Hapo hujajibu kitu. Kanuni ipi ya mahusiano? Inasemaje? Uhalali wa kanuni hiyo unatokana na chimbuko gani?
Ngoja ninyumbulishe.
Kuwa na mahusiano na ndugu yako wa karibu ni jambo baya.
Kwa kanuni za misingi ya kidini. Limekatazwa. Mtu anakataa kwa sababu za dini.
Hata kama mtu hakubali dini kama mimi, kanuni za kibaiolojia zinatoa sababu za kutokuwa na uhusiano na ndugu yako wa karibu, kwa sababu mnahatarisha genetic pool watoto kuwa na magonjwa.
Hivyo ni wazi kwamba, kiutu, ukaribu wa undugu unavyozidi, ndivyo jamii inavyoona mahusiano ya kimapenzi yanakuwa hayafai.
Hivyo basi, kuna sehemu hapo ukaribu huo unafifia mpaka mahusiano hayo yanaanza kuonekana yanaruhusiwa. Ndiyo maana kuna tamaduni nyingine, baadhi ya waarabu kwa mfano, unaruhusiwa kuoa au kuolewa na binamu yako.
Sasa, ukaribu huu wa kutokuwa na mahusiano unaishia wapi? Na unapotaka kuwajumuisha rafiki za mume/mpenzi wako wa zamani, unawajumuisha kwa minajili gani? Kwa uhalali gani?
Ndugu wanajulikana ni ndugu wa maisha. Hivyo katazo la kuwa na uhusiano na ndugu wa karibu ni la maisha. Hao rafiki wa mume/mpenzi wako wa zamani, wakisema wanavunja urafiki naye ili wawe nawe utawakubali? Vipi kuhusu rafiki zake wa zamani uliowajua ambao hana urafiki nao tena? Vipi kuhusu rafiki zake wa zamani ambao hukuwajua ambao wamepoteana hawana mawasiliano muda mrefu? Vipi kuhusu rafiki zake waliopoteana kutoka darasa la kwanza? Vipi kuhusu rafiki za kaka yake ambao si rafiki zake? Vipi kuhusu rafiki za rafiki zake? Vipi kuhusu rafiki za rafiki za kaka yake?
Uchunguzi wako wa nani atakufaa kwa minajili ya kutokuwa rafiki wa mume/m penzi wako wa zamani utaanzaje na kuishaje? Utaanzia wapi na kuishia wapi? Utajiridhishaje? Vipi mtu akikutongoza mtaani humjui, utaanza kwa kumpa hojaji ya kuonesha uhusiano wake wote yeye kumhusu huyo mume/ mpenzi wako wa zamani? Vipi kama yeye si rafiki wa mume/ mpenzi wako wa zamani, lakini ana rafiki ambaye ni rafiki yake?
Vipi kuhusu wajane? Mwanamme akifa napo rafiki zake hawaruhusiwi kumuoa mke wa rafiki yao aliyefariki? Au wanaruhusiwa? Kwa sababu gani?
Watu wengine wanaishi katika jamii ndogo ya vijiji ambavyo watu wote wanajuana na kila mtu ni rafiki wa kila mtu.
Na hawa nao utataka wakiachika wasiolewe au kuwa na mahusiano na kijiji kizima? Wahame kijiji kwa sababu wameachika?