Wanandoa Wenye Furaha Katika Ndoa

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,972
Reaction score
22,933
Wanandoa wenye furaha katika ndoa yao ni watu wanaoishi kwa ukaribu sana. Hapa sizungumzii kuhusu wale wa 'piga makalio kisha tufanye ngono.' Bali namaanisha wale wa kugusana kimwili mara kwa mara - kupigana mabusu shavuni, kugusana kidogo begani na kupeana raha zote pasipo masharti.

Wanandoa wenye furaha hupongezana kila siku. Hupeana mahaba kwa kutamkiana maneno rahisi kama vile.... "Wewe ni mtamu sana," au "Unaonekana mzuri," au "Chakula cha jioni kilikuwa kitamu sana" kiukweli , hufanya tofauti kubwa katika ndoa kwa kufurahishana wakati wote.

Wanandoa wenye furaha huombana msamaha wanapokosea. Wanaendelea kusameheana. Na wanaonyesha shukrani. Wanathaminiana. Hawachukuliani kawaida.

Wanandoa wenye furaha hupanga bajeti ya mapato yao pamoja. Wanandoa salama hawana siri za pesa kati yao. Na hawaruhusu mtu wa tatu wakiwemo wakwe zao kuingilia ndoa yao ili kuwagawanya.

Wanandoa wenye furaha hutumia wakati wa mapumziko pamoja. Wanatoana out kupata vinywaji ama chakula pamoja. Pia wanaruhusu wenzi wao kukaa na marafiki zao. Mtu aliye salama hamtengi mwenza wake kutoka kwa jamii.

Jitahidi uwe wanandoa mwenye furaha.

Ubarikiwe.
 
Ujumbe mzuri ila so sad tunaishi jamii ya hovyo ambayo watu wanaingia kwenye mahusiano kwa lengo la kupata mahitaji yao binafsi na si kushirikiana ili kufika mbali kimaisha.

Wanawake wanaingia katika mahusiano wakiwa na akili zilizojawa hofu ya kutendwa, kudhurumiwa, kuachwa, kutelekezwa na kudumazwa na wanaume kifikra, kiuchumi, na kijamii, hali inayowafanya wanaume washindwe kujitoa kwa hawa wanawake maana ni ngumu sana kumuamini mtu ambaye hana imani na wewe.

Ukichunguza chanzo utagundua ni wanawake ndio walianzisha huu mvurugano sababu ya kuingia katika mahusiano na fikra potofu ambazo wametoka nazo huko kwa mama zao na shangazi zao waliowajaza hofu kutokana na maisha waliyopitia.

Ni kawaida sana kukutana na kabinti ka miaka 17 wakati wa kumtongoza akakwambia mmmmmmhmn mimi wanaume siwaamini hata kidogo wanafanya hivi na hivi na hivi. Ukijiuliza binti wa miaka 17 wanaume amewajulia wapi unabakia kustaajabu tu.

Huwezi kutana na kijana umri wa balehe na kukua mfano miaka 18 kuendelea awe na hofu ya mwanamke wengi muda huo hakuna wanalohofia wala kuwaza vibaya juu ya mwanamke sababu huwa wanamtazamia kama ni kiumbe mtamu kuwa nae karibu, hujisikia mahaba kumzoea, wanatamani kuwamiliki na wasijihusishe na yeyote yule nje yao, wanawivu nao, wapo tayari kuwapa chochote mradi wafurahi. Ila ni michezo ya akili, mapozi, tamaa za kupewa vitu visivyo vya ulazima, chuki za kurithishwa na mama zao ndivyo vitu baadhi kwa kutaja huwa vinaanza kuwaharibu akili hawa watoto wa kiume na kumuona mwanamke ni tatizo katika maisha yao.

Tuwarekebishe.
 
Pundamilia ni mzuri na mrembo kuliko punda wa nyumbani , ila jiulize kwa nini binadamu haishi na punda milia ana ishi na punda wa kawaida nyumbani, kamwacha milia msituni anateseka na simba huko akitaka kumwona anaenda tu kama mtalii na kumwacha huko huko na hekaheka za wanyama wakali.
 
Kwaiyo unataka kusema nn labda!?
 

[emoji419]
 
Ma Singo Wanaishi Kwa Shida Sana..!

Upweke....

Hawana moments Za Pamoja Za Furaha...!

Mara nyingi huishia Kuwa Singo Maza/Faza..!

Huanzisha Familia ambazo Sio Stable.!
 
akakwambia mmmmmmhmn mimi wanaume siwaamini hata kidogo wanafanya hivi na hivi na hivi. Ukijiuliza binti wa miaka 17 wanaume amewajulia wapi unabakia kustaajabu tu.
Ukikutana na kabint kenye mawazo ya hivyo fahamu tu kuwa kamelelewa na single mom, ila ukikomaa nacho unaweza kukibadilisha kikawa mke mwema.
 
Baada kujiridhisha kuwa inawezekana kabisa kumfuga Pundamilia na akafanyishwa kazi kama punda Donkey, bado kuna sababu kama mbili hivi zinapelekea asifugike. Sababu hizo ni zifuatazo;

Utalii.
Wanasema kwa kuruhusu afugwe majumbani itapunguza thamani yake na hivyo kuathili utalii .

Tabia
Wataalamu wanasema kitabia, Zebra ni kama walivyo wanyama wa porini, ni unpredictable na wepesi ku panic. Hiki kinawafanya wawe hatari, maana wakishapanic huwa ni wepesi to attack and Kill or kujeruhi vibaya.
 
We unazungumzia sinema.sio ndoa.
 
Umeongea kwa uchungu sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…