Wanaoshabikia serikali mbili hawaendi na wakati

Nambarione

Member
Joined
Sep 3, 2013
Posts
63
Reaction score
60
Wana JF nimesikia baadhi ya watu wakipinga pendekezo la Serikali 3 eti kwa maelezo kuwa itakuwa ni gharama, nk. Nampongeza Jgd Warioba kwa ufafanuzi alioutoa jana kuhusu suala la gharama. Ni ukweli usiopingika kuwa, Muungano wa Serikali 2 hautufai kwa mazingira ya sasa. Hebu mnikumbushe, ni lini Rais wetu wa JMT ameenda kufanya ziara ya kukagua shughuli za maendeleo kule Zanzibar kama anavyofanya Tanganyika huko Simiyu nk. Ukisikia Rais wa JMT yupo Zanzibar ni kwenye sherehe za Mapinduzi, nk. Sasa kwa mazingira hayo unamwita rais? Huwezi kujiita baba mwenye nyumba wakati siku zote upo kwa mke mkubwa, kule kwa mke mdogo unaenda tu unaishia nje ya nyumba na hauna lolote unalolifanya huko kama baba mwenye nyumba.

Jamani twende na wakati, Serikali 3 ni suluhisho la matatizo ya Muungano wetu, vinginevyo ni bora iwe Serikali moja au Muungano uvunjike.
 
Umenena vyema Nambarione. Mimi naona kelele zote hizi za Serikali 3 ni hofu tu ya baadhi ya wana CCM kupoteza kete zao. Mfano, EL amewekeza sana kwa ajili ya kuwa Rais wa JMT. Sasa unapoongeza Rais wa Tanganyika na Zanzibar, unamharibia hesabu zake kabisa. Hivyo, lazima atapambana sana na jeshi lake kupinga hilo. Nawaomba Watanzania, tunapotengeneza Katiba yetu, masuala binafsi tuyaweke kando. Katiba hii ni kwa ajili yetu na kizazi kijacho. Kama Biblia ingeandikwa leo, nadhani baadhi ya watu wangepambana sana ili amri za usiibe na usizini zisiwepo. Lakini kwa kuwa iliandikwa na watu wa Mungu wa zama zile ambao hawashabikii mambo yao binafsi, amri hizo zipo mpaka leo. Tuwe objective. Serikali 3 hazikwepeki kwa mazingira ya sasa.

Wana JF nimesikia baadhi
ya watu wakipinga pendekezo la Serikali 3 eti kwa maelezo kuwa itakuwa
ni gharama, nk. Nampongeza Jgd Warioba kwa ufafanuzi alioutoa jana
kuhusu suala la gharama. Ni ukweli usiopingika kuwa, Muungano wa
Serikali 2 hautufai kwa mazingira ya sasa. Hebu mnikumbushe, ni lini
Rais wetu wa JMT ameenda kufanya ziara ya kukagua shughuli za maendeleo
kule Zanzibar kama anavyofanya Tanganyika huko Simiyu nk. Ukisikia Rais
wa JMT yupo Zanzibar ni kwenye sherehe za Mapinduzi, nk. Sasa kwa
mazingira hayo unamwita rais? Huwezi kujiita baba mwenye nyumba wakati
siku zote upo kwa mke mkubwa, kule kwa mke mdogo unaenda tu unaishia nje
ya nyumba na hauna lolote unalolifanya huko kama baba mwenye nyumba.

Jamani twende na wakati, Serikali 3 ni suluhisho la matatizo ya Muungano
wetu, vinginevyo ni bora iwe Serikali moja au Muungano
uvunjike.

tukiacha porojo za kisiasa na uhafidhina,serikali tatu is the best practice.
 
Umenena vyema Nambarione. Mimi naona kelele zote hizi za Serikali 3 ni hofu tu ya baadhi ya wana CCM kupoteza kete zao. Mfano, EL amewekeza sana kwa ajili ya kuwa Rais wa JMT. Sasa unapoongeza Rais wa Tanganyika na Zanzibar, unamharibia hesabu zake kabisa. Hivyo, lazima atapambana sana na jeshi lake kupinga hilo. Nawaomba Watanzania, tunapotengeneza Katiba yetu, masuala binafsi tuyaweke kando. Katiba hii ni kwa ajili yetu na kizazi kijacho. Kama Biblia ingeandikwa leo, nadhani baadhi ya watu wangepambana sana ili amri za usiibe na usizini zisiwepo. Lakini kwa kuwa iliandikwa na watu wa Mungu wa zama zile ambao hawashabikii mambo yao binafsi, amri hizo zipo mpaka leo. Tuwe objective. Serikali 3 hazikwepeki kwa mazingira ya sasa.

Njaa kitu mbaya sana jamani. Wote wanaopinga Serikali tatu ni kwa ajili ya matumbo yao. Kwa nini tusiige wenzetu wa Kenya ambao walitengeneza Katiba yao kwa kuwasikiliza wananchi? Mimi nashangaa sana mwanasiasa anapoelezwa kuwa haya ni maoni ya wananchi, lakini yeye bado anatokeza kwa wananchi haohao kupinga. Hii jeuri ya pesa na madaraka ndio imetufikisha hapa. Nchi nyingine watawala wanaheshimu sana maoni ya wananchi, lakini sio hapa kwetu TZ. Nawaombeni wanasiasa badilikeni. Nchi hii ni yetu sote. Hivyo, siku zote formula ya wengi wape ndiyo inayotawala. Mimi nilitegemea michango yetu kuanzia sasa ingekuwa ni namna ya kufanya hizo Serikali tatu zifanye kazi vizuri na sio kujadili ziwepo au zisiwepo, maana hilo tayari limefanyika. Wanasiasa, hasa wa CCM heshimuni maoni ya wananchi.

Hakuna jambo jema kama Serikali 3 kwa ustawi wa Tanganyika na Zanzibar. Mimi nilifurahi sana kusikia Tanganyika yangu inarudi. Hao wanaopinga wana lao jambo. Haiwezekani uwe na muungano wa nchi 2 halafu upate serikali 2. Ni aidha utapata serikali 1 au 3 finish. Wanaopinga wajinyonge, sisi tunasonga mbele. Tumechoka kuwa nchi inayoendeshwa kwa remote ya watu wachache. Sasa tufike wakati wananchi wakiamua jambo lao hilo ndilo libakie, sio ujanja ujanja ambao mwisho wake umelenga kuwanufaisha wachache. enough is enough.

Back
Top Bottom