Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
1. Kuna baadhi ya wanasiasa waliowahi kupanda chati sana kisiasa na baadaye kuporomoka kwa kupoteza umaarufu kwa kiasi kikubwa sana! Mfano wa wanasiasa hao ni Augustine Lyatonga Mrema. Huyu ni mpinzani ambaye aliwahi kupata kura nyingi zaidi kiasilimia kuliko wapinzani wote waliowahi kugombea kiti cha urais.
2. Mwanasiasa mwingine ambaye kuna kila dalili za kushuka kisiasa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Zuberi Kabwe. Kauli zake za hivi karibuni na vitendo vyake vinaashiria kushuka huko kisiasa. Sina haja ya kuzirejea kauli hizo, kama wachangiaji watahitaji tuzirejee nitafanya hivyo. Sina haja vile vile ya kuwataja wanasiasa wengine waliopanda na kushuka, wachangiaji mkihitaji nitawataja, nimetaja hawa wawili kama mfano tu.
3. Maswali yangu ni haya:
(a) Wanasiasa hawa ambao walituaminisha kwa kiasi kikubwa kwamba walijitoa kwa dhati kuwatetea watanzania halafu baadaye wakaonekana kuwa si lolote tunajifunza nini kwa jambo hilo?
(b) Tufanye nini ili tuchague viongozi ambao kweli hawatatetereka kwa namna yoyote ile hata kama itatumika nguvu ya dola kuwadhibiti kama ilivyofanyika kwa Mrema, labda na Zitto maana mpaka sasa hatujui yaliyomkumba?
(c) Tutawajuaje wapinzani "feki" ambao wamepandikizwa na Chama Tawala wakituminisha kwamba ni wapinzani kiukweli kumbe ni kiinimacho matokeo yake wanatupotezea muda wa kuwapigia kura na baadaye tunaanza kuvuna matunda mabaya ya kiutendaji na upandikizaji wa migogoro na migawanyiko isiyoisha inayosababishwa na wao? Hapa namlenga tena A. L. Mrema ambaye ametajwa mara kwa mara kuwa ni pandikizi la CCM.