Wananchi waombwa kununua chakula cha msaada

Wananchi waombwa kununua chakula cha msaada

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322


SERIKALI imewaomba wananchi kununua chakula cha msaada kilichotolewa na Hifadhi ya Taifa ya chakula (NFRA) licha ya kucheleweshwa na kukutana na msimu wa mavuno.


mahindi.jpg


Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Babati, Hamisi Malinga, wakati akizungumza na Nipashe katika ghala la kuhifadhia mazao la halmashauri hiyo.


Alisema ni vizuri wananchi waichangamkie fursa hiyo ya chakula kwa kukinunua na kukihifadhi ili kiwasaidie katika kipindi kigumu cha upungufu wa chakula.


“Changamoto tunayoipata zipo baadhi ya kata zinasema haziwezi kuchukua hiki chakula kwa kuwa bei elekezi iko juu zaidi ya bei ya kawaida iliyoko mitaani ya mazao yaliyoanza kuvunwa,’’ alisema Malinga.


Aidha, alisema bei elekezi kwa kilo moja ni Sh. 650 na mpaka sasa zimekwishachukuliwa tani 42 na amewaomba wananchi kuendelea kununua chakula hicho ili kije kiwasaidie wakati mwingine.


Malinga aliwaonya wafanyabiashara watakaonunua chakula hicho kwa kutokukipeleka nje ya nchi maana ni kwa ajili ya wananchi na amewataka kutanguliza uzalendo kwanza hata kama wanahitaji faida.


“Sisi kama viongozi hamna kitu kinakera sana kama kuwaongoza watu ambao wana njaa maana hawataweza kukusikiliza kwa chochote utakachowaambia,’’ alisisitiza.


Aliwataka kununua chakula hicho kwa kuwa mavuno ya msimu wa sasa siyo mazuri na kwa kipindi cha miezi miwili bei zitakuwa juu hivyo wasikipuuze eti kwa kuwa wameanza kuvuna na wakajiona kilichopo kinawatosha.


Aliongeza kuwa kwa wale wananchi wanaoishi kata za Nkaiti na Mwada wenye mifugo mingi kujenga tabia ya kuuza mifugo yao na kununua chakula na kukiweka ndani ili kiwasaidie kuepukana na shida ya njaa.


“Nia ya serikali ni kuleta maendeleo kwa wananchi wetu ila kama watu wana njaa hawawezi kukusikiliza na kama mtu hana pa kuhifadhi mazao aje ajiandikishe ahifadhi chakula chake hapa,’’ alisisitiza.


Chanzo: Nipashe
 
Badilidha heading, NFRA huwa haitoi chakula cha msaada bali yenyewe huuza chakula kwa ajili ya kuimarisha bei ya soko isipande juu sana. Taaisis Inayotoa chakula cha msaada ni Idara ya Uratibu wa Maafa ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na mara nyingi hutoa kwa extreme drougt cases only.
Pia sidhani kama wameombwa kununua bali wanakumbushwa kuwa hiyo ni fursa adimu kwakuwa chakula hicho huwa kinauzwa chini ya bei ya soko na hivyo kuwalazimisha wafanyabiashara nao washushe bei zao na kupelekea unafuu wa bei ya chakula kwa wananchi kwa ujumla. Kinachofanyika ni intervention ya kawaida na imekuwa ikifanyika kwa miaka mingi sana.
 
Back
Top Bottom