Wanasiasa na umasikini wa tanzania

Wanasiasa na umasikini wa tanzania

Luraja

Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
27
Reaction score
4
Nafuatilia mjadala wa posho ya wajumbe wa bunge la katiba.Inasikitisha sana kuona wajumbe ambao wengi wao ni wabunge na wasomi wetu wakiwa wanadai waongezewe posho.Wanajav kwa hesabu za haraka mjumbe mmoja atachukua milioni 21,000,000 kama bunge litadumu kwa siku 70.

Hivi hii ni haki? Kwa nchi ambayo bado wanafunzi wetu wanakaa chini,hawana vitabu hospitalini hakuna dawa.Hivi kweli mshahara wa mtu kwa siku 30 nyie wajumbe wetu mnasema ni kidogo kuwalipwa kwa siku moja.Kweli nimekubali kauli ya Zitto "Tusiwamini wanasiasa" watu wenye kupenda utajiri wa haraka.

Umasikini wa nchi umechangiwa wanasiasa na watu ambao hawana uzalendo, huruma, mafisadi wenye kupenda utajiri wa haraka.Wajumbe wa bunge la katiba mmepewa heshima kubwa na taifa kufanya kazi muhimu kwa mstabali wa taifa letu.
Mwisho ushauri wangu kwa mjumbe atakayeona posho ni kidogo harudi akaendelee kujenga taifa kwa kufanya kazi nyingine itakayo mpatia zaidi ya posho hiyo. Kwa maana wengi wenu ni wafanyabiashara na wasomi, hakuna mkulima anaweza kuiona 300000 ni kidogo.
 
Back
Top Bottom