wako wanawake wa hivyo wasiojua wajibu wao kwa waume zao
Au yawezekana ushagamjengea mazingira fulani ya kutokuamini
si mnaona majibu yao, hawa ndo wanawake wa dot com, hakuna adabu kabisa, mwanaume akiongea mwanamke nyamaza.
mwanaume ni nini?
Yaani we uanze kuaga tu eti naenda mkaoni kutafuta maisha bila kuelezea kiufasaha:-
Mfano
1. Unaenda kufanya kazi ambayo umeshaipata au ndo unaenda kuitafuta
2. Ya kuajiriwa au kujiajiri (kama ni kujiajiri hapa hapa vipi?)
3. Kama ni kwa ajiri yenu nyote si uende naye? Kama ana kazi ni issue nyingine tena.
Hivi wewe mwanaume mke wako akikwambia anaenda kutafuta maisha mkoa tofauti na mlipo unamruhusu?
mkuu wala si kuhamia, ni kwenda siku mbili tu kuangalia fursa mkoa mwingine tu na kurudi lakini unaambiwa unaenda kwa mwanamke wako.
Fursa gani mkuu, ndoa ni majadiliano, huwezi kuamka na kusema eti unaenda kuangalia fursa siku mbili, elezea ni kipi ulichokifikiria, target ni nini, mipango ikoje uone kama huruhusiwi.
Ndoa inadumishwa na mawasiliano chanya, uwazi na uaminifu. Hata ungekuwa wewe mtu akija akakuambia naenda kutazama fursa mkoa fulani kwa siku mbili huwezi kumwelewa bila kutoa ufafanuzi wa kina.
Mawasiliano ni kitu kikubwa sana kwenye ndoa, kushirikishana katika mipango ni muhimu na inajenga uaminifu.
Mkuu kama kila kitu nitahitajika kuwa details kiasi hicho basi kazi ipo, nadhani huwajui wanawake wewe.