Wanasheria: Toeni ufafanuzi suala la ICSID

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhisi wa Migogoro ya Uwekezaji (International Centre for Settlement of Investment Disputes - ICSID) hivi karibuni imeamuru Serikali ya Jamhuri ya Tanzania kuilipa Standard Chartered Bank of Hong Kong $185 million (Tsh 426bn) kutokana na mgogoro ulioibuka baada ya $122 (Tsh 306 bn) kuchukuliwa kutoka Akaubti ya Escrow.

Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa msemaji wa serikali Dr. Abbasi akasema kwamba Watanzania tusiwe na wasiwasi kwa kuwa atakayelipa ni IPTL na si serikali (ya wanyonge). Hebu wanasheria, akiwemo KaShivji kadogo, watueleze na kuthibitisha kaliuli ya Dr. Abbasi.

Pia soma
 
Ufafanuzi ushatolewa wa kila aina na hao wanasheria au wewe Unamtaka mwanasheria gani atoe ufafanuzi?
 
Sijaona mwanasheria yeyote anatoa ufafanuzi kuhudu kauli ya Dr. Abbas. Ndo sababu nawataka wanasheria watoe ufafanuzi.
Sio anawapotezea watu anachotaka ufafanuzi toka kwa wanasheria maana hukumu inasema hivi,msemaji anasema vile
 
Sio anawapotezea watu anachotaka ufafanuzi toka kwa wanasheria maana hukumu inasema hivi,msemaji anasema vile
Kwani hatujui kusoma kingereza? Au soma gazeti la Mwananchi. Kila kitu kipo wazi kabisa.

Huyo msemaji kama ana hukumu yake angeiweka mezani tusome wenyewe. Haina tija kusikiliza porojo.
 
Back
Top Bottom