Wanaume siku hizi mbona mnalia lia sana?

Wanaume siku hizi mbona mnalia lia sana?

cristela

Senior Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
138
Reaction score
297
Hata maandiko matakatifu yameandikwa mwanaume utahangaika juani ili umlishe mkeo na mwanamke atazaa kwa uchungu, sasa imekua siku hizi wanaume kumhudumia mwanamke imekua ni kulia lia sana mwanaume wa ukweli anatakiwa ajue mpenzi wake au mke anamhudumia vipi.

Hivi mnadhani nyie wavulana unakua hujaoa una mpenzi tu unataka aishi vipi unakuta unatoa vielfu 50 unalalamkika mpaka povu linakutoka unataka kumiliki msichana mrembo mzuri huku unatoa kihamsini unalalamika sana starehe gharama ukiona vyapendeza ujue vimegharamiwa.

Ebu kueni wastaarabu basi kutwa kulia lia humu JF, mnawadhalilisha sana kina dada anakuja kwako kajigharamia mwenyewe mapouda nini unamgaragaza unamtindua wewe ukimpa kihamsini unalalamikaaaaaa sasa unatakaje?

Acheni hizo basi ukimtoa out akija na rafiki yake wakinywa savana tu mnalia sasa mnataka wanywe viroba? Au safari?
 
Sisi kazi yetu kuwarea nyie ndyo maaana hamuishiw mizinga mkitaka kujua nyie mnashida utaskia "tuna taka haki sawa" alafu mnasaau mnasema tukiwezeshwa tuna weza teh teh teh teh
 
hata maandiko matakatifu yameandikwa mwanaume utahangaika juani ili umlishe mkeo na mwanamke atazaa kwa uchungu.. sasa imekua siku hizi wanaume kumhudumia mwanamke imekua ni kulia lia sana mwanaume wa ukweli anatakiwa ajue mpenzi wake au mke anamhudumia vipi hivi mnadhani nyie wavulana unakua hujaoa una mpenzi tuu unataka aishi vipi unakuta unatoa vielfu 50 unalalamkika mpaka povu linakutoka unataka kumiliki msichana mrembo mzuri huku unatoa kihamsini unalalamika sana starehe gharama ukiona vyapendeza ujue vimegharamiwa...ebu kueni wastaarabu basi kutwa kulia lia humu jf ..mnawadhalilisha sana kina dada anakuja kwako kajigharamia nywenye mapouda nini unamgaragaza unamtindua wewe ukimpa kihamsini unalalamikaaaaaa sasa unatakaje? acheni hizo basi ukimtoa out akija na rafiki yake wakinywa savana tuu mnalia sasa mnataka wanywe viroba? au safari?

"unamgaragaza unamtindua" Haya maneno jaman aseme mwanamke anayejiuza, Kama mmekubaliana na ni mme na mke kujamiiana is two way thing. Hata wewe you enjoy. Unapohusisha hicho kitendo na idadi ya fedha ndo umalaya wenyewe huo
 
Cristela kama upo Dar
naomba nikununulie chakula cha jioni leo!
 
Kumbe hilo mnalijua sasa haki sawa inatoka wapi na kwenye andiko gani
 
Mnashangaza, raha tunapata wote, tena nyie mnapata raha mara mbili yetu lakini mnataka mlipwe, jamani tusaidiane kwa chochote alichonacho mwanaume, kama ni usafi tutaoga wote bafu moja.
 
kipengele cha kuhongwa tafsir yake ni kuhangaika kwa jasho? huo uchungu mnazaa wapi wakat trend ya operation siku hz imekua kama fashion kwa wadada...
 
Back
Top Bottom