Wanasiasa wataka kukampeni kilugha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa wataka kukampeni kilugha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BAK, Jun 6, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Na Exuper Kachenje
  05 June 2010


  [​IMG]
  Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)Rajabu Kiravu, akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja kati ya tume hiyo na viongozi wa vyama vya siasa Dar es Salaam jana. Kulia ni Makamu mwenyekiti wa Tume hiyo, Omar Makungu. Picha na Venance Nestory


  WANASIASA wa vyama mbalimbali nchini jana waliibua mjadala mzito kwenye mkutano wao na Tume ya Uchaguzi (Nec) walipotoa hoja nzito za kutaka waruhusiwe kutumia lugha za makabila yao wakati wa kampeni kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

  Mkutano huo, uliofanyika jijini Dar es salaam, ulikuwa wa kujadili rasimu ya maadili ya uchaguzi, lakini ukatawaliwa na hoja hizo za lugha ya kutumia kwenye kampeni.

  Mjadala huo mkali uliibuka katika baada ya mkurugenzi wa Nec, Rajab Kiravu kutoa mwongozo na kusoma mapendekezo na maoni yaliyotolewa na vyama hivyo pamoja na maoni ya Nec katika vipengere vya rasimu hiyo yenye kurasa 39.

  Kipengere cha 2.1 (k) cha rasimu hiyo kinasema: "Kiswahili itakuwa ndiyo lugha pekee katika kampeni za Uchaguzi, pale ambapo Kiswahili hakieleweki na itakapolazimu, mgombea atazungumza Kiswahili na mkalimani atatafsiri katika lugha inayoeleweka katika eneo husika."

  Kipengele hicho ndicho kilichoamsha hoja za wawakilishi hao wa vyama.

  CCM, ambayo haikutuma mwakilishi, iliandika katika mapendekezo yake kuwa "mgombea anaweza kuzungumza Kiswahili na, au lugha inayoeleweka sehemu hiyo".

  Lakini Chadema ilipingana na maoni hayo ikisema kuwa kutumia lugha ya sehemu hiyo ni ubaguzi wa lugha na au utamaduni, huku kikihoji sababu za Kiswahili kuwa lugha pekee kwenye kampeni.

  Nec ilieleza katika maoni yake kuwa Kiswahili ndiyo lugha ya taifa inayoeleweka kwa Watanzania wote na kwamba kutumia lugha za kienyeji kutabagua watu wengine kwa kuwa hazifahamiki kwa Watanzania wote.

  Ilieleza kuwa kuruhusu matumizi ya lugha hizo itakuwa ni kurudisha nyuma jitihada za serikali za kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania na kutaka kifungu hicho kibaki.

  Lakini wadau hao, wengi wakiwa viongozi wa ngazi za juu wa vyama vya siasa, walipinga kwa nguvu huku Chama cha Wakulima (AFP) pekee kikiunga mkono matumizi ya Kiswahili.

  "Hakuna ubaguzi katika kutumia lugha za makabila. Tusipotumia lugha za makabila ni sawa na kuukana Utanzania wetu ambao unaazia katika makabila yetu zaidi ya 120," alisema mwakilishi wa PPT Maendeleo.

  Naye Julius Mtatiro kutoka CUF alisema: "Matumizi ya lugha za makabila hayaathiri maisha, wala uchaguzi. Ni vema wananchi waendelee kuongea lugha zao za makabila, mbona kiingereza tunaongea hata bungeni."

  Tundu Lissu kutoka Chadema alisema: "Yapo maeneo watu hawawezi kuuliza swali kwa Kiswahili... sidhani kama ni dhambi ukienda wanapoongea Kinyaturu ukaongea Kinyaturu, haina maana kuongea Kiswahili wakati watu hawaelewi. Wananchi wapewe uhuru kutumia lugha zinazoeleweka maeneo yao."

  Aliongeza kuwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ibaki kama moja ya sharti kwa mgombea katika fomu za kuwania nafasi ya uongozi.

  Hata hivyo, mkurugenzi wa Nec alikumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa suala la lugha lilijadiliwa kwa kina kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005 kwa kuwa inawezekana mgombea mmoja akawa si wa asili ya eneo hilo na kwamba sheria haizuii mtu kugombea mahali ambapo si asili yake.

  Mkutano huo ulihudhuriwa na CUF, NLD, Chadema, TLP, NCCR, SAU, Tadea na AFP.
  NEC imepanga tarehe nyingine ya kukutana na wadau hao kukamilisha mjadala huo kabla ya kutoa rasimu ya pili ya maadili hayo ya uongozi.

  Mbali na mjadala wa lugha vyama vya siasa vilipinga kipengere cha 1.1.3 kinachoeleza wajibu wa kusaini maadili kikitaka kila chama cha siasa na kila mgombea kuwajibika kusaini maadili hayo na kwamba chama kitakachokataa kusaini maadili hayo na mgombea atakayefanya hivyo watakataliwa na kuondolewa kushiriki uchaguzi, wakisema kinakiuka katiba ya nchi.

  Ufunguzi wa mkutano huo uliofanywa na makamu mwenyekiti wa Nec, Jaji Omar Makungu aliyeeleza kuwa wamepokea maoni kutoka vyama vinane vya siasa huku TLP ikiwasilisha maoni hayo jana asubuhi.
   
 2. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sitaki kuamini kuwa 'wazalendo' wa siku hizi wamefikia hapa. Kesho utamkuta anayepigia mchepuo ujinga huu anajinasabisha na Mwalimu Nyerere. Mbaya zaidi ni kuona wenye kupaswa kusema na sauti ikasikika wamenyamaza kimya. Nasema hapana kwa siasa za ujanjaujanja kama hizi. hapana.hapana.hapana
   
 3. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yaani hata msomi mpambanaji huyu amefikia hapa. Ninaweza nikawaelewa hawa jamaa zangu wengi lakini inapofikia hata mtu kama Lissu anakumbatia ujanjaujanja kama huu mradi kurahisisha mradi wake kisiasa, kwa kweli inauma mno. Ama kweli siasa ni uwanja wa fisi. Kubaki muadilifu wa misingi ni sawa na.........

  omarilyas
   
 4. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tuwe wakweli wakuuu. Kama hatuyaelewi vizuri maeneo mengine ya hii nchi yetu ni bora kukaa kimya.

  Hivi sasa nipo katika mkoa mmoja kama mwezeshaji katika mafunzo fulani ya viongozi wa ngazi fulani si za juu. Washiriki wameniambia kiswahili changu kigumu hawana hakika kama wananielewa vizuri hivyo kila mara narudia maelezo yangu. Sasa hawa hawanielewi na ninaongea kiswahili chepesi kama ninachotumia hapa, huko kwa waombwa kura je?

  Tusifanye masihara! Je swala la msingi ni kuongea kiswahili na unaongea nao wasikuelewe? Au kutafuta lugha mnayoweza kuelewana? Na ikibidi mkalimani?
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sipata picha pale Thame kwa Mlala:

  VANDUU VANGU NIBIGIENI KURA NIVAJENJE MVONE IVUNDE HE ISANGA LA VAATHU!
   
 6. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Iliwezekanaje wakati wa kupigania uhuru na kujenga taifa linaloitwa Tanzania? Kama mnaona njia za mkato zimewanufaisha wenzetu wengine kama wakenya then tuendelee kujaribujaribu kucheza na misingi. Hivi Mwalimu alipotoka bara kuja Dar es salaam kiswahili hakikuwa kigumu kwake? Anegeweka mbele urahisi wa kufanikisha kazi yake sidhani kama tungeluwa na Tanzania ili tofauti na wengine kama ambayo tmekuwa nayo kwa muda mrefu kabla ya ujanjaujanja haukushika hatamu kama inayoelekea sasa.

  Njia za mkato ndiyo kichochoro cha maovu na uharibifu jamani...

  omarilyas

  Omarilyas
   
 7. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono matumizi ya lugha za asili kama tunavyounga mkono ngoma za kienyeji/asili. Ni sehemu ya utamaduni wetu. Utamaduni siyo ngoma tu.

  Unaweza ukatoa laana za aina zote kwa mtetezi wa lugha za asili, lakini ni kosa kubwa ktk Taifa kudhani kwamba tutakuza lugha ya Kiswahili kwa kuua lugha za asili. Ili iweje?

  Kampeni kama hizi nimekuwa nikizisikia huko China, Uturuki, nk. ambako lengo imekuwa ni kulazimisha kifo cha lugha za makabila wasiyoyapenda na yanayodhalaulika.

  Sipendi kudanganywa kwamba eti umoja wetu umetokana na lugha ya kiswahili. wapi na kwa jinsi gani? Au kwa sababu ilisemwa na baba wa Taifa? Nonsense!

  Tumeingia kwenye mtego kwamba eti Kiswahili ni lugha ya Taifa, wapi ilikoandikwa hivyo? Miaka ya 60 ilitangazwa kiswahili kuwa ni lugha ya kiofisi (Official language) na siyo lugha ya Taifa (National language).

  Wengi tuko tayari kuona Rais akitoa hotuba kwa kiingereza ikulu mbele ya wageni toka ulaya lakini hatutaki kusikia akihutubia kikwele bagamoyo!

  Tumejenga tabia ya kuchukia lugha zetu kiasi kwamba mtu anaishi Dar miaka 30 bila hata kujua salamu ya kizalamo lakini akiishi US kwa wiki chache anarudi akinadi slang yao!
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Tunahitaji kulitafakari kiasi jambo hili, kwangu mimi its not a good idea kuingia huku. Najaribu kufikiria kama kama mchaga atagombea usukumani atawezaje kutumia lugha hii? Hii inafaa zaidi kwa jiranii zetu but huko bongo tulivyochanganyikana sidhani kama itakuwa busara sana!
   
 9. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2010
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatalazimika kutumia Kisukuma, kimsingi kwa asilimia kubwa kampeni hufanyika na itaendelea kufanyika kwa Kiswahili.

  Lakini kwanini tumkataze mgombea kufanya kampeni kwa Kisukuma(kama anakijua) kwenye kijiji ambacho 100% ya wananchi wanaongea Kisukuma lakini kuna asilimia 5 hawajui Kiswahili kabisa na asilimia 15 hawajui kiswahili vizuri?

  Mie binafsi nakutana sana na tatizo hili ninapokwenda vijijini, watu wengi vijijini bado wanajua lugha za asili kuliko kiswahili na si vizuri tuwanyime haki ya kuwasikiliza wagombea wao pale inapowezekana.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Jun 6, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Omari,

  Naona hujaelewa kinachozungumzwa hapa..Hoja ni hii Kanuni za Maadili ya uchaguzi zilikuwa zinataka kwamba kampeni mwaka huu zifanywe kwa kiswahili nau kingereza tu.Inawezekana wewe hujatembea vijijini ambako wakati mwingine hakuna sababu ya kuzungumza kiswahili wakati kijiji kizima wanazumgumza lugha zao za asili mabazo ni rahisi kuzielewa,kama wewe ni mtumwa wa kabila laoko basi ni wewe lakini ni muhimu watu kuzngumza lugha zao.

  Ndugu yangu kwa wasomi wnegi siku hizi hatuwezi kuzumgumza kiswahili completely unapokuwa unazungumza sasa kwa hali hii kule kijijini unapokuwa unaomba kura halafu unaweka maneno ya kingereza amabpo wenzako hawakulewi inakuwa haileti maana kabisa.

  Kiuhalisia bora uzungumze kilugha hutachanganya na kingereza..lakini pili kwanini Kingereza ambayo sio lugha yetu iwe halali halafu lugha zetu zisiwe halali?

  Think deeply acha kuwa mtumwa....wewe unaelewa kwa ufasaha lugha hizi wenzako hawaelewi..Nenda vijijini ukajionee.
   
 11. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wanataka iwe kama kenya, ukiwa mtaani Nairobi, utakutana na watu wanaongea kikuyu tuuuu, wengine kikambaaaa, wengine kijaluo kila mtu kama apendavyo...kuna radio zinazoongea kikuyu tu, kuna redio za kijaluo au kikamba, kuna forum zingine kama hizi zingine ni za wajaluo tu, zingine za wakikuyu tu...ndo maana ilikuwa rahisi sana kuorganise kipindi kile yale mapigano, kwasababu walikuwa na mahali pa kukutania kama kabila na kuambizana nini cha kufanya na wapi...anaemaidi ukabila tz ni adui mkubwa...kiswahili kama lingua franca yetu tumepata heshima kubwa dunia nzima..kutocharaza kilugha mtaani kwetu tumepata heshima dunia nzima..
   
 12. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haya wewe uliyejikomboa. Mwenzio huko utumwani nilifundishwa kuwa ...don't break principles as they will break you...kupigia chepua lugha za kikabila ni muendelezo wa ulimbukeni wa demokrasia unaowalazimu wanasiasa wetu kujifaragua na new found civility in the name of oppurtunism...but sishangai mitazamo hiyo kutoka huko ambako siasa ni opportunities na sio responsibilities

  omarilyas
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280

  Miaka ya nyuma nilipata bahati ya kusafiri katika mikoa na wilaya mbali mbali za Tanzania na nyingi usafiri kwa kweli ulikuwa ni shida kubwa sana. Kitu ambacho nilijivunia katika safari zangu hizo niliweza kuwasiliana na wenyeji kwa kiswahili, nikisema wenyeji namaanisha wakazi ambao wengi wao hawakuwahi kupata bahati ya kutoka katika maeneo hayo waliokuwa wanaishi. Inawezekana kabisa lafudhi zetu (pamoja na office mates tuliokuwa nao) zilikuwa na tofauti lakini tulielewana bila matatizo yoyote yale. Na mara nyingi katika mazungumzo yetu tulisifia sana uamuzi wa Mwalimu wa kukifanya kiswahili kiwe lugha ya Taifa. Hili la kutumia kilugha katika kampeni mimi siliafiki hata kidogo hasa ukitilia maanani Watanzania wamejichanganya mno katika mikoa mbali mbali.
   
Loading...