Wanaopinga uamsho wamepetoka - ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaopinga uamsho wamepetoka - ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malaria Sugu, Jun 21, 2012.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  SIKU mojabaada ya Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kutangazakukaribisha maoni yote kuhusu Muungano, yakiwemo ya kuuvunja, Waziri asiyekuwana Wizara Maalumu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mansour Yussuf Himidametangaza kuvutiwa na misimamo ya Jumuiya ya Mihadhara ya Uamsho kuhusuMuungano.
  Katikatamko hilo,ameweka wazi kuwa anapendezwa na misimamo hiyo aliyoiita yenye malengo yakutetea maslahi ya Wazanzibari katika Muungano na kutaka Wazanzibari waachiwewapumue bila kufafanua dhana hiyo ya kuachiwa wapumue.
  WaziriMansour ambaye ni Mwakilishi Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM, alitoa kauli hiyojana wakati akichangia Bajeti ya SMZ kwa mwaka wa fedha 2012-2013 katika Barazala Wawakilishi.
  Mbali nakuwa mwakilishi kwa tiketi ya CCM, ambayo imeweka wazi kuwa itatetea kuwepo kwamuundo wa Muungano wa serikali mbili, Mansour pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuuya Chama hicho na Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha ya Chama hicho, Zanzibar.
  Pamoja nakutofafanua dhana ya Wazanzibari waachiwe wapumue, Mansour alisema anakubalianana mikakati na misimamo ya jumuiya hiyo yenye malengo ya kuwepo kwa Muunganoutakaokuwa na maslahi kwa upande wa Zanzibar ingawa hakubaliani na vuruguzinazohamasishwa na viongozi hao.
  “Mimimsimamo wangu unafahamika wazi wazi katika Muungano...ni kuwepo Muungano wenyemaslahi kwa wananchi wa Zanzibar.Ingawa sio mfuasi wa Uamsho lakini nakubaliana na misimamo yao yenye malengo ya kuwepo kwa Muunganoutakaojali maslahi ya Wazanzibari na kutaka Wazanzibari tuachiwe tupumuwe,”alisema.
  Alisemawananchi wa Zanzibar wanataka Muungano, lakini kutokana na muundo wa Muunganouliopo sasa wamekuwa na mawazo mbalimbali kwamba umekuwa ukiwanyonya nakurudisha nyuma mipango ya maendeleo.
  Alitoamfano wa muundo uliopo sasa wa Muungano wa serikali mbili, ambao ndio msimamowa CCM, akasema wananchi mbali mbali wamekuwa hawaridhiki nao huku ukiwa haunatija kwa Wazanzibari.
  AonyaPolisi Aidha Mansour alionya vitendo vya Dola kutumia nguvu kwa watu wenyemawazo tofauti kuhusu Muungano ikiwemo wale wanaopinga Muungano na kutakauvunjike na kusema kufanya hivyo ni kwenda kinyume na demokrasia na uhuru wawananchi kutoa maoni yao na kujieleza.
  Alisemakinachotakiwa kufanywa ni kuwashawishi watu ambao hawataki Muungano kwakuwaelimisha na kuwatajia mazuri yatakayopatikana katika Muungano wa pandembili na athari zitakazopatikana kama Muungano utavunjika.
  “Naombavyombo vya Dola viache kutumia nguvu kwa watu wanaoukataaMuungano...tunachotakiwa kufanya ni kuwashawishi wale watu wanaokataa Muunganokwa kujenga hoja ya faida za Muungano na athari kama ukivunjika,” alisemaMansour.
  AwaliMansour aliwataka wananchi mbalimbali wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kutumianafasi yao ya demokrasia kutoa maoni kuhusu muundo wa Muungano wanaoona unafaakwa sasa wakati wa kutoa maoni kuhusu Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano.
  Alisemahiyo ndiyo fursa muhimu na pekee iliyopo sasa ambayo kama wananchi wataitumiavizuri, basi watatua matatizo mbalimbali yaliyomo katika Katiba ikiwemo mamboya Muungano.
  “Hii ndiyofursa muhimu na pekee iliyopo sasa kwa wananchi kutoa maoni yao kuhusu muundogani wa Muungano wanataka,” alisema.
  Mwakilishiwa Magomeni, Salmin Awadh (CCM), alisema wakati umefika kwa wananchi waZanzibar kutoa maoni yao kuhusu muundo wa Katiba ikiwemo muundo wa Muungano.
  “Wananchiwanatakiwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kuhusu muundo wa Muunganopamoja na marekebisho ya Katiba...hiyo ndiyo fursa pekee ya kikatiba iliyopokwa sasa,” alisema.
  Mjadala wakujadili Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012- 2013 umetawaliwa na mamboya Muungano huku wajumbe wakitaka kujua haki za Zanzibar zilizopo katikaMuungano.
  Muundo waMuungano umekuwa ukiamsha mjadala mkubwa ambapo kwa Zanzibar, CCM imekuwaikitetea msimamo wa kuwa na muundo wa serikali mbili; wakati CUF, ikisisitizamuundo wa serikali tatu.

  source: habarileo watu wanaodai huwezi kukopi


   
Loading...