Wanasiasa wanamwogopa mungu kweli?

Wanasiasa wanamwogopa mungu kweli?

Joined
Apr 21, 2011
Posts
7
Reaction score
1
Jamani nisaidieni kujua. Hawa wanasiasa wetu mara nyingi wanahubiri wasiyoyaamini
wenyewe na hawajali wanaowarepresent. Hivi kweli hawa watu wana dini na wanamwogo mungu?pa
 
Mkuu yepi wasioyaamini? Em jaribu kuwa wazi ili wachangagiaji wajue nn wachangie..
Mi nadhan hofu ya Mungu ya kweli haiko ndani yao.
 
Wanasiasa hawana shida na kwenda mbinguni/peponi, hata yule wa mlima wa moto anahadaa waumini wake! Kwenye siasa zetu hasa za kiafrika hakuna sincerity, zaidi ni kudanganya ili tu the end justifies the means! Wakimwogopa Mungu hawawezi kuendesha mashangingi!
 
Mi sifikiri kwamba wanasiasa wanamwogopa mungu, bali, kama mungu yupo, labda yeye ndiye anayewaogopa wanasiasa.

Kwa sababu uta explain vipi mijitu inakwiba mamilioni ya dola huku nchi zao masikini, watoto wadogo wanakufa ?

This just goes to show that "mungu" is a man made myth.
 
Hawawezi kumwogopa Mungu kwa sababu hata njia walizopatia hizo nafasi za kisiasa wengi wao ni kinyume na mapenzi ya Mungu. :A S 39:
 
jamani nisaidieni kujua. Hawa wanasiasa wetu mara nyingi wanahubiri wasiyoyaamini
wenyewe na hawajali wanaowarepresent. Hivi kweli hawa watu wana dini na wanamwogo mungu?pa

kwa namna wanavyopenda mali hujisahau na kufikiri mungu ni mali!!!!!!
 
Hawamuogopi Mungu na siku ya mwisho HAWAIOGOPI.
 
Wengi wao hawamwogopi Mungu. Wanatamani hata kumbinafsisha awe wa kwao peke yao!
 
Mi sifikiri kwamba wanasiasa wanamwogopa mungu, bali, kama mungu yupo, labda yeye ndiye anayewaogopa wanasiasa.

Kwa sababu uta explain vipi mijitu inakwiba mamilioni ya dola huku nchi zao masikini, watoto wadogo wanakufa ?

This just goes to show that "mungu" is a man made myth.

Wahasibu wana kanuni moja inaitwa "Conservatisim". Mtu ukikabiliwa na "options" mbili, moja inaweza kukuletea matukio mazuri, na nyingine mabaya kanuni hii inakutaka ufanye maamuzi "as if" kile kibaya ndicho kitakachokutokea.

Ushauri wa bure kwako na wenye mtazamo kama wako kuhusu Mungu: Bora ufanye maamuzi yako ukitegemea kuwa kuna Mungu halafu uje uone kuwa hayupo KULIKO kuamua hayuko halafu umkute.
 
Back
Top Bottom