GE2025 Wananchi Siha wakataa maandamano ya Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Its Tesha

Senior Member
Joined
Oct 6, 2025
Posts
168
Reaction score
604
Wananchi wa Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro wamepinga wito wa kufanya maandamano tarehe 29 Oktoba, wakisisitiza kuwa wanataka kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu.

Wakizungumza wakati wa kampeni za Mgombea Ubunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mollel, wananchi hao wamesema watajitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kupiga kura ya urais, lakini hawatashiriki maandamano yoyote.

Hadi sasa, Dkt. Mollel ametembelea vijiji 56 kati ya 60 vilivyopangwa, na anatarajiwa kukamilisha ziara yake katika vijiji vinne vilivyosalia ndani ya siku mbili zijazo.

Katika mikutano yake, Dkt. Mollel amesisitiza wananchi wa Siha kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, akieleza kuwa uongozi wake umeleta mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakisubiri kutangazwa kwa tarehe mpya ya uchaguzi wa ubunge, kufuatia kifo cha mgombea kupitia Chama cha CAFU.

Dkt. Mollel ameeleza dhamira ya CCM kuendeleza miradi ya maendeleo katika maeneo ya elimu, afya, maji safi na miundombinu, ili kuhakikisha wananchi wa Siha wanaendelea kunufaika na matunda ya serikali ya awamu ya sita.
 
Sio wananchi,Sema WanaCCM tena wasio na akili
 
D9 inarudiwa

Back
Top Bottom