Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,047
- 3,980
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala, alisema wanaopata mimba shule kusoma elimu ya ufundi wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Huduma ya Kisaikolojia na Malezi kwa Watoto.
Mkutano huo unaoendelea jijini hapa kuhusu usawa kwa wasichana, wavulana na vijana, umeandaliwa na Shirika la Repssi na kuwashirikisha zaidi ya washiriki 400 kutoka nchi wanachama za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari wa nje ya nchi waliohoji hatua ya serikali kukataa wanafunzi wanaopata mimba kuendelea na masomo ya sekondari, Naibu Waziri Kigwangala, alisema watoto hao watapata elimu mbadala ya ufundi stadi.
Alisema uamuzi huo unatoa fursa kwa wasichana hao kuendelea na masomo wakati wakinyonyesha na pia kuendelea kuwapa maadili mazuri wanafunzi.
“Serikali haikumaanisha kuwafungia wazazi hao kupata elimu, watapata fursa nyingine ya kupata elimu ya ufundi stadi.
“Hatukusudii kuwatenga wanafunzi hao kutii kiu yao ya elimu, wamepewa fursa mbadala,” alisema.
Kauli ya Dk. Kigwangala imekuja baada ya Rais Dk. John Magufuli, kutamka hadharani kwamba wanafunzi watakaopata mimba hawataruhusiwa kuendelea na masomo katika shule za msingi au sekondari za umma.
CHANZO: Nipashe