real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Maafisa wa uhamiaji nchini Tanzania wanawazuilia watu watano wanaoshukiwa kuwasafirisha wanawake kinyume na sheria kwenda nchini za Asia na Mashariki ya Kati.
Washukiwa hao wanatoka nchi za Saudi Arabia, Morocco, Kenya na wawili kutoka Tanzania.
Afisa mkuu wa uhamiaji John Msumule alisema kuwa washukiwa hao walikamatwa mjini wa Dar es Salaam.
Watu hao walikuwa safarini wakiandana na wasichana 12 kutoka nchini Burundi.
Bwana Msumule alitangaza kukamatwa watu hao kama hatua kubwa katika vita dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu nchini Tanzania.
Wiki iliyopita serikali ya Tanzania ilitangaza kuwa zaidi ya wanawake 500, wamekwama nchi za Asia na Mashariki ya kati baada ya kuhaidiwa ajira zisizokuwepo.
Chanzo:BBC