Wanawake akili zenu dah! Kila siku mnanipa mafundisho in a hard way

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
17,624
47,250
Tz kila kitu siasa. Ukienda kanisani siasa,sokoni siasa,hospitali siasa,ajira nazo siasa. Hadi bongo movie nao wanatuletea siasa. Kwa ufupi siasa imekuwa jipu ndio maana binafsi nashinda MMU tu.

Any way twende direct kwenye point.

Miezi minne iliyopita nilihama Dar nkaja kujichimbia pande za Songea maana Dar brand imeshuka. Kufika nikapokelewa na binti mmoja,sio mzuri ila kwenyr wabaya hayupo.

Kutokana na ugeni,huyu binti akawa kampan yangu kubwa kiasi ikapelekea mioyo ikaongea.

Baada ya uhusiano wetu kudumu kwa miezi mitatu,sasa juzi tumetoka kiwanja nkampeleka kwao na mimi nkarudi home. Jana mida ya jioni akanitumia text inasomeka hivi:

"Hellow honey, sorry kuna kitu nimekuwa nikijaribu kukwambia kwa muda mrefu ila sikujua nianzie wapi. Mimi nina mpenzi wangu ambae nilikuwa nae kabla hata hujaja Songea,kwa ukaribu tuliokuwa nao nikajikuta naingia mapenzini. Samahani sana sidhani kama tutaweza kuendelea mimi na ww"

Nikajaribu kumuuliza kwa undani,akasisitiza kuomba msamaha ila hatoweza kumuacha huyo mwingine maana yuko nae kwa muda mrefu.

Baada ya kujifkiria sana,kidume kwavile nilishalewa penzi la mrembo ikabidi nimwambie tuendelee tu ila asimuache jamaa wake. Ila akagoma.

Njia nzima toka job hadi nakaribia home nabembelezea hapo.

Nikamkuta sehemu ananisubiria ( maana niliomba tuonane face to face)

Baada ya kukutana,mwisho wa siku binti akaniuliza swali ambalo jibu lake nikatoa boko hadi ikapelekea kuandika huu uzi.

Aliniuliza "Hivi ungekuwa wewe katika situation yangu ungefanya nini?"

Kwanza nikamkumbuka Catheline wangu wa Dar. Alafu ilikumuondoa wasi wasi nikamwambia:

"Najua mamii ugumu wa maamuzi ulionao,ila nikawaida usijali mbona hata mimi nina mpenzi japo yupo Dar kwasasa lakini me na ww tuko poa tu"

Dah,akabidilika ghafla. Kwamba alikuwa ananitania kunipima tu. Akanipa na simu yake niangalie but sikukuta chochote cha ajabu. Nikiwa bado najiuliza akachukua simu akakuta ni kweli nna girl akazidi kufura kwa hasira.

Kipindi najiuliza nimpoze vipi,ikaingia text kwa namba ngeni ikiniita Honey,ndio ikamtibua kabisa.

Kiufupi kwasasa nipo single huku Songea.

Najiuliza,hivi niutani gani huu aliouanzisha yeye?

Utani kaukomalia kwa masaa mawili hadi nikajua kweli.

Any way,acha aende tu.
 
Mbona kitu kidogo hicho wala usiumize kichwa ww piga kimya akijirudi mwenyewe endelea kumfaidi akizingua mazima endelea na Catherine wako

Tatizo mabinti wa siku hizi wanataka wapenzi waishi kama wako kwenye ndoa wakati mahusiano mengine ni kwa ajili ya kuwekana mjini tu sio yataishia kwenye ndoa
 
Teh dah umechotwa umeingia king kweli. Umeuza ramani ya vita.

Bro sio kila 'mchepuko' unaweza kuuambia ukweli. Hata akasirike vp


Hamna haja ya kummbembeleza..... Songa mbele
michepuko ina shidaaaeeeee
 
Mbona kitu kidogo hicho wala usiumize kichwa ww piga kimya akijirudi mwenyewe endelea kumfaidi akizingua mazima endelea na Catherine wako

Tatizo mabinti wa siku hizi wanataka wapenzi waishi kama wako kwenye ndoa wakati mahusiano mengine ni kwa ajili ya kuwekana mjini tu sio yataishia kwenye ndoa
Nshapotezea tayari. Life linasonga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom