Wananchi Mtwara Mjini wafanya maandamano makubwa kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!

Nimeangalia taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku maandamano hayo hayakuonyeshwa. Kuna anayejua yameonyeshwa katika TV ipi?
 
Mhhhhhh...who is behind the mobilisation?
-People themselves?
-Local goverments?
-Central goverment??
-Oppositions?
-Agencies?
-NGO's
?????????
Kama wayasemayo ni ya kweli na haki, inabaki ni ukweli na haki ni haki, bila kujali nani kasema.
 
Watu wa Mtwara hawana maana hiyo wanachotaka uzalishaji wote ufanyike huko ili wapate ajira na mapato yatakayotokana na rasilimali yao, nakuuliza swali la kizushi hivi gesi tuliyoanza kutumia tangu zamani ilikuwa inazalishwa maeneo tuliyokuwa au ilikuwa inapatikana kutoka sehemu nyingine na hata nje ya nchi?

Mkuu hebu niambie kijana aliyeko mitaani huko Mtwara atapata ajira gani kwenye power station (mtambo wa kuzalisha umeme)? Kulinda mitambo au? Jibu la swali lako ni kwamba gesi tuliyokuwa tunatumia ilikuwa imported kutoka nje ya nchi.
 
Naomba na ajitokeze mtu na aeleze faida ya Gesi ya Mtwara kubaki Mtwara...

Pia aeleze hasara za gesi ile kupelekwa katika miji mingine kama Darisalama....Kwa watu wa Darisalama, kwa watu wa Mtwara na Kwa Watanzania wote....


you are very igno, tunataka plant iwe mtwara na kama ni kusambaza ianze na tentatively baby steps around mtwara, lindi, songea inasogea taratibu mpaka musoma, sio kipenga cha gesi kinapulizwa mala long pass mpaka dsm tena bagamoyo, huu ni ukuda haukubaliki.
 
Sijui yameoneshwa wapi haya maandamano maana hata heading ya TBC sijaona kitu
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

we bwe,ge kweli..haki haiombwi hata siku moja,inapiganiwa we kama unamaslahi na magamba basi endelea kubwabwaja.haki inapiganiwa haiombwi kenge wewe.
 
asalaam aleykum,

hivi leo tumeamka na kusikia habari kuu ya maandamano ya kulinda rasilimali huko mtwara,

kwamba gesi ya mtwara ijali kwanza maslahi ya waamtwara, NA WOTE WAISHIO NDANI YAKE..

mimi nawaunga mkono kwa asilimia 200 % nauita huu ni mwisho wa viinimacho na mwanzo mzuri wa tanzania mpya,,,

sijui ni nani aliwafundisha utundu huu wanamtwara, lakini wanaingia katika vitabu vya historia kama manamapinnduzi wa ukweli wa tanzania...

wenye nia ya kuleta maendeleo ya ukweli, yenye usawa na fursa nyingi kwa nchi nzima...

je ni yanini kuua wanaGEita, na Wanatarime, kisa unaitamani na kuichimba BLOODY GOLD?

huku ukiwaacha wanamaeneo yao masikini hohe hae wa kutupwa? kila siku kuwapiga risasi na kuwafunika mashimoni?

je mbona zile habari za kuchukua minara ya dhahabu kwa wakuu wetu kutoka kwenye migodo kila wakati zinajirudia? japokuwa wamedhibiti zsana kamera siku hizi? si juzi wamebeba kule geita? wakiwwaachia wananchi mashimo? haya anayeweza akane tetesi hii...kwamba kila wiki geita inatoa tani ya dhahabu? na ndege zinapakiza mzigo bila kuwa audited?

mikataba inasainiwa mahotelini uingereza, pasenti zinashukia uswisi kwenye akaunti za vigogo, serekali inapata pasenti chache....na yenyewe inaishia kununua ma shangingi na kufunga viyoyozi masaki?

watoto weto wakisomea ardhini, chini ya miti, na wengi wa watanzania kuwa wasioshiba kila siku? ni kwanini lakini? NI KWA SABABU WANAONUFAIKA NA MIKATABA SIO WALE WANAOATHIRIKA NA UVUNAJI HUU HARAMU...

sasa imetosha na tusemem basi.....UDALALI SASA BASI!!!!

kwani mnadhani ni kwanini Zanzibar wamewachukia watanganyika? ni hasa baada ya kugundua mafuta na kujua kabisa dili zote zitakuwa wizi mtupu!!!! wenyewe wametamka hadharani kuwa so far hakuna hata fisadi mmoja aliyetokea visiwani...

ndio maana wako moto kutaka kuanza kufukua urani bila kuwa na sera, kwa sababu wao hawaishi Bahi...

na suala la watoto kuzaliwa na kende moja halitawahusu ...kwani watakuwa dar es salaam......ilihali akaunti zao zinapumua uswisi......

sasa basi nitawarudisha darasani... nani aliwahi sikia sera za maendeleo za mipango mikoa RIDEPS? NA KWANINI ZILIKUFA?

NITAWAELEZA, maendeleo kwa falsafa ya mipango uwiano huzingatia sana rasilimali zilizopo pahala (endowment)..... zitumike kuwatoa watu wa pahala pale, ile waweze kushiriki moja kwa moja katika maendeleo ya mikoa.....na hatimaye taifa...

naam hiyo ndiyo dawa pekee, hata ukienda australia hata uk hata USA hiyo hadi leo inatumika....

yaani Integrated Development Planning.......

leo watu wa mtwara wamekuwa na gesi, mwaipora, watoto wao wakaajiriwe wapi? mtwara ichangamke lini? kwa faida ya nani?

nitarudi kwa sera za majimbo, CHADEMA ni sera yao....na wameihubiri sana,,,CCM wamewaita wakabila....na kama kawaida yao wananchi wengi watanzania ambao ni mavuvuzela wanashangilia.... sasa mavuvuzela yameamka...

chadema walisema tanzania iwe na majimbo manane...jimbo la kati ni dodoma, mororogo na singida....

chakula cha eneo hili, madini ya eneo hili, rasilimali za eneo hili zitatumika kuendeleza eneo hili..

si uchoyo bali ndio falsafa pekee inayoweza kufanya kazi kati nchi zilizojaa ufisadi..

na zile zinazotaka kusonga mbele...

mbona marekani, ukienda florida wako vizuri,,,,,ukienda misisipi...wako vizuri....ukienda teenese..wako vizuri...na sie tubadilike..........

mbona afrika kusini wana serekali za majimbo? na mabunge yake? na pia serekali kuu.......

tubadilike....tunahitaji kubadili mfumo wa siasa na utawala wa saasa....toka ule wa kikoloni unaokandamiza maendeleo....

hadi huu wa majimbo unaokuza maendeleo...na iingizwe kwenye katiba mpya


watanzania tuache siasa...tufanye kaziiiiiiii tujiletee mendeleo...

karibuni kuunga siredi!

Kaka umenena kabisa...
 
Hii siyo tanzania tena, kama hili nalo tunaliona kama ni sawa. Hivi kweli gesi izalishwe hapo na itumike hapo hapo? kweli? hatuangalii hata mifano toka kwa nchi zilzoendelea? siasa gani hizi za kudumaza vichwa vya watanzania na kuanza kuona maandamano kama staili ya kutafuta haki?
Ni Tanzania hii hii. Katiba yetu inasema:
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania toleo la 1977

Ibara ya 18 (a) inasema, Kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake.


Ibara ya 20 (1) inasema, Kila mtu anao uhuru wa kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika, kushirikiana na watu wengine na kwa ajili hiyo kutoa mawazo yake hadharani na kuanzisha na kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
Walichofanya watu wa Mtwara ni haki yao ya kikatiba. Labda utuambie unatumia sheria gani wewe.

Msingi muhimu wa kuanzisha miradi ulipuuzwa, ambao ni kushirikisha wananchi wa eneo husika katika mipango, na kuhakikisha maslahi yao yanazingatiwa.
 
..... Haijaniingia akilini... wanaandamana kuzuia gas isije Dar? inaamaana ikija Dar itaisha wao watakosa au? Hapo najiuliza iwapo kila mkoa utaamua kuzuia mali zilizoko katika maeneo yao ingekuwaje katika Tz? .....

Hii ndio inavotakiwa kila mkoa ujiendeshe ili kupunguza wezi kupeleka uswiz,na itapunguza wakimbiz kuja dar watu wengi watabakia mikoani kwakua ajira zitakuweko.
 
Hivi kuna nini na vyombo Vya habari Vya walamba miguuu?.....naona ITV...hawajatoa hii habari kabisa.....we need Nation TV in Tanzania.
Gesi-bagamoyo
Bandari- bagamoyo
Airport-bagamoyo
EPZ-bagamoyo

Mtwara
Reli-hamisha
Bandari ya asili- uwa kabisa
Gesi- nyonya
Mafuta-fyonza

Duuuuuuuuuuu!
 
Hili sasa linahitaji kuzungumzwa kitaifa (Bungeni) na kuwekewa utaratibu wa kisheria na Serikali ijipange kutoa shule katika kila ngazi ya utawala ili lieleweke once and for all.

Ni kweli kuwa mahala palipo na rasilimali kama hizi lazima wapate unafuu fulani kutokana na rasilimali hizo na tumeshasikia faida kama hizo huko kusini na hata katika maeneo yanayozunguka Hifadhi za Taifa, Migodi n.k. ingawa si clear fidia/ unafuu uwe wa kiwango gani kwa wenyeji watakaofaidi hiyo faida na pia kudefine wenyeji wanaostahili kupata hiyo faida (targeted beneficiaries) ni akina nani hasa (Kijiji / Mtaa au Kata au Tarafa au Wilaya au Mkoa ).

Pamoja na yote hayo; kusema kuwa rasilimali zote za mahala hapo ni zao pekee ni upotofu mkubwa sana maana hili likiruhusiwa basi hatutakuwa na Nchi- Tanzania bali tutakuwa na Mikoa au Wilaya au Vijiji vyenye rasilimali na vitapaswa vijiendeshe vyenyewe kwa hiyo rasilimali yao tu kitu kisichowezekana.
Fikiri Kilimanjaro waseme fedha za utalii kuupanda Mlima Kilimanjaro zote ziwe zao; Wilaya ya Serengeti au Mara nao waseme hivyo kuhusu Serengeti National Park na Ngorongoro – Ngorongoro CA , na mikoa yote yenye madini na makumbusho ya kitaifa na uzalishaji wa mazao waseme hivyo tutakuwa Taifa la aina gani?

Kusafirisha gesi kuelekea katika eneo la viwanda vingi si kitu cha ajabu duniani kibiashara; kinachotakiwa ni kuhakikisha tu kuwa Mikoa yote yenye rasilimali hizo inapata takwimu sahihi ya kile kinachopatikana katika uzalishaji au faida ya huduma husika ili asilimia iliyopatikana kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na Bunge ibaki kunakohusika.
 
Mkuu iyo kwenye nyekundu bado sana mkuu, hivi kweli unategemea mtu anayeishi kwenye nyumba ya nyasi apikie gesi? Au watu mnajisemea tu. Tuna safari ndefu ya kuboresha maisha ya watu kwanza na ndo waanze kupikia gesi nyumbani. na je wengine wasitumie gesi hiyo mpaka maisha ya watu wa Mtwara yatakapoboreshwa waweze kutumia gesi ndo ipelekwe kwingineko? Give me a break.

Ok let me give you a break by forcing common sense into your head: Kuna kitu kinaitwa 'strategic planning'. Unabuni mkakati ambao utatekelezwa kwa hatua hadi mwisho ndani ya kipindi fulani. Swala la wananchi wetu kuishi nyumba za nyasi leo mwaka 2013 ni swala la kujitakia na makusudi kwa upande wa serikali na siyo wananchi.
Kama ungekuwepo mfumo wa utawala unaotumia malighafi za wananchi husika kwa mipango ya maendeleo yao ya msingi, basi ujue tangu leo kwamba nyumba za nyasi mikoani zingetoweka hatua kwa hatua. Tanzania kwa miaka mingi sasa hatujawa na serikali zenye kufanya kazi kwa kufuata strategic planning na matokeo yake hata wewe unayaona kwenye makazi, afya, elimu, ajira, uzalishaji, n.k.
Hakuna anayesema gesi ibaki Mtwara tu, kinachozungumziwa ni uzalishaji na processing vibaki Mtwara na sisi wengine tuipate gesi kwa kuipokea kupitia miundombinu.
I guess I have given you the break you asked for.
 
Tatizo watawala wa hii nchi wanajua Tanzania ni Dar es salaam. Mikoa mingine ni wasindikizaji tu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
hivi kuna nini na vyombo vya habari vya walamba miguuu?.....naona itv...hawajatoa hii habari kabisa.....we need nation tv in tanzania.
Gesi-bagamoyo
bandari- bagamoyo
airport-bagamoyo
epz-bagamoyo

mtwara
reli-hamisha
bandari ya asili- uwa kabisa
gesi- nyonya
mafuta-fyonza

duuuuuuuuuuu!
korosho - kopa, kulipa kwa mbinde mpaka kituo cha polisi kichomwe moto
inaumiza sana.
 
Katika kipindi cha mwaka mmoja ulioyopita, Tanzania ilipata mkopo wa karibu sh. trilioni moja kutoka China kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar Es Salaam.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom