Wanaume wanatuchosha lakini hatusikii na wala hatuoni.

Ndugu yangu Panga la shaba,hiyo picha hapo inanitisha mno,honestly am not confortable.Please,am sorry but can you do the changes.Please my dear.............
 

Kabla ya kupewa pesa huyo mdada alikolezwa kwa KATERERO kumbe tusemeje, miezi mitatu huwezi kumwani mtu hivyo
 
ajitoe ufahamu tu, pesa itarudi, hata kama itachukua miezi ila mabango na mikimiki ntakayompa lazima arudishe pesa

hapo hakuna cha mapenzi hao ni kupambana tu lol
 
wangechukua hamsini ingekuwa vizuri,millioni sita?? Wanaume wengine jamani!!! kweli wanatisha....nafurahi haya maneno yanapotoka kwa mwanaume....Bwana Yesu Rudi tu!!!

Nani mwenye kosa kati yao??? Mimi naona huyo dada ni Msheeee.......malizieni. Mbona wake zetu wa ndoa tukiomba hiyo amount hatupewi????kwani huyo mwanaume alimfanyia nini kizuri hadi kamkopea 6m?? au katerero????????//
 
Mkuu sio viherehere, kushikwa na penzi ndo kunasababisha haya. Iko siku deni litaisha, na huyo mhuni hatafika popote na udhulumaji wake.

Aisee ataniibia mapenzi tu sio pesa, ntapambana nae naye mpaka akome hata polisi nampeleka ili mradi pesa yangu irudi
 
pole sana kwa huyo dada,inaonyesha huyo kijana ndio tabia yake.angemtahadharisha na huyo dada mpya.kwa dizaini hiyo,atapawapata wadada wengi tu.nahisi ngao yake anayoitumia ni kujifanya ana mapenzi mazito kwa hao wasichana.huyo ni tapeli,bora akomolewe ili aache utapeli wake
 
Bado sijaona Logic ya hilo tukio hadi kupelekea kuhusisha wanaume wote.. Huyo jamaa amepewa nafasi na yeye ameitumia kulingana na roho yake mbaya, na ujambazi wake..

Hii ni sawa sawa na kusema wanaume wote ni vibaka au majambazi kwa sababu tu, siku zote wanaofanya na kukamatwa kwenye hayo matukio ni wanaume.

Wakati mwingine ninamu-admire Miss Judith kwa kauli zake za kuwavulia nguo wanaume kabla ya ndoa..Kama umefikia nafasi ya kumpa mwili wako auchezee, sio vigumu kukopa na kumtafutia pesa. (kwani pesa ina thamani gani kama mwili wako)..Aende tu kwenye vituo vya polisi watamsaidia kumtafuta huyo jamaa
 

Kipenda roho Michelle!!.......Si unasikia jamaa alionyesha mapenzi moto moto "jamaa kuonyesha mapenzi mazito haswa mpaka wenzake wakawa wanaona mamsapu kapata bwana wa ukweli" akadhani amepata kumbe amepatikana! Hakuna mapenzi yoyoye ni TAPELI TU!
 
Hapo Kaka mpendwa umenena(Nowadys mabinti/wasichana/wanawake hawajali utu wao.Utu, thamani ya mwanamke iko katikati ya miguu yetu jamani,kabla ya kutenda tufikiri kwa kutumia vichwa na sio hisia).Hata mimi sioni haja ya kulaumu wanaume wakati wote,au kulaumu wanaume kila wakati.Kwani wanatubaka?Na kama umeamua kutenda la ndoa kabla ya ndoa kama ambavyo wengi wanafanya then kuwa makini kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale yanayohusiana na sekta hiyo.
 
Kipenda roho Michelle!!.......Si unasikia jamaa alionyesha mapenzi moto moto "jamaa kuonyesha mapenzi mazito haswa mpaka wenzake wakawa wanaona mamsapu kapata bwana wa ukweli" akadhani amepata kumbe amepatikana! Hakuna mapenzi yoyoye ni TAPELI TU!

Hayo mapenzi motomoto ndo yapi,mpaka utoe milioni sita....Mungu pitisha mbali,hata kama ni matamu namna gani sitaki kitu cha kuniondolea uwezo wa kufikiri....khaaaaaaaaaaaaaa!
 

Ni kweli dada unachokisema. nilikuwa nasikiliza documentary moja ya porn stars, wengi wanaojihusisha ni wale ambao wana background ya kuwa abused. Point ni kwamba, wasi mwanamke akishavua, au akivuliwa chupi yake, anajiona thamani yake imeshuka (iwapo hakufanya kwa hiari yake), au atamthamini yule aliyemvulia kwa hiari yake na kumfanya yeye ndio kila kitu. Kumbe unakuta mwanaume alikuwa na nia ya kupita tu kwa muda..matokea yake mwanamke ana baki na machungu ya kutendwa.

Kwa mwanamke, ukishamvulia mtu nguo, basi unatakiwa ujiandae kwa lolote wakati wowote..wapo wananegotiate wanafanikiwa kufika hadi ndoa, lakini still wengi wao ndo unakuwa mwanzo wa kutendwa, na kujuta kwa nini waliingia kwenye mapenzi..
 
Mapenzi ya hivi hata shetani angeyapa heshima yaani miezi mitatu then ushaenda kujiweka bond kwa mijihela mingi hivyo kwa stranger. Ama kweli wanawake mnapenda vibaya nikiwaita hamnazo sio kama ninawatukana ila ninawaamsha mtoke usingizini hata kama akikuambia ndoa ndani ya kipindi kifupi hivyo shituka huyo analake jambo.
 

Mpe pole, ndio maisha... Shetani anatembea kwa miguu, tunakula nae, tunasali nae, tunachekanae, tunalala nae, tunapanda nae dala dala, tunampalift, tunamnunulia vocha nk nk. TAKE CARE GUYZ
 


Ebu niambie ndugu yangu. Kweli huu si ni unyama jamani. Dada aliniomba ushauri nikamwambia asali tu amwachie Mungu, ila kwa kweli jamaa kuna siku tu litampata la kumpata, machozi ya mtu na jasho la mtu haviwezi kwenda burem maana hapo atafanya nini, hana cha ushahidi wala nini. Kwa kipindi kifupi tu alimwamini akadhani labda atakuwa mwenzi wa maisha yake. Yaani sijui kwa nini huwa tunawaamini kwa haraka kiasi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…