Wanandoa mlioko makazini talaka yaja

Wanandoa mlioko makazini talaka yaja

The only

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
11,201
Reaction score
14,777
Binadamu wakikaa eneo moja huwa wanakuwa kama watoto unakuta kijana wa miaka 27 fresh from chuo kaajiriwa anarafiki yake ana miaka 56 wale BBC ambaye ni umri wa babake lakini wanapiga story za udukuzi wanawake na za kijinga nyingi hii ni natural hutokea.

Lakini lililonifungulisha uzi si kushangaa hili bali kutahadhalisha Kutokana na kisanga hiki, tujage mwananawane:

Mke alimuarifu mumewe mwenye hulka ya kumpitia kazini kwamba jioni watakuwa na kasuprise ka birthday ya bosi wao na kumuaga mtumishi mwenzao, hivyo jamaa Adelay kama saa na kiduchu anywe mbili tatu mahali ndo ampitie, baada kama ya saa 2 toka muda wa kawaida wa kumchukua jamaa akatimba ofisini kweli alisikia kelele ukumbi wa nyuma, mlinzi anamjua akamkaribisha kwa bashasha na kumuelekeza apitaje kufika alipokaribia akabidi achungulie dirishani apate mtu wa kumwitia chombo yake, lahaula la kwata shaabash akashuhudia live mkewe akiwa anayarudi singeli akipigiwa makofi akicheza kawimbo...eeeh kamatia chini kwa chini mwendo wa mateka eehhh..

Jamaa akakodoa zaidi akashuhudia njemba ikichezea shanga, mkewe kainama kagusa chini kiuno ka feni. Jamaa kimsingi mstaarabu sana akamwita dada mmoja akamwambia niitie mamsapu hakuonesha kupanic ila uso ulikuwa wa rangi ya samawiti isiyovutia na macho kodo kama kameza gunzi la mahindi akamchukua mkewe wakaelekea kugari, mkewe alikuwa akitetemeka mithili ya nguchilo wa kolomije, wambea hatukujua kilichojiri maana jamaa hakutaka washambenga tuwe na chakusimulia wakasepa, kesho yule dada alipiga simu ya kuomba annual leave anafamily issue za kusolve.

Ok turudi kwenye yanayotuhusu maana mlivyotumbua macho wabongo kwa kupenda mabalaa, jamani ni vyema sasa tukatambua mahusiano yetu na watumishi wenzetu lazima yawe yenye limit jichunguze ushiriki wako makundi ya whatsup humo wake zetu wana wapenzi wa utani, wanawaita watu baby of which is not necessary adui yako kwenye kundi anaweza likisha ukaomba annual leave, kimsingi marafiki wa ndoa ni mke na mume, waliobaki ni maadui kila unapoongea nao ongea kama uko interview.

Kalamu wino umekwisha, si budi kuahirisha.

Alamsiki
 
Hawa bila kufungwa kamba mguuni lazima rangi iwe ya samawati

Psalm 133:1[emoji768] "Behold, how good and how pleasant it is for brethren to dwell together in unity."
 
Mungu niepushie invident kama hiyo na mamsapu....naweza nikaenda jela kama atapata nguvu za kwenda central baada ya wiki nzima ya kua hoi muhimbili.
 
ofcoz humu makazini huwa kunakuwa kama shule jinsi mnavyoishi, vijana na wazee wote mnakuwa hamna tofauti, ila kutaniana hiyo haiepukiki hata hizo za kuitana mpenzi sijui mama watoto zipo sana tu, ila cha msingi ni kujiheshim na kujiwekea mipaka, hiyo uliyoleta sijui kam ani stori au kitu cha kweli lakini huyo mwanamke anaonekana hana limit na hajiheshim huwezi kucheza hivyo tena kwenye party ya ofisi ukizingatia na wakubwa wako wa kazi wanakuwa hapo mbaya unaachia mfanyakazi mwenzio wa kiume aanze hadi kukushika shika hivyo duh, labda tuseme ni pombe mana nimeshawaona hata hapa kweltu kwenye party wakilewa wanacheza mziki balaa lakini sio kwa kujidhalilisha hivyo
 
Back
Top Bottom