Wanaume wenzangu wa Dar, tujifunze kukubali tunapokataliwa

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,522
Habari za asubuhi wakuu, tumaini langu ni wazima wa afya,

Nimeonelea nilete bandiko hili kutokana na tabia tuliyokuwa nayo wanaume wengi japo hapo juu nimesemea kwa wa Dar hata mikoani mnahusika.

Ifahamike kwa mtoto yoyote wa kiume kutongoza ni jambo la fardhi(wajibu) Na swala la kukataliwa ni Sunnah (ni mwenendo ambao hata babu na mababu zetu waliupitia).

Wengi tumekuwa wagumu kukubali matokeo hasa yanapokuwa kinyume na Tulivyokuwa tunatarajia na hasa tunapokataliwa.

Tumekuwa wagumu kulikubali hili kwamba si kila mwanamke basi utamlala au utakuwa naye, tukubali wengine watupite.

Imekuwa ni tabia iliyojengeka kwetu wanaume wengi tukikataliwa na mwanamke, basi tunajenga chuki vitisho wakati mwingine hata kejeli na kueneza kasumba kuwa yule mwanamke hivi na vile.

Tujifunze kukubali matokeo na hasa yanapokuwa kinyume na matarajio yetu, pia tuwe wavumilivu wa kuyapokea matokeo yaliyokinyume na fikra zetu.

Tukubali tunapokataliwa, maana kukataliwa na mmoja si wote ,na huwezi kukubaliwa na kila mwanamke, wengi tuna maneno yetu ya kujifariji na hasa yanapotukuta masahibu haya, "Acha nitafte pesa, pesa ndo kila kitu, jamani Unaweza ukapata pesa na mwisho wa siku akatokea wa kukusumbua na pesa zako.

Tujifunze kitu kimoja, jambo la kukataliwa ni jambo la kimaumbile, kila mwanadamu lazima ulipitie, uwe tajiri masikini maarufu na mengineyo, hili uwezi liepuka.

Mfano ulo hai, binafsi ninayo listi ya wanawake walionikataa na wakati mwingine unajiuliza huyu ananikataa kwa sababu gani au ninakasoro gani, basi unachokuja kugundua kila jambo lina majaaliwa na halina sababu,(kupendwa hakuna sababu) na huwa hakuangaliii umaarufu wa mtu au cheo au pesa zake. Pia hata kukataliwa pia hakuna sababu,unaweza ukawa na kila kitu na pia ukamwagwa.

Na huwezi jua mtu alokukataa mungu anakuepusha nini? Nilishawai kataliwa na msichana mmoja baada ya muda kupita akaja kugundulika na ukimwi, dah nilimshukuru sana mungu na kujiapiza kuwa mwanamke akinikataa huwa simlazimishi maana sijui kwanini hataki labda lipo ambalo Mungu ananiepushia, sasa tukiwa vin'gan'ganizi ndo tutakutana na zile kauli "Mtoto akililia wembe. Mtamalizia wenyewe.

Wito wangu kwenu tuache matusi kejeli chuki, inawezekana asiwe na tatizo lolote la kiafya ila ikawa hujapangiwa, maana si kila mwanamke utakuwa naye, ndomana kumepatikana dada shangazi mama wadogo, n.k wengine acha wabaki kuwa dada zetu wa hiyari shemeji zetu japo siku izi haina ushemeji ila inapobidi hakuna jinsiiii.

Siku njema wanaume wenzangu wa Dar na mikoani, pia wadada Mtupunguzie shit Tunapowatokea.

Kama hamtutaki basi tujibuni kistarabu, ukweli huwa tunaumia na wakati mwingine mnaweza kutusababishia madhara kwa tunaokuja wapata baadae maana mioyo inakuwa ishakufa, akili zishavurugwa na tunachoangalia hapo ni kisasi tu.

Ni hayo tu;

Nyoka mzee
 
Hio inaitwa husinikubali haraka haraka
Apo chacha ndo tunapoisoma namba ,kusubiriwa jibu la ndio ni sawa na kupanga foleni ya kuhakiki tin nomber maana kipindi ww wasubiri wenzio wanahakikiwa mpaka foleni yako ikifika ww hoii na mtoa huduma hoiiii
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Wanaume wengine ukiwakataa ndio wanakununia kabisaaa
Kama mlikuwa mnasoma wote anaacha. . .ukaribu anautoa

Bora umewaambia
ww tena hahahah ,ila muwe mnapunguza basi na yale majineno yenu ya shombo kidogo,maana unaweza ukaambiwa maneno na mtoto wa kike mpaka ukajihisi hata jinsia yako nayo ni Ke

mtuhurumie hatukate kukataliwa tunachokataa yale maneno yanauma
 
Back
Top Bottom