Wanaobeza waambiwe kuwa ndege, madaraja na reli ya umeme ni miongoni mwa vipaumbele vyetu

jaruri

JF-Expert Member
Jul 16, 2014
717
459
Binadamu ni kiumbe Wa ajabu sana ,,hata ufanye jambo gani jema kamwe hawezi ridhika ,,hapa ndipo ninapo ukumbuka msemo Wa kizungu usemao I can't give you formula for success but that of failure that "if you want to fail try to please every one"
Ni kweli nchi ina mapungufu mengi katika sekta mbalimbali Elimu ,afya ,kilumo n.k
Hizi sector zinahitaji fedha na kamwe huwezi pata fedha bila kujenga mazingira rafiki ya biashara,kilimo na uwekezaji.

Tukianza na Usafiri Wa anga: Utalii ambao ni chanzo cha fedha za kigeni utaweza shamiri tu kama kutakuwepo na mazingira rafiki kama Usafiri Wa uhakika na vivutio vya utalii ,ndio maana serikali imewekeza Pesa nyingi katika sector hii ili tupate fedha zetu wenyewe na tupunguze utegemezi.

PILI;Usafiri Wa reli ya umeme utaleta faida zifuatazo
-Fursa za ajira
-Utalii
-Kuongezeka watumiaji Wa bandari ya DSM hivyo kuongeza kipato
-Kupunguza matumizi ya nishati ya mafuta
-Kupunguza uharibifu Wa Barbara zetu
Kwa uchache

Tatu,,madaraja ni muhimu kuunganisha maeneo yanayo tenganishwa na maji kama mito,bahari n.k hii ni kwa ajili ya kuwezesha accessibility ya watu toka eneo moja kwenda jingine.
Itapunguza Vifo vya:
-Wagonjwa wanaoshindwa kutoka remote areas kwenda hospital
-Wanao fia majini baada ya kujaribu kuvuka mito kutokana na ukosefu Wa madaraja
Madaraja pia yanawezesha Usafiri na hivyo kusaidia wakulima na wafanya biashara kusafirisha bidhaa mbalimbali na hivyo kuwainua kiuchumi

Kwa mtanzania mzalendo ataunga mkono juhudi za serikali katika kuwezesha haya Unapo shindwa kuona jitihada za serikali katika kuleta maendeleo na kubeza ninapata mashaka na uraia wako kweli we ni Mtanzania?

Long live JPM HAPA KAZI TU!!
 
Miundombinu na Viwanda bado ni njozi nzuri.
Ukisikiliza kila mtu, Ukienda kwenye kilimo watakwambia Rudi Elimu, Ukiridu elimu watakwambia Miundo mbinu ndio kila kitu.
 
25cd8e64c805fea566f287ef1e57a2b8.jpg
083c9fc2a5ed2eebc43d5995b82d1e5e.jpg
0b57edc9b4c7c3fb08ec43dc747a80f0.jpg
 
We ndo utoke ndani ya box,,development is multidimension to build a house you must have foundation na ndo anakifanya Rais wetu otherwise tutazidi kutegemea wahisani,,,Think out of the box and stop these issues of copy and paste ,,,you can do more than that
 
Kweli kabisa
 
Tunatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo,wapinzani wameishiwa pumzi wanapiga kelele.

Tuliahidi,tunatekeleza...CCM oyeeeeeeeeeeee.
 
Unajua upinzani 2020 wanaweza kukosa sera maana naona kila mkoa unazidi kutekwa na hiki chama kwa sasa Morogoro wamepatwa na CCM baada ya treni ya umeme
 
Yote nayaunga mkono lakini suala la ndege HAPANA!!! Unapokuwa na uhaba wa raslimali lazima ufahamu ni namna gani raslimali hizo chache zilizokuwepo unaweza kuzitumia vizuri!!

Hakuna mtalii hata mmoja aliyekuwa anashindwa kuja Tanzania kwa sababu tu hatukuwa na ndege

Hakuna mtu yeyote aliyekuwa anashindwa kwenda popote ndani ya Tanzania hii kwa sababu tu ATCL hawakuwa na ndege

Hakuna mwekezaji hata mmoja ambae alishindwa kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu tu hatukuwa na ndege

Mifano ipo mingi na yote hiyo inajibu jambo moja tu!!! Utumiaji wa shilingi trilioni moja na ushee kununua ndege ni uwekezaji usio na maana yoyote kwa nchi ambayo ina changamoto lukuki za msingi!!

Hata kama ni muhimu kwa ATCL kuwa na ndege zake lakini kwa sasa haikuwa lazima hasa ukizingatia ukweli kwamba, wakati hakuna chochote ambacho kilishindikana kufanyika kwa sababu tu hatukuwa na ndege; kinyume chake hadi leo kuna mambo kadha wa kadhaa hayaendi sawa kwa sababu tu changamoto zake hazijatatuliwa!!!
 
Hii ndo Tanzania Mpya tunayoitaka lazima baadhi ya watu waumie ili tufike tunakoenda
Baadhi ya watu ndio wanaoumia?!!! Mlalahoi ndio kiama chake unga tu shida, hospital hakuna dawa hiyo elimu bure nako shida tupu!! Waliaminishwa kuwa utumbuaji majipu ungewepa unafuu wa maisha kumbe ndio kifo kabisa!! Daraja na afya na maji kipi kipaumbele?!
 
We ndo utoke ndani ya box,,development is multidimension to build a house you must have foundation na ndo anakifanya Rais wetu otherwise tutazidi kutegemea wahisani,,,Think out of the box and stop these issues of copy and paste ,,,you can do more than that
Umaposema rais wetu una maanisha nini wewe gamba?? ivi ile reli na ule mradi uliofunguliwa pale dsm haukua kwa misaada ya wahisani???
 
Tawala za kidhalimu hujidhihirisha tu, yani mnakumbuka umuhimu wa miundombinu leo!? SHAME ON YOU.
Ukizungumza hoja kama hizi za mtoa mada kwenye midahalo mikubwa utaishiwa kuzomewa tu na watu wenye hasira kali ni bahati nzuri sana Tanzania hakunaga midahalo muhimu ya kitaifa au hotuba za viongozi na maswali ya uso kwa uso wangekimbia na suti zao.

Elimu na afya, hivi ni muhimu sana msijitoe tu ufahamu ukimpa mtu elimu bora atajiajiri na kueza kujitafutia kipato halali, ataeza kulipa kodi stahiki, hiyo kodi itatumika kujenga hiyo miundombinu bora na imara.
Afya napo ni hivyohivyo angalia India wameweza sababu waliwekeza kwanza kwa elimu hata afya inakuja vizuri automatically na sasa mnakimbilia kutibiwa huko.
Ukiwekeza kwenye elimu na afya vingine vyote vinakuwa rahisi.

Sasa elimu duni afya duni mnafikiria kujenga viwanda! Serious? Sifikirii kama mko timamu jamani mtakuwa na mental problems tu.
Viwanda gani hivyo kabla ya kuandaa man power ambayo inatakiwa iwe very skilled? Hivi mnatumia akili kweli?
Au mwafikiri hiyo skilled labour itatoka Jupiter siyo, heheheee vituko haviishi huko Tanzania.
 
Kwa hili la reli tutamkumbuka sana hasa sisi wa mikoa Ya uchumi wa reli mengine aakimaliza aandike THE END maana naona usaniiii tu
 
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia serikali kati ya bajeti ya 29 trillion inadaiwa 6.5 trillion na makandarasi na wazabuni wengine
Ukijenga miundo mbinu bila kujali sekta nyingine ni sawa kutibu donda kidoleni huku moyo unasimama
Pure tripe
 
Yote nayaunga mkono lakini suala la ndege HAPANA!!! Unapokuwa na uhaba wa raslimali lazima ufahamu ni namna gani raslimali hizo chache zilizokuwepo unaweza kuzitumia vizuri!!

Hakuna mtalii hata mmoja aliyekuwa anashindwa kuja Tanzania kwa sababu tu hatukuwa na ndege

Hakuna mtu yeyote aliyekuwa anashindwa kwenda popote ndani ya Tanzania hii kwa sababu tu ATCL hawakuwa na ndege

Hakuna mwekezaji hata mmoja ambae alishindwa kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu tu hatukuwa na ndege

Mifano ipo mingi na yote hiyo inajibu jambo moja tu!!! Utumiaji wa shilingi trilioni moja na ushee kununua ndege ni uwekezaji usio na maana yoyote kwa nchi ambayo ina changamoto lukuki za msingi!!

Hata kama ni muhimu kwa ATCL kuwa na ndege zake lakini kwa sasa haikuwa lazima hasa ukizingatia ukweli kwamba, wakati hakuna chochote ambacho kilishindikana kufanyika kwa sababu tu hatukuwa na ndege; kinyume chake hadi leo kuna mambo kadha wa kadhaa hayaendi sawa kwa sababu tu changamoto zake hazijatatuliwa!!!
Think big by Hen Carson inakuhusu
 
Think big by Ben Carson
Tulikuwa na idea kama zako ndo maana tuko hapa tulipo ,,you really need to change your way of thinking!!
 
Binadamu ni kiumbe Wa ajabu sana ,,hata ufanye jambo gani jema kamwe hawezi ridhika ,,hapa ndipo ninapo ukumbuka msemo Wa kizungu usemao I can't give you formula for success but that of failure that "if you want to fail try to please every one"
Ni kweli nchi ina mapungufu mengi katika sekta mbalimbali Elimu ,afya ,kilumo n.k
Hizi sector zinahitaji fedha na kamwe huwezi pata fedha bila kujenga mazingira rafiki ya biashara,kilimo na uwekezaji.

Tukianza na Usafiri Wa anga: Utalii ambao ni chanzo cha fedha za kigeni utaweza shamiri tu kama kutakuwepo na mazingira rafiki kama Usafiri Wa uhakika na vivutio vya utalii ,ndio maana serikali imewekeza Pesa nyingi katika sector hii ili tupate fedha zetu wenyewe na tupunguze utegemezi.

PILI;Usafiri Wa reli ya umeme utaleta faida zifuatazo
-Fursa za ajira
-Utalii
-Kuongezeka watumiaji Wa bandari ya DSM hivyo kuongeza kipato
-Kupunguza matumizi ya nishati ya mafuta
-Kupunguza uharibifu Wa Barbara zetu
Kwa uchache

Tatu,,madaraja ni muhimu kuunganisha maeneo yanayo tenganishwa na maji kama mito,bahari n.k hii ni kwa ajili ya kuwezesha accessibility ya watu toka eneo moja kwenda jingine.
Itapunguza Vifo vya:
-Wagonjwa wanaoshindwa kutoka remote areas kwenda hospital
-Wanao fia majini baada ya kujaribu kuvuka mito kutokana na ukosefu Wa madaraja
Madaraja pia yanawezesha Usafiri na hivyo kusaidia wakulima na wafanya biashara kusafirisha bidhaa mbalimbali na hivyo kuwainua kiuchumi

Kwa mtanzania mzalendo ataunga mkono juhudi za serikali katika kuwezesha haya Unapo shindwa kuona jitihada za serikali katika kuleta maendeleo na kubeza ninapata mashaka na uraia wako kweli we ni Mtanzania?

Long live JPM HAPA KAZI TU!!
Umesahau kuweka namba yako ya simu ili upewe ukatibu tarafa
 
Back
Top Bottom