Wanapojiremba kupita kiasi ina maana gani?

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,906
Siku hizi, kuna ugumu wakati
mwingine, kujua kama mtu ni
mwanamke au ni mwanaume. Vijana
na hata watu wazima wengi
wanaume hujipamba sana kwa
kutumia vipodozi, ambavyo kwa
kawaida, vimekuwa vikitumiwa na
wanawake.

Kuna wanaume wanaopaka nyuso
zao dawa za kung’arisha na
kupambana
kabisa na ndevu. Hawa ukiwatazama
nyuso zao ni kama za wanawake,
kwani mwanaume mwenye uso
mororo sana huonekana kama
mwanamke kwa kiasi cha kutosha.

Kuna wanaume wanaovaa hereni, bila
hata kujua wazivae kwa namna gani.

Uvaaji wa hereni kwa wanaume,
ambapo inasemekana ulianzia kule
Marekani, ulikuwa ukifanywa kwa
sababu maalum na kwa namna
maalum.

Kwa mfano kuna waliokuwa,
au wanaovaa ili kuonesha upendeleo
wao kimapenzi (kwa mfano ushoga)
na wengine kwa sababu mbalimbali.

Kwa kawaida mwanaume anapotoga
sikio moja tu, hasa la upande wa
kulia na kulivisha hereni,
inamaanisha kwamba, mwanaume
huyo ni shoga!

Kwabahati mbaya
hapa kwetu kuna vijana ambao
hutoga sikio moja la kulia na bado
wanaamini kwamba, wako salama.

Ukweli ni kwamba siku akikutana na
raia wa Marekani wanaotafuta
mashoga, hawatasita kumwita na
kumtongoza. Ndio maana yake, kwani
nyie mlidhani vipi?

Kwa kawaida wanaume wamekuwa
wakikataa kuvaa mapambo na
kujipodoa kama wanawake katika
kuonesha kwamba, mwili wao
hauhitaji vitu hivyo kwani ni mwili wa
kazi hususan za nguvu na hivyo
mapambo hayawezi kuwa na maana
kwao.

Ndio maana najiuliza kujipodoa na
kujipamba huku kwa wanaume na
kuvaa hereni na makorokoro mengine
yanaashiria jambo gani?
 
Back
Top Bottom