beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,881
- 6,374
Serikali imepiga marufuku na kuwaonya watumishi wa Idara ya Wanyamapori wanaopiga risasi watu wanaowakamata wakifanya shughuli mbalimbali ikiwemo ujangili katika higadhi za taifa, kuacha na badala yake watumie sheria kukabiliana nao
Kadhalika, watumishi wa idara mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, wametakiwa kubadilika na kuachana na vitendo vya rushwa.
Agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, alipokutana na watumishi wa idara mbalimbali zilizo chini ya wizara hiyo katika Chuo cha Wanyamapori cha Pasiansi, jijini Mwanza.
Akizungumza na watumishi hao, Masanja alisema kuna malalamiko mengi katika baadhi ya hifadhi kwa maaskari kuwapiga risasi na kuwaua watu wanaowakuta ndani ya hifadhi na kuonya kuanzia sasa waache.
"Nimepata malalamiko mengi ya askari wetu wa wanyamapori kuwapiga risasi na kuwafanyia vitendo vibaya watu wanaowakuta ndani ya hifadhi, sasa vitendo hivi mviache,” alisema.
Chanzo: IPP Media