Wanaobeba vifurushi mgongoni huku wakiomba barabarani huwa wanabeba nini?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,579
44,826
Katikati mwa miji nakutana na wabibi wengine wanakuwa ombaomba wamefunga mizigo mgongoni ni kama vipande vya nguo kwenye kanga unakuta anatembea nao huo mzigo mchana kutwa, ile inakuwa ni kitu gani? Mbona kama ni mambo ya kishirikina wanakuwa nayo?

Mimi naogopa sana kumsaidia bibi wa namna hiyo na kuna wale wengine watoto wenye ulemavu wa akili unawakuta stand au sokoni wanaomba mpaka unajiuliza huyu anatumiaje hela, ananunua kitu gani?

Maana kwa hali aliyonayo hata msaada wa chakula atapewa bure na mama ntilie wale itakuwa wanatumwa na watu wakubwa, wamegeuzwa kama misukule.
 
Kuna mbibi alivaa ushungi wiki jana aliniomba maji niliyokuwa nakunywa kwenye chupa nikashangaa ila ikabidi nimpe, akauliza ninywe kidogo au nichukue yote nikasema chukua.
Nikasogea mbele nikashtuka, logic ya mtu kuniomba maji niliyokuwa nakunywa. Na mauzo siku mbili zilizofuata yalikuwa mabaya sana nikaona coincidence tu.

Ningefikiria vizuri ningempa hela akanunue mwenyewe
 
Pole sana mkuu
 
Yaani Hadi naogopa 😰😰.. sometimes hua najiuliza hivi Hawa hawana watoto maana sidhani kama Kuna mtu anapenda kumwona mzazi wake akiwa ombaomba
Wengine unakuta watoto wamewapuuzia wazazi na wengine unakuta watoto na wao hawana mwelekeo wowote.
 
Back
Top Bottom