Mkuu nakuunga mkono kwa hoja yako! Dar imejaa, haikaliki sasa hivi kwa sababu ya kulundika kila kitu huko! Maendeleo yawafuate watu na sio watu wanyang'anywe rasilimali kisha waanze kuzifuata Dar!
Maslahi ya kitaifa unayoongelea wewe ni yapi zaidi ya haya ya kuwawezesha wananchi kwa kutumia rasilimali za Nchi?
Tatizo sio kutompelekea mlaji..tatizo hapa ni kwa nini production isifanyike mtwara walau wananchi wa huko waambulie hata ajira ili waweze kuendesha maisha yao!.....
MAFILILI: CHADEMA inahusika vipi tena hapo we ukilala ukiamka unawaza CHADEMA tu, wao wamekwambia GAS kwanza vyama na siasa baadaye.
=Thesi;5315429]Hivi hiyo gesi ikibaki mtwara bila kupelekwa Dar ndo itawafaidia nini? Rasilimali ni vizuri ikajulikana ni za nchi wala siyo Mkoa, Wilaya au kanda. Kama Mtwara ungekuwa jiji lenye watu wengi na matumizi makubwa na fursa ya kutumia gesi ikapelekwa Dar na kuacha Mtwara hapo kungekuwa na tatizo.
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu
Good move kama wameruhusiwa...but waangalie wasivunje tu sheria!
Mahitaji yenu ni kiasi gani? Kuna uhaba kiasi gani?
Mimi mwenzenu mgumu kuelewa, hebu nisaidie tafsiri ya hii kauli "Gesi haitoki Mtwara NG'O"
Ina maana dhahabu zinazochimbwa Kahama, zisitoke Kahama, Almasi za Mwadui zinabaki Mwadui?
Maharage yakitoka Mbeya kwenda Mtwara, sisi wa Dar tunatakiwa tuchaji kodi ya barabara?
Shida imeanzia kwenye kuelimisha wananchi nini kinafanyika na wao wanafaidikaje.'production' gani unazungumzia maana mpaka sasa inafanyikia Mtwara. Ikiwa ni matumizi ya product - yaani gas - si raisi kwa idadi yote kutumika Mtwara, ndiyo maana lazima ingine iwe 'exported' kwa walaji wengine. Sasa Mtwara wadai mapato ya hii 'exportation' na siyo kuzuia. Hii inahitaji kubadili mfumo wetu wa utawala na uchumi.
MAFILILI ,Acha kutuona sisi Maboya narudia tena ,wewe unataja tu majina ya watu na vyeo vyao,mbona hao unaowataja hatuwaoni wakizungumza lolote kuhusu hii Saga?,Huyo M bunge Murji amefuatwa Ofisini kwake awaoneshe wana Mtwara Mkataba wa kusafirisha Gas anasema hata yeye hana (ukumbuke huyu ndiye aliyesema wana Mtwara wamekubari Gas iondoke tu hawana tatizo) ,Mayor hana majibu yoyote,Hiv MAFILILI hawa watu wanakupa nini wewe?
wameanza jitambua hapo!vzur wamakonde.
Sidhani, watu wamepigika sana kimaisha na wamekata tamaa. Pia wameshapewa ahadi nyingi sana za uongo.Naamini kunawatu hapa kwenye maandamano ukiwauliza wanaandamana kwa sababu gani utasikia sijui nimeona watu wanaadnamana na mimi nikaunga.