Hivi inakuwaje, Mara zote kama sio nyingi, Mwanaume/wanaume tunapoongea na wapenzi wetu/wake zetu, huwa tunaongea kwa Hasira sana, Mpenzi akiuliza "Upo wapi? Mtu anajibu.. "Unataka niwe wapi? Yaani tunajibu kwa ghadhabu kweli kweli...
Sasa Ngoja "Mchepuko" Upige simu, hata kama swali ni la kizushi, Utajibu kwa Upole na kwa kubembeleza.. " Nipo Ofisini Mama, nikitoka nitapita kukucheki sweetie "...
Swali, ni kwa nini tuna behave like that? Kwann wanaume tunakuwa wakali sana kwa wake zetu, na tunakuwa wapole sanaaa kwa Michepuko????? What's the secret behind such attitude?
mrudie Mungu
acha kumtesa mke wako
Ukioa mke uliepangiwa na MUNGU kamwe hutamdharau wala yeye hatakudharau,mtaheshimiana na kupendana sana siku zote na nyote hamtaona sababu za michepuko,lakini watu wengi hubeba wake/waume wasiokua wakwao kwa matamanio tofauti tofauti ya kimaumbile au fedha,na mkisha kaa kwa muda ule uhalisia unakuja na unaanza kuona ulienae hakufai,hilo tu ndilo linaloweza kusababisha haya uliyosema...
Mi akiniulizaga namie namjibugu ' niko nalewa bar' hata kama saa tatu asubuhi nyambaf
Ukiwa na mchepuko,lazima utakuwa mkali/jeuri kwa mkeo!Dawa ni KUBAKI NJIA KUU
Ukiwa mpole kwa mke wako andika "UMEEUMIA"
Sasa.. Wanasema njia kuu yako, ndio Mchepuko wa wenzio. Utavumilia wenzako wamchepukie mkeo wewe umetulia tuu....
Ukiwa mpole kwa mke wako andika "UMEEUMIA"
Nimejivika uhusika tuu, ili nisionekane nashambulia mtu. Mimi sifanyi hayo, ila nimeshuhudia marafiki zangu wengi wakiwajibu kwa ghadhabu wapenzi wao, na kuwabembeleza Michepuko yao...
Ila asante.