.

Sasa kwa mfano, ana tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani, badala ya kila siku wewe kulalamika na kulia pale anapokuja saa sita usiku hembu kaa siku moja mmetulia na muambie. Unajua mume wangu, nakuambuia uwahi kwakua siwezi kula chakula peke yangu, na mimi ikishafika saa nne siwezi kula kabisa.

Kwanini usiwe unawahi hata kabla ya hapo au ukaja ukala chakula halafu kama ni kutoka na marafiki zako ukatoka. Maana wakati mwingine unachelewa hata wewe kwa afya yako si nzuri, kama ni pombe angalau unywe ukiwa na kitu tumboni.

Unakuja unakula ukishashiba ndiyo unaenda kupata bia hamna shida, lakini hapa naona kabisa unaweza hata pata vidonda vya tumbo. Tumbo likiwa halina kitu daaa. Hapo anakuelewa kwakua umeongea kama mtu mzima, si kama mwanamke anayeonewa, ndiyo hao ni watu wawili tofauti.

Hivyo hembu jaribu kujifunza mbinu hii, si lazima ifanye kazi kwa kila mwanaume lakini hutaumia kwa kujaribu, ni muhimu kujua namna akili ya mwanaume inavyofanya kazi kama unataka kumdhibiti.
 
simba jike

Senior Member
Mar 23, 2017
182
1,000
We acha hela ya matumizi ya kutosha weekly or monthly watoto waende shule, mgegedo wa hadhi ya juu, uwe na funguo za getini na mlango mkubwa..... Rudi muda utakao wala sikuulizi ila hakikisha chakula cha jioni saa mbili mpk mbili unusu tumechelewa saa tatu "LAZIMA UWEPO MEZANI"
 
Espy

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
69,729
2,000
We acha hela ya matumizi ya kutosha weekly or monthly watoto waende shule, mgegedo wa hadhi ya juu, uwe na funguo za getini na mlango mkubwa..... Rudi muda utakao wala sikuulizi ila hakikisha chakula cha jioni saa mbili mpk mbili unusu tumechelewa saa tatu "LAZIMA UWEPO MEZANI"
Kama hayupo ajitahidi ale hukohuko si ndio!!!
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
43,844
2,000
We acha hela ya matumizi ya kutosha weekly or monthly watoto waende shule, mgegedo wa hadhi ya juu, uwe na funguo za getini na mlango mkubwa..... Rudi muda utakao wala sikuulizi ila hakikisha chakula cha jioni saa mbili mpk mbili unusu tumechelewa saa tatu "LAZIMA UWEPO MEZANI"
Alaa...wala huhofii usalama wa mumeo??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom