Nina imani na nafsi yangu inaniambia kuwa wakazi wa Dar wanabomolewa makazi yako kwa kuwa hawakuchagua CCM. Hii ni kisasi cha serikali kwao kwa visingizio vya mabondeni, mara mipango miji nk. Ukiangalia wabunge wote kasoro Ilala, kigamboni na Ukonga ni Upinzani. Kwani kama watu walikuwa wanajenga na wanaonekana na serikali za mitaa zilikuwepo waliachwa??mbona hata hiyo ishu ya karibu na fukwe nchi nyingine kama Uholanzi wanajenga hadi ndani ya maji kuongeza ardhi??nchi yetu imejaa vilaza wanaokaa mezani tu na kutengeneza mipango miji ya mezani ili kuonea wananchi. Hawajui wanachofanya ni kuvaa masuti tu na kukuza vitambi vya rushwa. Kuna wakati serikali haikuwa na pesa za kupima naeneo na walitegemea wananchi wawasubiri??ni wakati sasa kuigomea serikali hii onevu kwa walalahoi na nguvu ya umma itumike. Tusikae kimya kwa kuwa nyumba zetu hazijaguswa, tukemee hili kwa kuwa kuna uonevu kwa wananchi wasio na hatia.