Pull up
Member
- May 19, 2015
- 22
- 6
Habari wana JF,
Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali na mchango wa wadau wa mtandao huu na kuona busara zikitoka kwenu kusaidia wale wanaohtaji ushauri. Mimi nina langu linanikera, hili linafanywa na akina dada wengi mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27 ni askari wa JWTZ, nimejiunga mwaka 2008.
Katika kusaka maisha nilibahatika kukutana na binti mmoja ambae tulianza mahusiano takribani miaka 3 iliyopita, kwa bahati nzuri au mbaya nikawa nimempa ujauzito, kwa kuwa nilikuwa nampenda nikaamua kwenda kwao na kutoa posa ili nipangiwe mahari. Nashukuru Mungu mambo yakaenda sawia.
Kwa kipindi hiko yy alikuwa anaishi kwao (nje ya mkoa niliopo mm), basi baada ya kutoa posa nikapangiwa mahari nikaambiwa nikijikamilisha niipeleke ila wakasema nimchukue nikakae nae kwani mimba natakiwa niilee mwenyewe basi nikamchukua binti wa watu mpka kwang tukaanza maisha. Muda wa kujifungua ulipokarbia nikampeleka kwao na akajifungua salama, nikamrudisha ili tulee mwana.. Tukakaa pamoja mpka mtoto wetu akafikisha miez tisa.
TATIZO LIKAJA HAPA:
Tangu kipindi nianze kuishi na huyu mwenzangu ugomvi wangu mimi na yeye ni kutokuniamini mm kwa kigezo "nyinyi wanajeshi nasikia hamjatulia" kauli hyo ikiambatana na wivu uliopitiliza, kiasi kwamba akikupgia simu hata uwe kazini ukawa unatumika basi ujiandae kujibu ulikuwa unaongea na nani na ukirudi nyumbani unakuta kanuna hivyo umbembeleze ili muende sawa na kiukweli ndugu zangu mimi sio mchepukaji hata kidogo pia tangu niwe nae hajawahi kunifumania wala kuona napigiwa simu tatanishi, wala sieleweki mipasiwedi kwenye simu yangu.
Hapa nilipo nahisi tunakoelekea mimi ntashindwa kuendelea nae ila kinachoniuma ni mtoto wang na ukizingatia mm ctaki kuzaa na wanawake zaidi ya huyu. Kwasasa yupo kwao kaenda msibani na hatuna maelewano kisa profile picture ya wasap nimemuweka dadangu (mtoto wa mama yake na kakaangu tuliye kutana kwa baba) yuko form six Tanga, yeye anadai hamjui hvyo ni kimada wangu. Nimejarbu kumtumia nambari ampgie hataki, basi nikamwambia asome status niliandika "I miss u my lovely sister" anadai haijalishi.
Jamani nawaombeni kina dada mjue kuwa si kila mtu ni malaya na hakuna kipindi nilichoona jeshini wanafundisha kutongoza hii ni mtu mwenyewe. Pia wadau mnisaidie mawazo nifanye nini na uhusiano huu maana natumika sana, sasa naona mbeleko inachanika niliyembeba anarukaruka mgongoni kutwa kubembeleza tu.