We bwana unamatatizo makubwa kichwani,hyper tension of knowing and self centred.Huu ni ujuha wa watu waliokosa exposure!!!Kwa hyo unataka watu waitishe press conference ya kukufurahisha wew?Who are you?On my opinions,your simple literal terms are mostly void ,senseless and wild.This kind of reasoning is purely illogical and prematurely dramatic!!Ni Ombi langu tu Kwenu Wanasiasa wote nchini Tanzania kwamba muwe mnajitahidi pale mkiwa mnaitisha ' Press Conferences ' zenu kuzungumzia mambo fulani / jambo fulani muwe mnatuambia Watanzania vile Vitu ' vizito vizito ' na ' muhimu ' Kwetu na siyo kutuambia vile Vitu ambavyo wengine tumekuwa tukivisikia tokea tukiwa Shule za Msingi hadi leo.
Halafu na kama mnajijua kabisa kuwa huwa mnakuwa hamna jipya na la maana basi acheni kuwapotezea muda Watanzania kwa kuwapa hamu ya Kujua jambo geni Kwao halafu baadae wanakuja kuyasikia yale yale ambayo wameshayasikia na wameyazoea. Mnatukera na kutufanya sasa tuwaone ni kama vile mmeishiwa Kisiasa.
Kuna haja gani ya Wewe / Nyie Kuitisha ' Press Conference ' kisha unakuja Kutueleza Watanzania jambo lile lile ambalo pengine Mwanasiasa mwenzako ambaye nae alikuwa katika hiyo hiyo ' situation ' kama yako au hata alikuzidi kidogo nae alishawahi Kutuelezea? Na nyie Waandishi wa Habari muwe mnajiongeza kwani kama mkiwa mnawaona hawa Wanasiasa wa Kitanzania wanawaita halafu wanaenda Kuongea kile kile acheni kuwa mnatuhabarisha kwani mnatuchosha kama siyo mnatuboa.
Namalizia kwa Kusisitiza kuwa Wanasiasa wa Tanzania acheni kuwafanya Watanzania ni Mambumbumbu / Mbayuwayu na Kutaka Kujipatia ' Kiki ' kupitia mambo ambayo mnayapitia ambayo mengineyo yamewagharimu kutokana na ' Upuuzi ' wenu halafu baadae mnatafuta huruma. Watanzania wa leo tunataka Kusikia au Kuambiwa mambo yenye Tija na Mantiki halafu yawe mazito hasa na siyo Utoto Utoto na Kulialia tu.
Uzi wangu huu uende kwa Wanasiasa na Vyama vyao vyote vya Kisiasa ambavyo wanaviwakilsha.
Nawasilisha.