Wanasheria mko wapi kupinga suala la kodi mbili kwenye miamala?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,079
Reaction score
4,891
Hakika nilitarajiwa wanasheria wetu wangekuwa tayari wamefungua kesi mahakamani ya kupinga hii kodi mpya iliyotangazwa na serikali kwenye miamala. Wananchi tulio wengi hatuna ufahamu wa kusheria juu ya mambo ya kodi na ndio maana serikali ya ccm inatubambikizia kodi itakavyo ikijua hatuna cha kuifanya.

Tunawaona sana wanasheria wetu hebu fungueni kesi ya kupinga kodi hii wananchi tupo tayari kuwachangia gharama za kesi.Kodi hii ni maumivu kwa masikini na wanyonge walioipitisha kodi hii wanapokea mishahara minono na marupurupu mengi.

Wanakula kesi ya taifa.
 
Tulieni nyie, kuweni wazalendo. Hiyo sio kodi ni solidarity fund🤣🤸🐒
 
Utangulizi,

Nchi hii ina wenyewe, watu wanatumia koti la kodi ili kuongeza mapato katika biashara zao. Mfano, Waziri Mkuu ana shares katika kampuni ya vodacom, wala sio siri, na mstaafu ana share kwenye Halotel, pia sio siri. Na wengine wengi waliopo serikalini na bungeni wana shares nyingi tu kwenye mitandao ya simu. Sio siri pia.

Wananchi hebu nendeni kwenye masoko ya hisa mfuatilie wamiliki wa hisa katika makampuni ya simu muone wanene wanavomiliki hisa huko, ndio mtaelewa kwamba hii nchi ina wenyewe wanaolinda matumbo yao.

Na uzuri kwenye maswala ya umiliki wa hisa kwenye Dar Es Salaam Stock Exchange pamoja na Brella sio siri, mambo yapo wazi kabisa na wala sio yakificho.

Tunajazana ujinga na upumbavu kukaa kuaminishana serikali ipo kwaajili ya wanyonge sijui maswala ya Uzalendo (Solidarity). Hakuna kitu kama hicho. Hakuna.!!!

Swala La Mahakama,

Mahakama haiwezi kuingilia udhaifu wa sheria za nchi hii, kwasababu sheria zote zinazo husiana na Wizara zinawapa mamlaka Mawaziri kutunga "KANUNI (Sheria Ndogo)/MABADILIKO YA TOZO/MIENENDO YA WIZARA" na kuwaburuza masikini pale wanapojisikia.

Pili, kabla ya budget ya Wizara Ya Fedha kupitishwa bungeni, lazima ipitie kwenye baraza la mawaziri ili waipitishe. Kama kuna mabadiliko au kuongezwa kwa kodi/tozo n.k basi lazima budget hio ipitishwe na baraza la mawaziri. So that is to say, huu upumbavu ulipitishwa na Baraza La Mawaziri (Mawaziri Wote na wakiomgozwa na Waziri Mkuu) hata kabla haujapelekwa bungeni ili wabunge waipitishe hii budget ya Mwigulu Mchemba.

Tatu, Mahakama kazi yake kubwa ni "KUTAFSIRI SHERIA", sio kubadili sheria. Mtu akifanya kosa, na anapopelekwa kizimbani mahakama inakwenda kutafsiri sheria kutokana na ushahidi utakaopelekwa (Kwamba mshtakiwa kutokana na tafsiri ya sheria na ushahidi, ni kweli amevunja sheria au laaa).

Final,

Play By The Rules; The weak dont get to choose how they die, only the rich and powerful.

Endeleeni kuhuzunika/kulalamika/kupiga domo/kununa/wekeni gubu tuuuuu mpaka mpate majipu ya roho, ila hakuna kitu kitabadilika nchi hii. Mpaka wananchi akili ziwakae sawa na wajue umuhimu wa "KATIBA MPYA", ili kuwawekea "MIPAKA YA MADARAKA WATAWALA WETU" ili wasiwe wanajifanyia maamuzi wanavojisikia wao.
 
Jamani eeh tulieni nchi inafunguliwa ilikua kifungoni, muda si mrefu tutakua tunaokota Hela barabarani.
 
Kila nikiwaza ya nchi yangu machozi yanatiririka,waliomjengoni waliingia kwa mbeleko la mzee mwenyekwenda.Acha maisha yaende yakisimama tutakuwa ahera.
Hakika Nilitarajiwa WANASHERIA Wetu Wangekuwa Tayari Wamefungua KESI MAHAKAMANI ya KUPINGA Hii KODI MPYA iliyotangazwa na SERIKALI kwenye MIAMALA .WANANCHI tulio Wengi Hatuna Ufahamu wa KUSHERIA juu ya Mambo ya KODI na Ndio MAANA SERIKALI ya CCM inatubambikizia KODI ITAKAVYO ikijua HATUNA CHA KUIFANYA.
Tunawaona SANA WANASHERIA wetu Hebu FUNGUENI KESI ya KUPINGA KODI hii Wananchi Tupo TAYARI kuwachangia GHARAMA za KESI.KODI hii ni MAUMIVU kwa MASIKINI na WANYONGE Walioipitisha KODI HII wanapokea MISHAHARA MINONO na MARUPURUPU MENGI.
WANAKULA KESI YA TAIFA.
 
Utangulizi,

Nchi hii ina wenyewe, watu wanatumia koti la kodi ili kuongeza mapato katika biashara zao. Mfano, Waziri Mkuu ana shares katika kampuni ya vodacom, wala sio siri, na mstaafu ana share kwenye Halotel, pia sio siri. Na wengine wengi waliopo serikalini na bungeni wana shares nyingi tu kwenye mitandao ya simu. Sio siri pia.

Wananchi hebu nendeni kwenye masoko ya hisa mfuatilie wamiliki wa hisa katika makampuni ya simu muone wanene wanavomiliki hisa huko, ndio mtaelewa kwamba hii nchi ina wenyewe wanaolinda matumbo yao.

Na uzuri kwenye maswala ya umiliki wa hisa kwenye Dar Es Salaam Stock Exchange pamoja na Brella sio siri, mambo yapo wazi kabisa na wala sio yakificho.

Tunajazana ujinga na upumbavu kukaa kuaminishana serikali ipo kwaajili ya wanyonge. Hakuna kitu kama hicho.

Swala La Mahakama,

Mahakama haiwezi kuingilia udhaifu wa sheria za nchi hii, kwasababu sheria zote zinazo husiana na Wizara zinawapa mamlaka Mawaziri kutunga "KANUNI (Sheria Ndogo)/MABADILIKO YA TOZO/MIENENDO YA WIZARA".

Pili, kabla ya budget ya Wizara Ya Fedha kupitishwa bungeni, lazima ipitie kwenye baraza la mawaziri ili waipitishe. Kama kuna mabadiliko au kuongezwa kwa kodi/tozo n.k basi lazima budget hio ipitishwe na baraza la mawaziri. So that is to say, huu upumbavu ulipitishwa na Baraza La Mawaziri hata kabla haujapelekwa bungeni ili wabunge waipitishe hii budget ya Mwigulu Mchemba.

Mahakama kazi yake kubwa ni "KUTAFSIRI SHERIA", sio kubadili sheria. Mtu akifanya kosa, na anapopelekwa kizimbani mahakama inakwenda kutafsiri sheria kutokana na ushahidi utakaopelekwa (Kwamba mshtakiwa kutokana na tafsiri ya sheria na ushahidi, ni kweli amevunja sheria au laaa).

Final,

Play By The Rules; The weak dont get to choose how they die, only the rich and powerful.

Endeleeni kuhuzunika/kulalamika/kupiga domo/kununa/wekeni gubu tuuuuu mpaka mpate majipu ya roho, ila hakuna kitu kitabadilika nchi hii. Mpaka wananchi akili ziwakae sawa na wajue umuhimu wa "KATIBA MPYA".
Things are getting even worse and no one cares, we are very obidient citizents and they will take advantage of this stupid obidience to do whatever they want, ngoja sindano ituingie
 
Uko sahihi Asante kwa UFAFANUZI KATIBA MPYA NDIO KILA KITU
 
Things are getting even worse and no one cares, we are very obidient citizents and they will take advantage of this stupid obidience to do whatever they want, ngoja sindano ituingie
@Abrianna Leo nilitoa just 70,000/=Tsh kwa njia ya simu nikakatwa 4,700/=Tshs... Then nikatoa 30,000/=Tshs tena kwa njia ya simu nikakatwa 3,000/=Tshs.

Nikakumbuka juzi kati kipindi tupo chuo UDSM hio 7,700/=Tshs ilikua ndio ya chakula cha Asubuhi, Mchana na Jioni. Ila sasa hivi hio hela ndio makato ya kwenye simu tu, bado mtu hujala wala hujaweka mafuta ya usafiri.

Ukija kwa Mama Ntilie hio ndio faida yake kwa siku nzima kwa kuuza chai na chapati asubuhi na chakula cha mchana. Kazi ya siku nzima.

Ukija katika GDP Ya Tanzania, matumuzi ya mtanzania kwa siku ni chini ya USD 1. Ina maana hio 7,700/=Tshs kodi ya muda mchache ni matumizi ya chakula cha siku mbili kwa mtanzania.

Hii sio kusaidia masikini na kutokomeza umasikini katika taifa letu, hii ni kumkomoa masikini na kuongeza umasikini nchini. Hii ni kumfanya mtu wa hali ya chini hata akiugua maradhi akose hela za kwenda kufanya vipimo hospitalini, aishie kununua panadol tu zimvute siku moja au mbili za kuishi.

# Waziri Mwigulu hafai hata kuwa mwalimu wa shule ya msingi, huwezi ku complicate maisha ya watanzania kiasi hicho katika kipindi janga la Covid limeshika kasi. Kisa unatafuta sifa kwa watawala.
 
Zimwi likujualo halikuli likakwisha, walisema wahenga. Bora ya Mwendazake tulijua kabisa kuwa alidhamiria ubabe na ukatili. Tulikubaliana na ukweli, tukaufyata na maisha yakaendelea.
Maana japo alikuwa mbabe ila kuna aliyoyafanya tukayaona yenye tija. Sasa hili Zimwi jipya hatulijui ila inaelekea hili baya zaidi. Maana linatafuna mpaka mifupa huku likikuchekea.
 
@Abrianna Leo nilitoa just 70,000/=Tsh kwa njia ya simu nikakatwa 4,700/=Tshs... Then nikatoa 30,000/=Tshs tena kwa njia ya simu nikakatwa 3,000/=Tshs.

Nikakumbuka juzi kati kipindi tupo chuo UDSM hio 7,700/=Tshs ilikua ndio ya chakula cha Asubuhi, Mchana na Jioni. Ila sasa hivi hio hela ndio makato ya kwenye simu tu, bado mtu hujala wala hujaweka mafuta ya usafiri.

Ukija kwa Mama Ntilie hio ndio faida yake kwa siku nzima kwa kuuza chai na chapati asubuhi na chakula cha mchana. Kazi ya siku nzima.

Ukija katika GDP Ya Tanzania, matumuzi ya mtanzania kwa siku ni chini ya USD 1. Ina maana hio 7,700/=Tshs kodi ya muda mchache ni matumizi ya chakula cha siku mbili kwa mtanzania.

Hii sio kusaidia masikini na kutokomeza umasikini katika taifa letu, hii ni kumkomoa masikini na kuongeza umasikini nchini.

# Waziri Mwigulu hafai hata kuwa mwalimu wa shule ya msingi, huwezi ku complicate maisha ya watanzania kiasi hicho katika kipindi janga la Covid limeshika kasi. Kisa unatafuta sifa kwa watawala.
Mimi nimewaza nikajisemea kama kungekua na mbadala basi ningeachana na mambo ya mobile transaction kabisa n hata hivyo nitatumia tu in case of emergency, kwa sasa am out of it

Sijui hii idea ni ya nani lakini its a destruction to the majority especially sisi wananchi wa hali ya chini, na bado tumenyamaza kimyaa
 
Hakika nilitarajiwa wanasheria wetu wangekuwa tayari wamefungua kesi mahakamani ya kupinga hii kodi mpya iliyotangazwa na serikali kwenye miamala. Wananchi tulio wengi hatuna ufahamu wa kusheria juu ya mambo ya kodi na ndio maana serikali ya ccm inatubambikizia kodi itakavyo ikijua hatuna cha kuifanya.

Tunawaona sana wanasheria wetu hebu fungueni kesi ya kupinga kodi hii wananchi tupo tayari kuwachangia gharama za kesi.Kodi hii ni maumivu kwa masikini na wanyonge walioipitisha kodi hii wanapokea mishahara minono na marupurupu mengi.

Wanakula kesi ya taifa.
Kuna kitu inaitwa kwaajili ya "public interest" sera ya kuinua uchumi ulioporomoka hivyo mwananchi naye anahusika katika kurudisha uchumi ulioshuka kwa maslahi ya yeye mwenyewe mwananchi kurahisha kupata huduma za kijamii kama umeme ambao tuna ujenzi wa bwawa la Nyerere, pia katika kurahisisha usafiri katika ujenzi wa barabara za lami kuunganisha mikoa na wilaya nchi nzima pia ujenzi wa Reli ya kisasa tuna mradi wa SGR,pia uboreshaji wa huduma za afya ambapo Serikali imejenga vituo vya afya na zahanati nchi nzima na tayari imeshaajili watumishi wa afya siku za karibuni, maboresho katika elimu tukumbuke elimu inatolewa bure lakini lazima maboresho yafanyike zaidi kwa kuongeza vyumba vya madarasa na ukarabati wa shule kongwe ambazo miundombinu ilishachakaa kama Tabora boys na nyinginezo na kuzingatia elimu kwa watoto wa kike selikari inajenga shule za wasichana nchi zima lakini tusisahau selikari imeajili walimu na kusambazwa nchi nzima sasa katika yote hayo lazima nchi economically iwe imara hivyo sio mbaya mwananchi akahusishwa katika kuleta maendeleo kwa kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom