The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,915
- 19,125
Katika utafiti mpya uliofanyika katika chuo kikuu cha Oxford cha nchini Uingereza ukiongozwa na Prof. Konstantinos Monolopous unasema kua wanawake wenye makalio makubwa wana akili kuliko wenzao wenye makalio madogo(Flat Screen).
Utafiti huo unadai kua wanawake wenye makalio makubwa wana kiwango kidogo cha mafuta mwilini(Cholestrol) na mfumo wao wa homoni ni mzuri unaosaidia kuchakata sukari vizuri hivyo kusaidia kupunguza ugonjwa wa moyo na kisukari.
Utakumbuka pia hivi karibuni Chuo kikuu cha Pittsburgh na chuo kikuu cha California vya nchini Marekani walifanya utafiti unaodai kua wanawake wenye makalio makubwa huishi maisha marefu kuliko wanawake ambao hawana.
Utafiti huo uliongeza kua wanawake wenye makalio makubwa huzaa watoto wenye akili nyingi kuliko wenzao ambao hawana, hii ni kutokana na kiwango kikubwa cha mafuta kilichopo katika makalio ambayo husaidia katika makuzi na maendeleo ya ubongo wa mtoto akiwa angali tumboni.
Zaidi soma: http://elitedaily.com/news/world/big-butt-healthy-butt-study-says-women-big-butts-healthier/