Wananchi Mtwara Mjini wafanya maandamano makubwa kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!

Ukiunganisha dot vizuri za haya Mabango utaona ni jinsi gani Bagamoyo inavyoididimiza Mtwara .
DSC02571.JPG
 
Tutake tusitake, gas ni mali ya wananchi wa Mtwara na Tanzania kwa ujumla, maamuzi yoyote makubwa yahusuyo matumizi ya gas hiyo wananchi wa mtwara wanapaswa kushirikishwa. na hili haswa ndo lililokuwa dhumuni la MWL NYERERE kuwapatia wananchi wake ile elimu ya ngumbaru, lengo likiwa kufuta ujinga. ndo maana mwananchi leo hii bila kujali elimu yake anakuwa na hoja ya msingi cha maana MSIKILIZE usimpuuze , viongozi wetu leo hii wanatuona hatuna cha kuchangia sisi ni watu wa kuburuzwa wanafikiri kwa ajili yetu, hawana muda wa kutushirikisha mawazo yetu na akili zetu ,zinaishia kwenye kuwapigia kura. fedha zinazokusanywa maeneo mbalimbali pamoja na akiba za pesa za kigeni zinaishia ktk kujilipa masurufu ya safari kwa viongozi , wamekwenda mara kadhaa kukagua mradi huo wamejilipa mamilioni ya fedha kwa kutuandalia madudu kwa kutowashirikisha wananchi kwenye maamuzi .kwa elimu yetu ya ngumbaru tuone barabara ya ajabu toka DAR kwenda MTWARA kwenye gas. tuone ukarabati mkubwa wa bandari kwa ajili ya gas, tuone umeme wa uhakika MTWARA tuone mashule na mahospitali ya Mtwara yakiwa na madawa, waalimu na vifaa kwa ajili ya gas.na mambo yote mazuri yanayofikiriwa kuwekwa DAR kutokana na gas yawekwe MTWARA.
 
Kimya kingi kinamshindo mkubwa, wenye kuendelea kuwakashifu watu wa Mtwara waendelee. Watu wa Mtwara wanadai haki yao ya kiraia ya kufaidi raslimali ya ardhi waliyozaliwa. Hawana pengine pa kwenda na wala haiwezekani eti chakula kipikwe Mtwara walaji wawe sehemu nyingine bila wao kuonja hata punje.
 
akili zako hazina akili na je huko bagamoyo kuna watumiaji wengi si ndio?

JK anasema Dar imejaa mkoa wa Pwani watenge eneo la viwanda. Pwani ikijaa Morogoro. Kigoma, Mara lini? Mungu wangu we, hakukuwa na mantiki kuweka Bandari Bagamoyo, why not Tanga na Mtwara?
 
Jambo la msingi wakazi wa Ntwara waache gesi ije darisalama ila serikali ihakikishe kuwa kila kipato kitakachopatikana kutokana na gesi hiyo bac Ntwara nao wafaidike kwa namna moja au nyingine, for Gods sake ni mali asili yao so wanapaswa kunufaika kwayo.
 
Kuna wapuuzi wachache wanaotumia hoja kuwa Mtwara hakuna maendeleo kiasi cha kulazimisha gesi kusindikwa pale na mitambo kujengwa pale. Kwani wanaosababisha maendeleo ni kina nani kama si watu? kwani dar ya leo ni sawa na ya 1961? Mtwara imebarikiwa kwa mengi ikiwa ni pamoja na bahari, ardhi safi, na nchi jirani. kwa mtaji huu sera ya majimbo irudi tu maana kwa kigezo cha 'keki ya Taifa' watu wana misbehave
 
Hivi hiyo gesi ikibaki mtwara bila kupelekwa Dar ndo itawafaidia nini? Rasilimali ni vizuri ikajulikana ni za nchi wala siyo mkoa, wilaya au kanda. Kama Mtwara ungekuwa jiji lenye watu wengi na matumizi makubwa na fursa ya kutumia gesi ikapelekwa Dar na kuacha Mtwara hapo kungekuwa na tatizo.
Mji unakua kutokana na kuwepo kwa fursa za kiuchumi. Mtwara kuna bandari kama ilivyo Dsm na kiwanda chochote kinaweza kujengwa pale na kuweza kusafirisha product zake nje ya nchi kirahisi. Kama issue ni kuwa na umeme wa uhakika Dar, kwa nini wasipeleke umeme badala ya gesi? Wananchi wa Mtwara wako sahihi kabisa maana vijana hawana ajira na gesi ikibakia Mtwara viwanda vitajengwa Mtwara na watu watapata ajira.
 
bravo wamakonde, saa ya mabadiliko ni sasa. viwanda vya kuzalisha umeme vikiwekwa mtwara nafasi za ajira kwa wanamtwara watazipata na ukuaji wa mji utakuwep
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom