Wanawake hupendelea zawadi gani?

Wanawake hupendelea zawadi gani?

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Posts
8,597
Reaction score
1,690
Zawadi ni zawadi, muhimu ni Caring anayopata kutoka kwa mwanaume Wanaume wengi (si wote) hudhani kwamba kumpa mwanamke zawadi kubwa, au kumnunulia kitu cha thamani kubwa kama gari au nyumba au kumfanyia jambo kubwa kunampa alama kubwa (maksi) na ni kuonesha mapenzi makubwa na kwamba kwa kufanya hivyo basi mwanamke hastahili kutokuwa na furaha.
Ukweli ni kwamba kila zawadi au jambo unalofanya kwa mwanamke lina nafasi sawa au maksi moja tu kati ya mia, hivyo basi ukimnunulia gari unapata maksi moja, ukimjengea nyumba unapata maksi moja, ukimnunulia pipi unapata maksi moja, ukimbusu unapata maksi moja, ukimsaidia kufua nguo unapata maksi moja, ukimpeleka vacation nje ya nchi unapata maksi moja, ukimkumbatia unapata maksi moja, ukimpa neno la kumtia moyo unapata maksi moja nk.
Ukiongea naye kwa kumsikiliza unapata maksi moja, ukimununulia chocolate unapata maksi moja, ukimnunulia kiatu cha kisasa unapata maksi moja pia.
Kwa mwanamke zawadi zote zina thamani sawa, iwe kubwa au ndogo, kumfanyia vitu vidogo vina thamani sawa na kumfanyia mambo makubwa, hii ina maana kwamba kumpa zawadi kubwa au zawadi ndogo humpa furaha sawa.
Hivyo basi si kwa vile mkeo unampa kile anachikitaka ndio iwe sababu yaw ewe kurudi nyumbani muda unaotaka na kufanya yale unayootaka.
Unaamini pay cheque yako ina point nyingi (maksi 80) kuliko pengine kumsaidia mkeo kutandika kitanda (maksi 1) hajui kwa mwanamke kuwa na pay cheque kubwa kuna maksi moja na kumsaidia kutandika kitanda kuna maksi moja tu.
Unapotaka kumuelewa mwanamke huhitaji kuwa logical bali emotional, mwanamke yupo after romance, jinsi unavyompenda, unavyomsaidia vitu vidogo, unavyomsikiliza, unavyombembeleza, unavyompa muda wa kuwa pamoja na kufurahia, unavyombusu, unavyomkumbatia, unavyomtia moyo, unavyocheza naye nk, kwake ni muhimu kuliko kununua gari au nyumba na kuamini kwamba hapo mwanamke atakuwa na furaha na hana sababu ya Kutokuwa na furaha.
Unaruhusiwa kumfanyia mambo makubwa sana lakini kumbuka anza kwa kumfanyia mambo madogomadogo kwanza.

Kwa kuwa umefanya mambo makubwa haina maana kwamba hutakiwi kufanya mambo madogo na kwamba mambo makubwa au zawadi kubwakubwa ukimpa hana sababu ya Kutokuwa na furaha na kuona unamjali.





 
Kila mtu na taste yake
Mama yako anapenda vitenge na mabazee, dada yako anataka bikini
 
Hapo juu umeiweka clear sana!!!!!
Tunatofautiana wengine wanapenda mawigi...mi ukinipa gari
Nitakubeba juu juu
Source: Boflo
 
Duuu! Kumbe Lema anaweza kuwa mojawapo ya zawadi wanazopenda wanawake eee haha hahaaa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Zawadi nzuri sana unayoweza kumpa mwanamke wako ni matumizi ya condom pale unapochepuka kufanya mazoezi na timu za mchangani.

Najua wengine hawatanielewa lakini ukweli ni kuwa KAMA UNAMPENDA UTAMLINDA.

Shkamoo Blaki Womani.
 
Last edited by a moderator:
Zawadi nzuri sana unayoweza kumpa mwanamke wako ni matumizi ya condom pale unapochepuka kufanya mazoezi na timu za mchangani.

Najua wengine hawatanielewa lakini ukweli ni kuwa KAMA UNAMPENDA UTAMLINDA.

Shkamoo Blaki Womani.
Babu Asprin una mambooooo, ndiyo maana nilikataa kuwa msiri wako.
 
hahahaha Matola acha ubahili hujui wewe ni ATM lol......waweza toa mshahara wako wote zawadi baada ya hapo mikono kichwani lol
Haya wifi yako amenipigia simu nataka kwenda kumuona sasa hivi, niambie nimpelekee zawadi gani ya kawaida, Ice cream au .....
 
Haya wifi yako amenipigia simu nataka kwenda kumuona sasa hivi, niambie nimpelekee zawadi gani ya kawaida, Ice cream au .....

wifi yangu hataki makuu tafuta perfume nzuri sio marashi ya zanzibar lol
 
Zawadi nzuri sana unayoweza kumpa mwanamke wako ni matumizi ya condom pale unapochepuka kufanya mazoezi na timu za mchangani.

Najua wengine hawatanielewa lakini ukweli ni kuwa KAMA UNAMPENDA UTAMLINDA.

Shkamoo Blaki Womani.

Babu habari ya machimboni.........nimeanda mbuzi 2 na mbege dramu za kutosha
 
Babu Asprin una mamboo, ndiyo maana nilikataa kuwa msiri wako.

Taratibu msiri wangu Binti.com .... hilo neno "mamboo" wakware na vijana wa kisasa hawachelewi kulisoma vibaya na kuwazuia mambinti zao nisiwakague.

Haya hebu nambia hayo "mamboo" yangu yakoje?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom