Ipo hivii wanaume wenzangu leo nataka tujulishane juu ya hili jambo mwiba kwetu. Maana hii taasisi iitwayo ndoa imegeuka na sio kuwa sehemu ya furaha na amani kwetu ...imegeuka kuwa sehemu ya majuto makubwa, mauwaji ,ushirikina na utumwa ulio kithiri kwa jina la ndoa.
Wanaume wengi tumejikuta leo hii nyumba tulizo zijenga kwa pesa na jasho la uchungu ili tufurahie maisha huku tukinunua vitu vya thamani ili viweze kusaidia kuleta furaha katika hizo nyumba lakini imekua kinyume chake. Zaidi ya maumivu na mitafaruku isio kuwa na maana.
Wanaume tumejikuta tukihangaika kila pande ya dunia kuhakikisha tunapata chochote ili tukale na wale tunao jiongopea tunawapenda kwa furaha lkn mwisho wa siku juhudi zetu zimekuwa miiba kwetuna kuonekana hakuna tunacho kifanya yaani just nothing.
Wanaume tubadilike Kama wenzetu jinsia ya pili ilivyo amua kubadilika yaani kuanzia leo tunaoa kwa mission maalumu na haya mambo ya shida na raha tuwaachie babu zetu.
Mifano
......tuoe kwa sababu tunataka watoto ...tuoe kwa sababu Kuna kazi inataka mtu Alie oa.......just marry for a mission.
Tukiweza kuoa kwa mission haya maumivu na mabalaa tunayo pitia yataisha na tutageuza kibao kile Cha wanaume wanawahi kufa kuliko wanawake.
Mwanaume tutafute hela kwa ajiri yetu na mipango yetu sio kwa ajili ya kuwapa watu wasio na shukrani .....watu wasio weza kukithamini pale usipo kuwa na kitu.
Wanaume yale Mambo ya kuvaa kiatu kimoja miaka Saba na hela za kubadilisha unazo ila umeamua kuvaa kiatu kimoja miaka Saba ili umridhishe mtu kwa kumrundikia viatu Hadi hajui avae kipi huo ni upuuzi na mateso ya kifala .
Wanaume tujipende na tuwapende watoto na baadhi ya watu(ke) watakao thamini michango yetu kwao.
NB
Kuna mbuzi watakuja kusema man down....ila ninacho waambia tu kuwa nilicho kiandika hapo ndio ninacho kiishi na naishi maisha Safi kabisa na situmikii gereza wa kifungo chochote kile am just living my own life ....no one to judge me....no one to make explanation for what I did ....na ninaishi nikijua watu wanakuja maishani na kuondoka kwa kihiyo kuachwa/kutoswa kwangu ni sherehe sio majonzi Kama ilivyo kwenu ....ni furaha kwa sababu nakua nimepewa fursa ya kujua kwingine kupoje [emoji39][emoji39][emoji39]
Tafuta pesa nyingi .......jipende.......wapende watoto.....wapende baadhi ya ke wanao kupa furaha..... Na usikipoteze.