Wanaume njooni jandoni

Wanaume njooni jandoni

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,077
Reaction score
17,264
Unapata girlfriend/mchumba anakupenda na kukujali kwenye kila hali, anakupenda kupitiliza mpaka unajiona mwenye bahati kuliko wengine, dada wa Watu anajiachia kwako akijua wewe ndo utakuwa wake wa milele. Tatizo letu wanaume huwa linaanzia hapa, tunapopendwa kupitiliza huwa tunajisahau na kuanza kujiona kama miungu watu, tunaanza kuyachukulia mapenzi yake for granted, tunamuona anayetupenda kama vile amekosa mwingine wa kumpenda.

Hatujiulizi anafuatwa na wangapi na anawakatalia kulinda mapenzi yake kwetu, hatujiulizi ni wangapi wapo tayari kuwa naye ila wameikosa hiyo nafasi ukapatiwa wewe unayeichezea na kumuona aliyekupenda kama kapotea njia vile. Tumejisahau na kusahau kuwa naye ana moyo na anaweza kuamua lolote muda wowote, tumesahau kuwa naye ana maumivu kama ambavyo sie huumia.

Tusipopendwa vile tunavyotaka, tumesahau kuwa mapenzi ni pande mbili na si upande mmoja. Siku wakiamua kuondoka huwa ndio siku tunayokuja kutambua kuwa alikuwa na mapenzi ya kweli, ndio siku utakayojua kuwa kuna mapenzi ya kweli hapa duniani, ndo siku utakayoshtuka kumbe kumekucha na wewe bado una usingizi. Unapopendwa sana usichezee bahati uliyopewa, usitoe nafasi kwa mwingine akaja kuichukua ile furaha ambayo ulitakiwa kuipata wewe, usitoe nafasi kwa yule anayekupenda akalia juu yako, usije kujutia muda, mapenzi hayaji mara mbili, yakienda hayarudi, take it from me.
 
Unapata Girlfriend/Mchumba Anakupenda Na Kukujali
Kwenye Kila Hali, Anakupenda Kupitiliza Mpaka
Unajiona Mwenye Bahati Kuliko Wengine, Dada Wa
Watu Anajiachia kwako Akijua Wewe Ndo Utakuwa
Wake Wa Milele.
Tatizo Letu Wanaume Huwa Linaanzia Hapa, Tunapopendwa Kupitiliza Huwa Tunajisahau Na
Kuanza Kujiona Kama Miungu Watu, Tunaanza
Kuyachukulia Mapenzi Yake For Granted, Tunamuona
Anayetupenda Kama Vile Amekosa Mwingine Wa
Kumpenda.
Hatujiulizi Anafuatwa Na Wangapi Na Anawakatalia Kulinda Mapenzi Yake Kwetu, Hatujiulizi Ni Wangapi
Wapo Tayari Kuwa Naye Ila Wameikosa Hiyo Nafasi
Ukapatiwa Wewe Unayeichezea Na Kumuona
Aliyekupenda Kama Kapotea Njia Vile.
Tumejisahau Na Kusahau Kuwa Naye Ana Moyo Na
Anaweza Kuamua Lolote Muda Wowote, Tumesahau Kuwa Naye Ana Maumivu Kama Ambavyo Sie Huumia
Tusipopendwa Vile Tunavyotaka, Tumesahau Kuwa
Mapenzi Ni Pande Mbili Na Si Upande Mmoja.
Siku Wakiamua Kuondoka Huwa Ndio Siku
Tunayokuja Kutambua Kuwa Alikuwa Na Mapenzi Ya
Kweli, Ndio Siku Utakayojua Kuwa Kuna Mapenzi Ya Kweli Hapa Duniani, Ndo Siku Utakayoshtuka Kumbe
Kumekucha Na Wewe Bado Una Usingizi.
Unapopendwa Sana Usichezee Bahati Uliyopewa,
Usitoe Nafasi Kwa Mwingine Akaja Kuichukua Ile
Furaha Ambayo Ulitakiwa Kuipata Wewe, Usitoe
Nafasi Kwa Yule Anayekupenda Akalia Juu Yako, Usije Kujutia Muda, Mapenzi Hayaji Mara Mbili, Yakienda
Hayarudi, Take It From Me.
Fact
 
Ndio mnafundwa hivyo mwenye masikio na asikie [emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Afadhali umetupumzisha na sisi,haya wape beg part yao,alafu ww kungwi nn maana sikuelewagi?
 
Wewe lazima utakuwa Ndindindi tu, mwanaume wa kweli yupo bize na kutafuta pesa za watoto za ada, kosa pesa uone kama hayo unayoyasema yatatekelezeka
 
Tatizo lililopo hivi sasa kuweza kutofautisha kati ya True Love na Gold diggers ni kikwazo ndio mana wengi wana kuta bahati kama hizi zina wapita. Mahusiano yamekuwa kama vitega uchumi kwa wengine huku wengine wakizidi kupoteza uaminifu na wenza wao
 
Jamani JANDONI si wanakatwa sweta tu na kusepa? kama vile maelezo na kichwa cha habari haviendani.
 
Tatizo lililopo hivi sasa kuweza kutofautisha kati ya True Love na Gold diggers ni kikwazo ndio mana wengi wana kuta bahati kama hizi zina wapita. Mahusiano yamekuwa kama vitega uchumi kwa wengine huku wengine wakizidi kupoteza uaminifu na wenza wao
Kweli kabisa.. Hii ni dunia ya Nguruwe, na sio watu tena..!!
 
Wewe lazima utakuwa Ndindindi tu, mwanaume wa kweli yupo bize na kutafuta pesa za watoto za ada, kosa pesa uone kama hayo unayoyasema yatatekelezeka
Maisha sio kutafuta hela tu... Know that
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom