MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Sitaki kutetea wataalamu hawa lakini acha tu niseme ukweli kwa sababu wao nao ni wanadamu wenye damu na mioyo kama wanadam wenge!
Kinachomtofautisha mwanadamu moja na mwingine ni mazingira na aina ya maisha yanayoishi mtu, Mtu kuitwa Daktari, nurse, Engineer, Mfamasia au mtaalamu yeyote yule haimaanishi kua yeye sio binadamu kama wengine bali ni mazingira ya maisha ya taaluma yake.
Madaktari na wauguzi wamekua ni watu wanaobebeshwa lawama kubwa na nyingi bila hata kuzingatia mazingira ya kazi zao, Naweza kusema ni watu wanaofanya kazi ngumu kuliko kazi zingine duniani baada ya watumishi wa Mungu. Chukulia mfano huyu mtu anakuta umepata ajali utumbo umemwagika nje lakini yeye anaurudisha ndani kisha anakushona vizuri na kukupatia dawa za kutumia upone ili urudi kazini, lakini huyu mtu unamuona hafai unampiga hadi makofi na kumwita mwizi, hafai! hii inaudhi sana na tabia hii ni ya kukemewa kwa nguvu zote.
Inashangaza sana kuona wanasiasa wakubwa wa level za juu nchini wanawapa kiburi Wananchi hadi kufikia kuwadhalilisha wataalamu hawa! Kama mtu Kafanya kosa ni kwanini asiripotiwe mahali husika? Kwanini makosa ya watu wachache wajumuishwe watu wote?
UUZAJI WA MADAWA YA MAHOSPITALINI.
Hiki kitu kipo lakini sio kama inavyochukuliwa na baadhi yetu katika umma, haiingii akilini daktari ambaye sio mtunza dawa kiutaratibu eti amuuzie mgonjwa Dawa, kwanza kazi ya kutunza Dawa sio ya Daktari ni ya mfamasia na ndio wanaotunza stoo za Dawa! Daktari kazi yake ni kutibu na kushauri tu sio kuuza wala kuhifadhi dawa ieleweke hivyo! Kama ni watu wa kwanza kilalamikiwa ilitakiwa wawe wafamasia japo nao wa haki zao kisheria! Sio kila mpira tu ni kwa wauguzi na Madaktari kwanini?
Ni mbaya sana kuona watu wasiojua wala kuelewa taratibu za taaluma hii wanalalama tu, Kama ni suala ukosekanaji wa dawa mamlaka husika zinaeleweka na sio kuwalaumu wataalamu hawa.
Haimaanishi uwepo wa dawa katika duka la Dawa karibu na hospitali ndio zimeibwa kwenye hospitali hiyo, kwani ni haramu daktari kumiliki duka la Dawa kama sehemu ya kujipatia kipato zaidi ya kimshahara chake kidogo anachopata? Maduka ya kuuza dawa za jumla yamejaa kila kona ya nchi kwanini mtu asiende kununua dawa zake za kuuza ajiingize kwenye riski ya kuuza dawa za hospitali?
Suala hili liko wazi, kuisha kwa Dawa hospitalini huenda ni kwa sababu ya wingi wa wagonjwa au bajeti kua ndogo kuliko mahitaji ya hospitali husika!Muda mwingine ni kuchelewa kufika kwa dawa kutoka bohari ya dawa iliyoko kanda husika! Hapa wataalamu wa afya tunawalaumu bure.
KUPIGWA KWA DAKTAKI HUKO MTWARA!
Hili tukio linadhihirisha kua Wananchi sasa wamevishwa kiburi na wanasiasa kupita kiasi, yaani mtu badala ya kushukuru kua mgonjwa wake amekua reffered kwenda National hospital kulingana na tatizo lake lakini badala yake anamshsmbulia daktari kwa kumpiga ati ni kwanini anamhamishia Muhihmbili? Is this sensible? Yaani RMO kimya, RC kimya, hakuna tamko lolote juu ya hili! Hii sio kudhalilishana ni nini?
Lazima ukweli tu usemwe tu kwamba udhalilishwaji na lawama kwa hawa watu muhimu sana duniani vimezidi sana.
Au tunataka nao waanze kuzidai haki zao? Maana mtu akianza kuzidai haki zake morali ya huisha kabisa ambapo sio vizuri katika utoaji huduma.