...JK alidhani Urais wa Nchi ni sawa na kula wali kwa kachumbali kwenye sahani ya fedha! Urais ni kazi-dume; inahitaji wanaume wa shoka wenye mboni za kuona mbele zaidi ya wanavyoona wananchi wa kawaida. Urais si chetezo na ubani pekee kilichojazwa uvumba, manemane, ambari, mvuje na kashkash baruani...ni kazi ya kuonyesha njia yenye saada kiuchumi, kijamii na kisiasa.
JK amefeli tena amefeli mtihani uliyotungwa na Dr. Ndalichako (Mkurugenzi wa NECTA); kwa mshangao, mtihani uliyotungwa na Dr. Slaa (Operesheni Sangara) na Prof. Lipumba (Operesheni Zinduka) atatoka kweli? Sidhani! Mwacheni alie...kama walivyoimba MSONDO NGOMA, "ukimuona mtu-mzima analia ujue ana jambo". Amefilisika kisiasa, hana jipya...tusubiri maumivu makali ya msoto wa maisha ya kubangaiza kiuchumi, kisiasa na kijamii.